Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 11/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1991
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1990
  • Napaswa Kufanya Nini Watu Wakipiga Porojo Kuhusu Mimi?
    Amkeni!—1990
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 11/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Porojo Karibu mwaka mmoja uliopita, mimi nikawa mhanga mwenye kufanyiwa porojo zenye kudhuru. Niliudhika na kuumia hisia hapo kwanza, lakini baba yangu na mimi tukafuatilia porojo hiyo na kuikomesha siku hiyo hiyo. Makala hiyo (Machi 8, 1990) ilinisaidia kuuondolea mbali uwongo huo mbaya sana.

P. M., United States

Mimi nina umri wa miaka 17, na watu fulani walipiga porojo juu yangu. Usiku mmoja niliona mmoja wao, nisijue la kufanya. Nilipofika nyumbani, niliiona makala juu ya porojo. Nilimshukuru Yehova kwa moyo kwa kujibu sala zangu. Nilijifunza jinsi ya kushughulika na watu wa jinsi hiyo na nikaona kwamba sipaswi kujichukua kwa uzito mno. Ingawaje, mimi si wa maana sana hivi kwamba wao wataongea juu yangu muda wote uliobaki wa maisha yangu, na lililo la maana zaidi ni kwamba rafiki zangu halisi na Yehova wajua kwamba mambo waenezayo si ya kweli. Asanteni kwa kuyajua mahitaji ya vijana!

L. U., Brazili

Chakula Salama Mimi hutumikia nikiwa mhudumu anayesafiri wa Mashahidi wa Yehova, nikiandamana na mke wangu. Hatupendi kuwalemea wakaribishaji wetu kwa sheria nyingi juu ya kutunza chakula, kwa hiyo sisi huwa katika uwezekano wa kupatwa na matatizo ya kuyeyusha chakula tumboni. Mwaweza kuwazia jinsi makal hii (Aprili 8, 1990) imekuwa yenye msaada kwetu! Kwa kweli sisi twawashukuru kwa kufikiria kila jambo lililo jema kwa watu wa Mungu.

R. P., Venezuela

Kifo Chauzwa Kila jambo lililoandikwa katika makala yenu (Machi 8, 1990) lilikuwa lenye kuarifu na la kweli. Najua hivyo kwa sababu mimi nilivuta sigareti kwa zaidi ya miaka kumi. Tokeo: uchovu, kutoa jasho, na tabia ya ukali-ukali nilipokuwa sina tumbako. Niliamua kuacha kuvuta, lakini azimio langu likaendelea kwa miezi miwili tu. Muda fulani baadaye, nilianza kujifunza na Mashahidi wa Yehova na nikajifunza kutumia shauri la Biblia kwenye 2 Wakorintho 7:1, na mwishowe nikaacha. Karibuni natumainia kubatizwa kuwa Shahidi.

A. P., Hispania

Kuchelewa Nilithamini sana ile makala “Je! Wewe Huchelewa Sikuzote?” (Februari 8, 1990) Mlipendekeza kutazamia vipindi vya kungojea na kwenda na habari za kusoma ili kujishughulisha kwa njia yenye matokeo mazuri wakati wa kungojea wengine. Madokezo yenu yamethibitika kuwa yenye kutumika kweli kweli.

I. D., Naijeria

Historia ya Kidini Nina shukrani kwa ule mfululizo “Wakati Ujao wa Dini kwa Kutegemea Wakati Wayo Uliopita.” Mimi hukuta watu wenye malezi ya kidini ya namna mbalimbali. Makala hizi zitawasaidia wafuatilie asili ya dini tangu mwanzo hadi sasa.

D. S., United States

Mimi nausoma mfululizo juu ya historia ya kidini. Hakika nimejifunza mengi, mengi kuliko niliyopata kujifunza shuleni.

B. J., United States

Watoto Wanaokufa Mjukuu wangu wa kike mwenye umri wa miezi kumi alilemewa na ugonjwa wa kuhara. Hospitali ilimwambia aende nyumbani, na hali yake ikawa mbaya zaidi kila siku. Mimi niliikumbuka makala yenu juu ya kuokoa watoto kwa kutumia Matibabu ya Kurudisha Maji Mwilini Kupitia Mdomoni. (Mei 8, 1990) Nilifuata maagizo hayo, na kesho yake akaanza kuimarika tena. Mharo ulisimama, naye akapona kabisa.

R. M., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki