Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 5/8 uku. 31
  • Matusi Yaliyo Kwenye Muziki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matusi Yaliyo Kwenye Muziki
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
  • Je, Nihudhurie Maonyesho ya Roki?
    Amkeni!—1995
  • Roki ya Badala—Je, Inanifaa?
    Amkeni!—1996
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 5/8 uku. 31

Matusi Yaliyo Kwenye Muziki

“KUSUDI kuu la bendi za roki—kuudhi wazazi wengi iwezekanavyo—ni mgawo unaozidi kuwa mgumu katika ustaarabu unaozidi kukosa adabu kila siku,” zikasema habari za karibuni katika U. S. News & World Report. Lilionyesha, hata hivyo, kwamba bendi za roki nyingine zashinda huu “mwito wa kushtua walio na ganzi” kwa kutumia lugha yenye utovu ajabu—si katika miziki yao tu bali hata katika majina wanayojichagulia. Gazeti hilo liliripoti: “Sasa kuna angalau bendi 13 zilizo na majina ya viungo vya uzazi vya kiume, 6 zenye jina la viungo vya uzazi vya kike, 4 zenye jina la shahawa, 8 zenye jina la utoaji-mimba na moja yenye jina la ambukizo fulani la uke.” Liliongezea kwamba ukaguzi mmoja umepata angalau bendi kumi zilizoitwa majina ya “matendo mbalimbali ya ngono” na sita zenye jina la matapiko. Ni kweli, vingi vya vikundi si vile vikubwa-vikubwa hasa, lakini uvutano wavyo waweza kuhisiwa.

Katika Florida, U.S.A., korti ilitangaza kuwa yenye matusi sahani moja ya santuri ya bendi ya kikundi cha roki kiitwacho “2 Live Crew.” Sahani hiyo, kulingana na mmoja wa wachambuzi wayo, ilikuwa na “maelezo 87 ya ngono ya kutumia mdomo, mitajo 116 ya viungo vya uzazi vya kiume na kike na vifungu vingine vya kishairi vyenye kutaja mitoko ya shahawa.” Baadaye uamuzi wa korti ulikatiwa rufani na kubatilishwa. Hata hivyo, mwenye duka la rekodi alikamatwa na baadaye akapatikana na hatia akapigwa faini ya dola 1,000 kwa mashtaka ya matusi kwa kuiuza sahani ya santuri hiyo. Mawakili wake walipanga kuikatia rufani kesi hiyo.

Si kila mtu anayeudhiwa na matusi haya, hata hivyo. Katika The Olympia, gazeti moja la Washington State, U.S.A., mwandishi aliye mpitiaji wa habari alizungumza kwa hasira juu ya mchezo wa bendi yenye mdundo mkubwa. Alionyesha kwamba kikundi hicho ‘huenda kikawa kilifanya jambo lisilo na kifani’ kwa kutumia neno chafu la kutaja ngono wazi “zaidi ya mara 200 wakati wa maneno yacho yenye kutajwa-tajwa katikati ya wimbo. Umati uliitikia hivyo hivyo. Ilikuwa jioni ya matusi, na roki ya mtindo wa Kiamerika, na umati ulifurahi.” Alimalizia kwa kusema kwamba kikundi hicho “kilikuwa kizuri ajabu.”

Viwango vya baadhi ya miziki na wachambuzi wa siku hizi hakika ni kinyume sana cha shauri lenye hekima la Biblia: “Lugha yoyote mbaya haipaswi kupitia midomo yenu.” (Waefeso 4:29, The New English Bible) Wapenda muziki, wachanga kwa wakubwa, watafanya vizuri kuzuia matusi hayo yasipitie masikioni mwao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki