-
2 Wafalme 22:12, 13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Halafu mfalme akamwagiza hivi kuhani Hilkia, Ahikamu+ mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, mwandishi Shafani, na Asaya mtumishi wa mfalme: 13 “Nendeni mkatafute ushauri wa Yehova kwa niaba yangu, kwa niaba ya watu, na kwa niaba ya watu wote wa Yuda kuhusu maneno ya kitabu hiki ambacho kimepatikana; kwa maana ghadhabu ya Yehova iliyowaka dhidi yetu ni kali,+ kwa sababu mababu zetu hawakutii maneno ya kitabu hiki kwa kuyashika mambo yote yaliyoandikwa kutuhusu.”
-
-
Yeremia 39:13, 14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Basi Nebuzaradani mkuu wa walinzi, Nebushazbani yule Rabsarisi,* Nergal-shareza yule Rabmagi,* na wakuu wote wa mfalme wa Babiloni wakawatuma watu 14 wamtoe Yeremia katika Ua wa Walinzi+ na kumkabidhi kwa Gedalia+ mwana wa Ahikamu+ mwana wa Shafani+ ili apelekwe nyumbani kwake. Basi akaishi pamoja na watu wengine.
-
-
Yeremia 40:5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Hata kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akamwambia: “Rudi kwa Gedalia+ mwana wa Ahikamu+ mwana wa Shafani,+ ambaye mfalme wa Babiloni amemweka juu ya majiji ya Yuda, nawe ukae pamoja naye miongoni mwa watu; au uende popote unapotaka.”
Ndipo mkuu wa walinzi akampa posho ya chakula na zawadi, akamruhusu aende zake.
-