33 “Tazama! Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa binadamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi. Nao watamhukumia kifo na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa, 34 nao watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua, lakini baada ya siku tatu atafufuka.”+