55 Walipowasha moto katikati ya ua na kuketi chini pamoja, Petro alikuwa ameketi miongoni mwao.+ 56 Lakini kijakazi mmoja akamwona Petro akiwa ameketi kando ya moto, akamtazama kwa makini na kusema: “Mtu huyu pia alikuwa pamoja naye.” 57 Lakini Petro akakana, akisema: “Wewe mwanamke, mimi simjui.”