Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 14:66-72
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 66 Sasa Petro alipokuwa chini katika ua, mmoja wa wajakazi wa kuhani mkuu akaja.+ 67 Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama moja kwa moja na kusema: “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 Lakini akakana, akisema: “Simjui wala sielewi unachosema.” Kisha akatoka na kuelekea langoni.* 69 Yule kijakazi alipomwona akaanza tena kuwaambia wale waliosimama hapo: “Huyu ni mmoja wao.” 70 Petro akakana tena. Baada ya muda mfupi, wale waliosimama hapo wakaanza tena kumwambia: “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana, wewe ni Mgalilaya.” 71 Lakini akaanza kulaani na kuapa: “Simjui mtu huyu mnayezungumza kumhusu!” 72 Papo hapo jogoo akawika mara ya pili,+ naye Petro akakumbuka maneno ambayo Yesu alimwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”+ Naye akalemewa akaanza kulia.

  • Luka 22:54-62
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 54 Ndipo wakamkamata,+ na kumpeleka nyumbani kwa kuhani mkuu; lakini Petro alikuwa akiwafuata kwa mbali.+ 55 Walipowasha moto katikati ya ua na kuketi chini pamoja, Petro alikuwa ameketi miongoni mwao.+ 56 Lakini kijakazi mmoja akamwona Petro akiwa ameketi kando ya moto, akamtazama kwa makini na kusema: “Mtu huyu pia alikuwa pamoja naye.” 57 Lakini Petro akakana, akisema: “Wewe mwanamke, mimi simjui.” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona na kusema: “Wewe pia ni mmoja wao.” Lakini Petro akasema: “Mimi si mmoja wao.”+ 59 Baada ya saa moja hivi kupita mwanamume mwingine akaanza kusisitiza kwa nguvu: “Kwa hakika mtu huyu pia alikuwa pamoja naye, kwa maana, yeye ni Mgalilaya!” 60 Lakini Petro akasema: “Wewe mtu, mimi sielewi unachosema.” Mara tu alipokuwa akisema, jogoo akawika. 61 Ndipo Bwana akageuka, akamtazama Petro moja kwa moja, naye Petro akakumbuka maneno ambayo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.”+ 62 Naye akaenda nje akalia kwa uchungu.

  • Yohana 18:15-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 15 Sasa Simoni Petro na mwanafunzi mwingine wakamfuata Yesu.+ Mwanafunzi huyo alijulikana na kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu ndani ya ua wa kuhani mkuu, 16 lakini Petro alikuwa amesimama nje kwenye mlango.* Basi yule mwanafunzi mwingine, aliyejulikana na kuhani mkuu, akatoka nje na kuzungumza na mlinzi wa mlango, akamwingiza Petro ndani. 17 Basi kijakazi, aliyekuwa mlinzi wa mlango, akamuuliza Petro: “Wewe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu, sivyo?” Petro akajibu: “Hapana.”+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki