-
Mathayo 9:23-26Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
23 Basi alipoingia katika nyumba ya yule mtawala na kuwaona watu waliokuwa wakipiga filimbi na umati uliokuwa na vurugu,+ 24 Yesu akasema: “Ondokeni hapa, kwa maana msichana huyu mdogo hajafa bali amelala usingizi.”+ Ndipo wakaanza kumcheka kwa dharau. 25 Mara tu umati ulipoondolewa, Yesu akaingia na kumshika mkono,+ kisha yule msichana mdogo akainuka.+ 26 Bila shaka, habari hiyo ilienea katika eneo hilo lote.
-
-
Marko 5:38-43Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
38 Wakafika kwenye nyumba ya yule ofisa msimamizi wa sinagogi, Yesu akaona mvurugo wa watu waliokuwa wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa.+ 39 Baada ya kuingia, akawaambia: “Kwa nini mnaomboleza na kuleta mvurugo? Mtoto hajafa bali amelala usingizi.”+ 40 Ndipo wakaanza kumcheka kwa dharau. Lakini baada ya kuwatoa wote nje, akamchukua baba na mama ya yule mtoto pamoja na wanafunzi wake, akaingia mahali alipokuwa huyo mtoto. 41 Kisha akaushika mkono wa msichana huyo na kumwambia: “Talitha kumi,” maneno ambayo yanapotafsiriwa, yanamaanisha: “Msichana mdogo, ninakuambia, ‘inuka!’”+ 42 Mara moja yule msichana akasimama akaanza kutembea. (Alikuwa na umri wa miaka 12.) Ndipo wakawa na shangwe kubwa sana. 43 Lakini akawaagiza tena na tena* wasimwambie mtu yeyote kuhusu jambo hilo,+ naye akawaambia wampe mtoto huyo chakula.
-