-
Mathayo 26:69-75Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
69 Basi Petro alikuwa ameketi nje katika ua, kijakazi akamjia na kumwambia: “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mgalilaya!”+ 70 Lakini akakana mbele yao wote, akisema: “Sijui unachosema.” 71 Alipoenda kwenye chumba kilicho langoni, msichana mwingine akamwona na kuwaambia wale waliokuwa hapo: “Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.”+ 72 Akakana tena akiapa: “Simjui mtu huyo!” 73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesimama hapo wakaja na kumwambia Petro: “Hakika wewe pia ni mmoja wao, kwa maana matamshi* yako yanakutambulisha.” 74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa: “Simjui mtu huyo!” Na mara moja jogoo akawika. 75 Naye Petro akakumbuka maneno aliyosema Yesu, yaani: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”+ Naye akaenda nje akalia kwa uchungu.
-
-
Luka 22:55-62Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
55 Walipowasha moto katikati ya ua na kuketi chini pamoja, Petro alikuwa ameketi miongoni mwao.+ 56 Lakini kijakazi mmoja akamwona Petro akiwa ameketi kando ya moto, akamtazama kwa makini na kusema: “Mtu huyu pia alikuwa pamoja naye.” 57 Lakini Petro akakana, akisema: “Wewe mwanamke, mimi simjui.” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona na kusema: “Wewe pia ni mmoja wao.” Lakini Petro akasema: “Mimi si mmoja wao.”+ 59 Baada ya saa moja hivi kupita mwanamume mwingine akaanza kusisitiza kwa nguvu: “Kwa hakika mtu huyu pia alikuwa pamoja naye, kwa maana, yeye ni Mgalilaya!” 60 Lakini Petro akasema: “Wewe mtu, mimi sielewi unachosema.” Mara tu alipokuwa akisema, jogoo akawika. 61 Ndipo Bwana akageuka, akamtazama Petro moja kwa moja, naye Petro akakumbuka maneno ambayo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.”+ 62 Naye akaenda nje akalia kwa uchungu.
-
-
Yohana 18:25, 26Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama hapo akiota moto. Ndipo wakamwambia: “Wewe pia ni mmoja wa wanafunzi wake, sivyo?” Akakana na kusema: “Hapana.”+ 26 Mmoja wa watumwa wa kuhani mkuu, aliyekuwa mtu wa ukoo wa yule aliyekatwa sikio+ na Petro, akasema: “Nilikuona katika bustani pamoja naye, sivyo?”
-