Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wimbo wa Sulemani 5
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Wimbo wa Sulemani—Yaliyomo

    • MSHULAMI AKIWA YERUSALEMU (3:6–8:4)

Wimbo wa Sulemani 5:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, vikolezo.

Marejeo

  • +Wim 4:16
  • +Wim 4:13, 14
  • +Wim 4:11
  • +Wim 1:2

Wimbo wa Sulemani 5:2

Marejeo

  • +Wim 3:1
  • +Lu 2:8

Wimbo wa Sulemani 5:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Nafsi yangu ilizimia.”

Marejeo

  • +Wim 3:1, 3

Wimbo wa Sulemani 5:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “shela yangu.”

Wimbo wa Sulemani 5:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “vishada vya tende.”

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Amkeni!,

    1/8/1997, uku. 25

  • Fahirishi ya Machapisho

    g97 1/8 25

Wimbo wa Sulemani 5:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2015, uku. 30

    11/15/2006, uku. 19

    11/15/1987, uku. 25

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 19

Wimbo wa Sulemani 5:13

Marejeo

  • +Wim 6:2
  • +Wim 1:13

Wimbo wa Sulemani 5:14

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/2006, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 19

Wimbo wa Sulemani 5:15

Marejeo

  • +Zb 92:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/2006, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 19

Wimbo wa Sulemani 5:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Kaakaa lake.”

Marejeo

  • +Wim 2:3

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Wim. 5:1Wim 4:16
Wim. 5:1Wim 4:13, 14
Wim. 5:1Wim 4:11
Wim. 5:1Wim 1:2
Wim. 5:2Wim 3:1
Wim. 5:2Lu 2:8
Wim. 5:6Wim 3:1, 3
Wim. 5:13Wim 6:2
Wim. 5:13Wim 1:13
Wim. 5:15Zb 92:12
Wim. 5:16Wim 2:3
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Wimbo wa Sulemani 5:1-16

Wimbo wa Sulemani

5 “Nimeingia katika bustani yangu,+

Ewe dada yangu, bibi harusi wangu.

Nimekusanya manemane yangu na viungo* vyangu.+

Nimekula sega langu na asali yangu;

Nimekunywa divai yangu na maziwa yangu.”+

“Kuleni, rafiki zangu wapendwa!

Kunyweni, mlewe maonyesho ya upendo!”+

 2 “Nimelala usingizi, lakini moyo wangu uko macho.+

Ndiyo hiyo sauti ya mpenzi wangu akipiga hodi!”

“Nifungulie, ewe dada yangu, mpenzi wangu,

Njiwa wangu, mpenzi wangu asiye na kasoro!

Kwa maana kichwa changu kimelowa umande,

Mashungi ya nywele zangu yamejaa unyevu wa usiku.”+

 3 “‘Nimevua kanzu yangu.

Ni lazima niivae tena?

Nimeosha miguu yangu.

Ni lazima niichafue tena?’

 4 Mpenzi wangu aliondoa mkono wake kwenye tundu la mlango,

Hisia zangu kumwelekea zikasisimka.

 5 Niliinuka ili nimfungulie mpenzi wangu;

Mikono yangu ikadondosha manemane,

Na vidole vyangu manemane ya maji,

Ikadondoka kwenye vitasa vya mlango.

 6 Nilimfungulia mpenzi wangu,

Lakini mpenzi wangu alikuwa ameondoka, alikuwa ameenda zake.

Nilitamauka* alipoenda.

Nilimtafuta, lakini sikumpata.+

Nikamwita, lakini hakuitika.

 7 Nilikutana na walinzi waliokuwa wakizunguka jijini.

Wakanipiga na kunijeruhi.

Walinzi wa kuta wakanivua mtandio wangu.*

 8 Nawaapisha, enyi binti za Yerusalemu:

Mkimpata mpenzi wangu,

Mwambieni naugua kwa mapenzi.”

 9 “Mpenzi wako ni bora kuliko wapenzi wengine wote jinsi gani,

Ewe mwanamke mrembo kuliko wote?

Mpenzi wako ni bora kuliko mpenzi mwingine yeyote jinsi gani,

Hivi kwamba unatuapisha hivyo?”

10 “Mpenzi wangu anang’aa tena ni mwekundu;

Anavutia zaidi miongoni mwa wanaume elfu kumi.

11 Kichwa chake ni dhahabu, dhahabu bora zaidi.

Mashungi ya nywele zake ni kama majani ya mtende yanayotikisika.*

Nywele zake ni nyeusi kama kunguru.

12 Macho yake ni kama njiwa kando ya vijito vya maji,

Wanaooga ndani ya maziwa,

Wakiwa wameketi kando ya dimbwi lililojaa maji.

13 Mashavu yake ni kama kitalu cha viungo,+

Vilima vya mimea yenye manukato.

Midomo yake ni mayungiyungi, yanayodondosha manemane ya maji.+

14 Mikono yake ni fito za dhahabu, zilizopambwa kwa krisolito.

Tumbo lake ni pembe ya tembo iliyong’arishwa na kufunikwa kwa yakuti.

15 Miguu yake ni nguzo za marumaru zilizowekwa kwenye vikalio vya dhahabu bora zaidi.

Sura yake ni kama Lebanoni, kama mierezi isiyo na kifani.+

16 Kinywa chake* ni utamu mtupu,

Na kila kitu kumhusu kinatamanika.+

Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye mpendwa wangu, enyi binti za Yerusalemu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki