Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wafalme 25:4-7
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 4 Sehemu ya ukuta wa jiji ilibomolewa,+ na wanajeshi wote wakakimbia wakati wa usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, wakati Wakaldayo walipokuwa wakilizingira jiji; naye mfalme akafuata njia inayoelekea Araba.+ 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha. 6 Kisha wakamkamata mfalme+ na kumpeleka mpaka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla, nao wakamhukumu. 7 Wakawachinja wana wa Sedekia huku akitazama; kisha Nebukadneza akampofusha macho Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba, na kumpeleka Babiloni.+

  • Yeremia 52:7-11
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 7 Mwishowe sehemu ya ukuta wa jiji ikabomolewa, na wanajeshi wote wakakimbia kutoka jijini wakati wa usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, wakati Wakaldayo walipokuwa wakilizingira jiji; nao wakafuata njia inayoelekea Araba.+ 8 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia Sedekia+ katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha. 9 Kisha wakamkamata mfalme na kumpeleka mpaka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akamhukumu. 10 Na mfalme wa Babiloni akawachinja wana wa Sedekia huku Sedekia akitazama, na pia akawachinja wakuu wote wa Yuda huko Ribla. 11 Kisha mfalme wa Babiloni akampofusha macho Sedekia,+ akamfunga kwa pingu za shaba, akampeleka Babiloni, na kumfunga gerezani mpaka siku aliyokufa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki