-
Mathayo 26:69-75Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
69 Basi Petro alikuwa ameketi nje katika ua, kijakazi akamjia na kumwambia: “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mgalilaya!”+ 70 Lakini akakana mbele yao wote, akisema: “Sijui unachosema.” 71 Alipoenda kwenye chumba kilicho langoni, msichana mwingine akamwona na kuwaambia wale waliokuwa hapo: “Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.”+ 72 Akakana tena akiapa: “Simjui mtu huyo!” 73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesimama hapo wakaja na kumwambia Petro: “Hakika wewe pia ni mmoja wao, kwa maana matamshi* yako yanakutambulisha.” 74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa: “Simjui mtu huyo!” Na mara moja jogoo akawika. 75 Naye Petro akakumbuka maneno aliyosema Yesu, yaani: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”+ Naye akaenda nje akalia kwa uchungu.
-
-
Marko 14:66-72Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
66 Sasa Petro alipokuwa chini katika ua, mmoja wa wajakazi wa kuhani mkuu akaja.+ 67 Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama moja kwa moja na kusema: “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 Lakini akakana, akisema: “Simjui wala sielewi unachosema.” Kisha akatoka na kuelekea langoni.* 69 Yule kijakazi alipomwona akaanza tena kuwaambia wale waliosimama hapo: “Huyu ni mmoja wao.” 70 Petro akakana tena. Baada ya muda mfupi, wale waliosimama hapo wakaanza tena kumwambia: “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana, wewe ni Mgalilaya.” 71 Lakini akaanza kulaani na kuapa: “Simjui mtu huyu mnayezungumza kumhusu!” 72 Papo hapo jogoo akawika mara ya pili,+ naye Petro akakumbuka maneno ambayo Yesu alimwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”+ Naye akalemewa akaanza kulia.
-
-
Yohana 18:18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Sasa wale watumwa na maofisa walikuwa wamesimama kuzunguka moto wa makaa waliokuwa wameuwasha, kwa sababu kulikuwa na baridi nao walikuwa wakiota moto. Petro pia alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
-