Yeremia
47 Hili ndilo neno la Yehova kwa nabii Yeremia kuwahusu Wafilisti,+ kabla ya Farao kushambulia Gaza. 2 Yehova anasema hivi:
“Tazama! Maji yanakuja kutoka kaskazini.
Yatakuwa mto unaofurika.
Nayo yataifunika nchi na kila kitu kilichomo,
Jiji na wale wanaokaa humo.
Wanaume watalia kwa sauti,
Na kila mtu anayeishi katika nchi ataomboleza.
3 Watakaposikia sauti ya kishindo cha kwato za farasi dume wake,
Watakaposikia kelele za magari yake ya vita
Na mvumo wa magurudumu yake,
Akina baba hata hawatageuka kuwatazama wana wao,
Kwa maana mikono yao italegea,
4 Kwa sababu siku inayokuja itawaangamiza Wafilisti wote;+
Itamwangamiza kabisa kutoka Tiro+ na kutoka Sidoni+ kila msaidizi aliyebaki.
Ashkeloni limenyamazishwa.+
Utanyamaza mpaka lini?
Rudi ndani ya ala yako.
Pumzika na unyamaze.
7 Upanga unawezaje kukaa kimya
Wakati Yehova ameuamuru?
Ushambulie Ashkeloni na pwani ya bahari,+
Hapo ndipo alipoupa kazi.”