Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 27
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Wafilisti wampa Daudi Siklagi (1-12)

1 Samweli 27:1

Marejeo

  • +1Sa 19:18; 22:1, 5
  • +1Sa 18:29; 23:23

1 Samweli 27:2

Marejeo

  • +1Sa 25:13; 30:9
  • +1Sa 21:10, 14; 27:12

1 Samweli 27:3

Marejeo

  • +1Sa 25:43
  • +1Sa 25:39, 42

1 Samweli 27:4

Marejeo

  • +1Sa 23:14; 26:25

1 Samweli 27:6

Marejeo

  • +Yos 19:1, 5; 1Sa 30:1; 2Sa 1:1; 1Nya 12:1, 20

1 Samweli 27:7

Marejeo

  • +1Sa 29:3

1 Samweli 27:8

Marejeo

  • +Yos 13:1, 2
  • +Mwa 36:12; Kut 17:8, 14; Hes 13:29; 1Sa 15:2; 2Sa 1:1
  • +Mwa 25:17, 18; Kut 15:22; 1Sa 15:7

1 Samweli 27:9

Marejeo

  • +Kum 25:19; 1Sa 15:3

1 Samweli 27:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Dhidi ya Negebu ya.”

Marejeo

  • +Yos 15:1, 2
  • +1Nya 2:9
  • +Hes 24:21; 1Sa 15:6

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

1 Sam. 27:11Sa 19:18; 22:1, 5
1 Sam. 27:11Sa 18:29; 23:23
1 Sam. 27:21Sa 25:13; 30:9
1 Sam. 27:21Sa 21:10, 14; 27:12
1 Sam. 27:31Sa 25:43
1 Sam. 27:31Sa 25:39, 42
1 Sam. 27:41Sa 23:14; 26:25
1 Sam. 27:6Yos 19:1, 5; 1Sa 30:1; 2Sa 1:1; 1Nya 12:1, 20
1 Sam. 27:71Sa 29:3
1 Sam. 27:8Yos 13:1, 2
1 Sam. 27:8Mwa 36:12; Kut 17:8, 14; Hes 13:29; 1Sa 15:2; 2Sa 1:1
1 Sam. 27:8Mwa 25:17, 18; Kut 15:22; 1Sa 15:7
1 Sam. 27:9Kum 25:19; 1Sa 15:3
1 Sam. 27:10Yos 15:1, 2
1 Sam. 27:101Nya 2:9
1 Sam. 27:10Hes 24:21; 1Sa 15:6
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
1 Samweli 27:1-12

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

27 Hata hivyo, Daudi akasema moyoni mwake: “Siku moja mkono wa Sauli utaniua. Jambo bora la kufanya ni kukimbilia+ nchi ya Wafilisti; halafu Sauli atakata tamaa ya kunitafuta katika eneo lote la Israeli,+ nami nitaponyoka kutoka mkononi mwake.” 2 Basi Daudi akaondoka pamoja na wanaume 600+ waliokuwa naye, akavuka kwenda kwa Akishi+ mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi. 3 Daudi na wanaume wake wakakaa na Akishi huko Gathi, kila mwanamume na familia yake. Daudi alikuwa na wake zake wawili, Ahinoamu+ wa Yezreeli na Abigaili+ Mkarmeli, mjane wa Nabali. 4 Sauli alipoambiwa kwamba Daudi alikuwa amekimbia kwenda Gathi, aliacha kumtafuta.+

5 Ndipo Daudi akamwambia Akishi: “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, naomba unipe mahali katika mojawapo ya majiji ya mashambani, ili niishi huko. Kwa nini mimi mtumishi wako niishi pamoja nawe katika jiji hili la kifalme?” 6 Basi Akishi akampa Siklagi+ siku hiyo. Ndiyo sababu tangu siku hiyo Siklagi limekuwa jiji la wafalme wa Yuda.

7 Daudi aliishi katika eneo la mashambani la Wafilisti kwa muda wa mwaka mmoja na miezi minne.+ 8 Daudi alikuwa akipanda pamoja na wanaume wake kuwavamia Wageshuri,+ Wagirzi, na Waamaleki,+ kwa maana walikuwa wakikaa katika nchi iliyoanzia Telamu mpaka Shuri+ na kushuka mpaka nchi ya Misri. 9 Daudi alipokuwa akiishambulia nchi, hakumwacha hai mwanamume wala mwanamke yeyote,+ bali alichukua kondoo, ng’ombe, punda, ngamia, na mavazi, kisha alirudi kwa Akishi. 10 Na Akishi alipokuwa akimuuliza: “Ulivamia wapi leo?” Daudi alimjibu: “Upande wa kusini wa* Yuda”+ au “Upande wa kusini wa Wayerahmeeli”+ au “Upande wa kusini wa Wakeni.”+ 11 Daudi hakumwacha hai mwanamume au mwanamke yeyote ili wasiletwe Gathi, kwa kuwa alisema: “Wasije wakawaambia habari zetu wakisema, ‘Hivi ndivyo Daudi alivyofanya.’” (Alizoea kufanya hivyo muda wote alioishi katika eneo la mashambani la Wafilisti.) 12 Kwa hiyo Akishi akamwamini Daudi akisema moyoni mwake: “Bila shaka ananuka miongoni mwa watu wake wa Israeli, kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu sikuzote.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki