Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wafalme 25:5-7
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha. 6 Kisha wakamkamata mfalme+ na kumpeleka mpaka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla, nao wakamhukumu. 7 Wakawachinja wana wa Sedekia huku akitazama; kisha Nebukadneza akampofusha macho Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba, na kumpeleka Babiloni.+

  • Yeremia 52:8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia Sedekia+ katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha.

  • Yeremia 52:11
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 11 Kisha mfalme wa Babiloni akampofusha macho Sedekia,+ akamfunga kwa pingu za shaba, akampeleka Babiloni, na kumfunga gerezani mpaka siku aliyokufa.

  • Ezekieli 12:12, 13
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 12 Mkuu aliye miongoni mwao atabeba mizigo yake begani na kuondoka kukiwa na giza. Atatoboa shimo ukutani na kuibeba mizigo yake kupitia humo.+ Ataufunika uso wake ili asione chini.’ 13 Nitautandaza wavu wangu juu yake, naye atakamatwa katika wavu wangu wa kuwindia.+ Kisha nitampeleka Babiloni, kwenye nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona; naye atafia huko.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki