17 Ee Yehova, ni kweli kwamba wafalme wa Ashuru wameharibu mataifa na nchi zao.+18 Nao wameitupa miungu yao motoni, kwa sababu haikuwa miungu+ bali kazi ya mikono ya wanadamu,+ miti na mawe. Ndiyo sababu waliweza kuiangamiza.
15 Sasa msiache Hezekia awadanganye au kuwapotosha hivyo!+ Msimwamini, kwa maana hakuna mungu yeyote wa taifa lolote au ufalme aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka mikononi mwangu na kutoka mikononi mwa mababu zangu. Basi, Mungu wenu atawezaje kuwaokoa ninyi kutoka mikononi mwangu?’”+