Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 29
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Agano pamoja na Waisraeli kule Moabu (1-13)

      • Onyo kuhusu kutotii (14-29)

        • Mambo yaliyofichwa, mambo yaliyofunuliwa (29)

Kumbukumbu la Torati 29:1

Marejeo

  • +Kut 24:8

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 520

Kumbukumbu la Torati 29:2

Marejeo

  • +Kut 19:4; Yos 24:5

Kumbukumbu la Torati 29:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “majaribu makubwa ambayo.”

Marejeo

  • +Kum 4:34; Ne 9:10

Kumbukumbu la Torati 29:4

Marejeo

  • +Ro 11:8

Kumbukumbu la Torati 29:5

Marejeo

  • +Kum 1:3; 8:2
  • +Kum 8:4; Ne 9:21; Mt 6:31

Kumbukumbu la Torati 29:7

Marejeo

  • +Hes 21:26
  • +Hes 21:33
  • +Zb 135:10, 11

Kumbukumbu la Torati 29:8

Marejeo

  • +Hes 32:33; Kum 3:12, 13

Kumbukumbu la Torati 29:9

Marejeo

  • +Kum 4:6; 8:18; Yos 1:7, 8; 1Fa 2:3; Zb 103:17, 18; Lu 11:28

Kumbukumbu la Torati 29:11

Marejeo

  • +Ne 8:2
  • +Kut 12:38

Kumbukumbu la Torati 29:12

Marejeo

  • +Kum 1:3; 29:1

Kumbukumbu la Torati 29:13

Marejeo

  • +Kut 19:5; Kum 7:6; 28:9
  • +Kut 6:7; 29:45
  • +Mwa 17:1, 7; 22:16, 17
  • +Mwa 26:3
  • +Mwa 28:13

Kumbukumbu la Torati 29:16

Marejeo

  • +Kum 2:4

Kumbukumbu la Torati 29:17

Maelezo ya Chini

  • *

    Huenda neno la Kiebrania linahusiana na neno “mavi,” nalo hutumiwa kuonyesha dharau.

Marejeo

  • +Hes 25:1, 2

Kumbukumbu la Torati 29:18

Marejeo

  • +Kum 11:16; Ebr 3:12
  • +Ebr 12:15

Kumbukumbu la Torati 29:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kitu kilichonyweshwa maji vizuri pamoja na kitu kilichokauka.”

Kumbukumbu la Torati 29:20

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “chini ya mbingu.”

Marejeo

  • +Yos 24:19
  • +Kum 27:26; 28:15

Kumbukumbu la Torati 29:23

Marejeo

  • +Mwa 19:24; Yud 7
  • +Mwa 10:19; 14:2

Kumbukumbu la Torati 29:24

Marejeo

  • +1Fa 9:8, 9; 2Nya 7:21, 22; Yer 22:8, 9

Kumbukumbu la Torati 29:25

Marejeo

  • +1Fa 19:10
  • +Yer 31:32

Kumbukumbu la Torati 29:26

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “hakuwapa.”

Marejeo

  • +Amu 2:12

Kumbukumbu la Torati 29:27

Marejeo

  • +Law 26:16; Kum 27:26

Kumbukumbu la Torati 29:28

Marejeo

  • +Kum 28:45, 63; 1Fa 14:15; 2Fa 17:18; Lu 21:24
  • +Ezr 9:7; Da 9:7

Kumbukumbu la Torati 29:29

Marejeo

  • +Ro 11:33
  • +Zb 78:5; Mhu 12:13

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/1987, uku. 31

    5/15/1986, kur. 10-15

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 29:1Kut 24:8
Kum. 29:2Kut 19:4; Yos 24:5
Kum. 29:3Kum 4:34; Ne 9:10
Kum. 29:4Ro 11:8
Kum. 29:5Kum 1:3; 8:2
Kum. 29:5Kum 8:4; Ne 9:21; Mt 6:31
Kum. 29:7Hes 21:26
Kum. 29:7Hes 21:33
Kum. 29:7Zb 135:10, 11
Kum. 29:8Hes 32:33; Kum 3:12, 13
Kum. 29:9Kum 4:6; 8:18; Yos 1:7, 8; 1Fa 2:3; Zb 103:17, 18; Lu 11:28
Kum. 29:11Ne 8:2
Kum. 29:11Kut 12:38
Kum. 29:12Kum 1:3; 29:1
Kum. 29:13Kut 19:5; Kum 7:6; 28:9
Kum. 29:13Kut 6:7; 29:45
Kum. 29:13Mwa 17:1, 7; 22:16, 17
Kum. 29:13Mwa 26:3
Kum. 29:13Mwa 28:13
Kum. 29:16Kum 2:4
Kum. 29:17Hes 25:1, 2
Kum. 29:18Kum 11:16; Ebr 3:12
Kum. 29:18Ebr 12:15
Kum. 29:20Yos 24:19
Kum. 29:20Kum 27:26; 28:15
Kum. 29:23Mwa 19:24; Yud 7
Kum. 29:23Mwa 10:19; 14:2
Kum. 29:241Fa 9:8, 9; 2Nya 7:21, 22; Yer 22:8, 9
Kum. 29:251Fa 19:10
Kum. 29:25Yer 31:32
Kum. 29:26Amu 2:12
Kum. 29:27Law 26:16; Kum 27:26
Kum. 29:28Kum 28:45, 63; 1Fa 14:15; 2Fa 17:18; Lu 21:24
Kum. 29:28Ezr 9:7; Da 9:7
Kum. 29:29Ro 11:33
Kum. 29:29Zb 78:5; Mhu 12:13
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 29:1-29

Kumbukumbu la Torati

29 Haya ndiyo maneno ya agano ambalo Yehova alimwamuru Musa afanye pamoja na Waisraeli katika nchi ya Moabu, mbali na agano alilofanya nao kule Horebu.+

2 Kisha Musa akawaita Waisraeli wote na kuwaambia, “Mmeona mambo yote ambayo Yehova alifanya mbele ya macho yenu katika nchi ya Misri, mambo ambayo alimtendea Farao na watumishi wake wote na nchi yake yote,+ 3 hukumu kubwa ambazo* macho yenu yaliona, zile ishara kubwa na miujiza.+ 4 Lakini mpaka leo hii Yehova hajawapa moyo wa kuelewa na macho ya kuona na masikio ya kusikia.+ 5 ‘Nilipokuwa nikiwaongoza kwa miaka 40 nyikani,+ nguo mlizovaa hazikuchakaa na viatu mlivyovaa havikuchakaa miguuni mwenu.+ 6 Hamkula mkate wala kunywa divai wala kinywaji chochote chenye kileo, ili mjue kwamba mimi ni Yehova Mungu wenu.’ 7 Mwishowe mkafika mahali hapa, na Sihoni mfalme wa Heshboni+ na Ogu mfalme wa Bashani+ wakaja kupigana nasi, lakini tukawashinda.+ 8 Baada ya hayo tukachukua nchi yao na kuwapa Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase iwe urithi wao.+ 9 Kwa hiyo, shikeni maneno ya agano hili na kuyatii, ili kila jambo mnalofanya lifanikiwe.+

10 “Leo ninyi nyote mmesimama mbele za Yehova Mungu wenu; viongozi wa makabila yenu, wazee wenu, maofisa wenu, kila mwanamume wa Israeli, 11 watoto wenu, wake zenu,+ na mkaaji mgeni+ anayeishi kambini mwenu, kuanzia mtu anayewakusanyia kuni mpaka anayewatekea maji. 12 Mko hapa ili mwingie katika agano la Yehova Mungu wenu na kiapo chake, agano ambalo Yehova Mungu wenu anafanya pamoja nanyi leo+ 13 ili leo awafanye ninyi kuwa watu wake+ na ili awe Mungu wenu,+ kama alivyowaahidi ninyi na kama alivyowaapia mababu zenu, Abrahamu,+ Isaka,+ na Yakobo.+

14 “Sasa sifanyi agano hili na kiapo hiki pamoja nanyi tu, 15 bali nafanya pamoja na ninyi mnaosimama hapa pamoja nasi leo mbele za Yehova Mungu wetu na pamoja na wale ambao leo hawapo hapa pamoja nasi. 16 (Kwa maana ninyi mnajua vizuri jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyopita katikati ya mataifa mbalimbali tulipokuwa safarini.+ 17 Nanyi mlikuwa mkiona vitu vyao vinavyochukiza na sanamu zao zenye kuchukiza*+ za miti na mawe, fedha na dhahabu, walizokuwa nazo.) 18 Jihadharini kusiwe na mwanamume au mwanamke, familia au kabila lolote kati yenu leo ambalo moyo wake utageuka na kumwacha Yehova Mungu wetu ili kwenda kuabudu miungu ya mataifa hayo,+ ili miongoni mwenu kusiwe na mzizi unaozaa tunda lenye sumu na pakanga.+

19 “Lakini mtu akisikia maneno ya kiapo hiki na kujigamba moyoni mwake akisema, ‘Nitakuwa na amani, ingawa ninasisitiza kwamba nitaendelea kutembea katika njia za moyo wangu mwenyewe,’ na hivyo kuharibu kila kitu* kilicho kwenye njia yake, 20 Yehova hatakuwa tayari kumsamehe.+ Badala yake, hasira kali ya Yehova itawaka dhidi ya mtu huyo, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki hakika itampata,+ na Yehova kwa kweli atafutilia mbali jina la mtu huyo kutoka duniani.* 21 Kisha Yehova atamtenga kutoka katika makabila yote ya Waisraeli ili apate msiba kulingana na laana yote ya agano iliyoandikwa katika kitabu hiki cha Sheria.

22 “Kizazi cha wakati ujao cha wana wenu na pia wageni kutoka nchi ya mbali watakapoona mapigo ya nchi, magonjwa ambayo Yehova ameleta juu yake— 23 kiberiti na chumvi na kuteketea, hivi kwamba nchi yote haitapandwa wala kuchipuza mimea, wala hakuna mmea wowote utakaoota ndani yake, kama ilivyokuwa wakati wa maangamizi ya Sodoma na Gomora,+ Adma na Seboiimu,+ majiji ambayo Yehova aliyaangamiza katika hasira yake na katika ghadhabu yake— 24 wao pamoja na mataifa yote watauliza, ‘Kwa nini Yehova aliitendea hivi nchi hii?+ Ni nini kilichomfanya awake hasira kali hivi?’ 25 Kisha watasema, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Yehova,+ Mungu wa mababu zao, ambalo alifanya pamoja nao alipowatoa nchini Misri.+ 26 Lakini walienda na kuabudu miungu mingine na kuiinamia, miungu ambayo hawakuwa wameijua na ambayo hakuwaruhusu waiabudu.*+ 27 Ndipo hasira kali ya Yehova ikawaka dhidi ya nchi hiyo, naye akailetea nchi hiyo laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki.+ 28 Kwa hiyo, Yehova akawang’oa kutoka katika ardhi yao kwa hasira yake+ na ghadhabu kali na hamaki na kuwapeleka katika nchi nyingine, mahali walipo mpaka leo.’+

29 “Mambo yaliyofichwa ni ya Yehova Mungu wetu,+ lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu na wazao wetu milele, ili tutekeleze maneno yote ya Sheria hii.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki