-
Danieli 5:23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
23 Badala yake, ulijikweza mwenyewe dhidi ya Bwana wa mbinguni,+ ukawaamuru wakuletee vyombo vya nyumba yake.+ Kisha wewe pamoja na wakuu wako, masuria wako, na wake zako wadogo mkavitumia kunywea divai na kuisifu miungu ya fedha na ya dhahabu, ya shaba, chuma, miti, na mawe, miungu ambayo haioni chochote na haisikii chochote na haijui chochote.+ Lakini hujamtukuza Mungu ambaye pumzi yako na njia zako zote zimo mikononi mwake.+
-
-
Matendo 12:21-23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Siku moja iliyochaguliwa, Herode alivaa mavazi ya kifalme akaketi kwenye kiti cha hukumu na kuanza kuwahutubia watu wote. 22 Ndipo watu waliokusanyika wakaanza kusema kwa sauti kubwa: “Hii ni sauti ya mungu, si ya mwanadamu!” 23 Papo hapo, malaika wa Yehova* akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu, naye akaliwa na wadudu akafa.
-