Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 10:1
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 10 Basi akawaita wanafunzi wake 12 na kuwapa mamlaka ya kuwafukuza roho waovu+ na kuponya kila aina ya ugonjwa na kila aina ya udhaifu.

  • Luka 9:1-6
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Ndipo akawaita pamoja wale 12, akawapa nguvu na mamlaka ya kufukuza roho wote waovu+ na kuponya magonjwa.+ 2 Kisha akawatuma kuhubiri kuhusu Ufalme wa Mungu na kuponya, 3 akawaambia: “Msibebe chochote kwa ajili ya safari, wala fimbo wala mfuko wa chakula wala mkate wala pesa;* wala msiwe na mavazi mawili.*+ 4 Lakini mtakapoingia katika nyumba yoyote, kaeni humo mpaka mtakapoondoka huko.+ 5 Popote ambapo watu hawatawakaribisha, mnapotoka katika jiji hilo kung’uteni mavumbi yaliyo kwenye miguu yenu ili uwe ushahidi dhidi yao.”+ 6 Kisha wakaenda katika eneo hilo kutoka kijiji mpaka kijiji, wakitangaza habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki