Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 7/8 kur. 23-25
  • Maajabu ya Sufi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maajabu ya Sufi
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Utumizi wa Karne Nyingi
  • ‘Kuupanda Mgongo wa Kondoo’
  • Kwa Nini Ni ya Ajabu Sana?
  • Kutoka kwa Kondoo Hadi Kwako
  • Utunzi Mzuri kwa Maisha Marefu
  • Sufi ni ya Ajabu
  • Kufuga Kondoo Ndiyo Kazi Yetu
    Amkeni!—1993
  • Kushona Sweta—Katika Patagonia
    Amkeni!—1998
  • Huwalinda Kondoo Dhidi ya Mbwa-mwitu
    Amkeni!—1998
  • Zuru Bara, Zuru Kondoo!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 7/8 kur. 23-25

Maajabu ya Sufi

Na mleta habari za Amkeni! kutoka Australia

NI NINI chenye joto ya kustarehesha katika kipupwe lakini chenye ubaridi wenye kushangaza wakati wa kiangazi? Ni nini kilicho kigumu kuliko pamba, ilhali hufanyiza nyuzi nyepesi? Ni nini kilicho kingo la mtu mwenye kwenda juu ya theluji na yenye kumpendeza sana mbuni wa mitindo? Ni nini kinachoweza kunyooshwa karibu theluthi moja ya urefu wacho na kirudie urefu wacho kinapoachiliwa?

Jibu la maswali haya yote ni sufi—sufi yenye kufaa, yenye kudumu! Naam, koti lenye kustaajabisha la kondoo mwelekevu huandaa moja ya nyuzi zenye mafaa kwa kazi zozote zinazopatikana kwa mwanadamu.

Utumizi wa Karne Nyingi

Wavumbuzi wa mapema walipowasili Amerika Kusini, walipata wengi wa watu wake, kama vile Waperu, wakivaa mavazi ya sufi nzuri ya alpaka (mnyama aliye kama Kondoo). Hata huko nyuma zaidi, nyakati za kale za Biblia, makundi makubwa ya kondoo yalifugwa, na mavazi yenye kutiwa rangi yaliyotengenezwa na sufi yalifanyizwa.—Kutoka 26:1; Mambo ya Walawi 13:47.

Historia ya kisasa inakazia kondoo mnono wa Kihispania wa aina ya merino, ambaye hatokezi tu kwa utoaji wake wa sufi ya hali ya juu inayotegemeka sana, bali pia kwa ajili ya nguvu yake na uwezo wake wa kudumu katika hali za hewa zilizo mbaya. Merino mwenye nguvu alifaa sana kwa ajili ya hali ya hewa kavu ya Australia, bara lililo kisiwa la chini. Mwishoni mwa karne ya 18, waanzilishi wa koloni mpya walikuwa wanatafuta kitu zaidi ya chakula. Walihitaji bidhaa iliyofaa kuuzwa nje ya inchi ili kujenga uchumi.

Walichagua sufi kwa sababu hiyo hukua katika mnyama aliyehai. Kondoo zingetangatanga kwa vipindi virefu vya wakati, na kufanya kazi chache sana kulihitajiwa ili kutokeza sufi kwa wingi. Ingepakiwa kwa urahisi na haikuchakaa ghalani. Kuzuia kwake kuvu kungeiwezesha ivumilie safari ndefu ya miezi sita ya melini kuelekea Uingereza. Faida nyingine kubwa ya sufi ilikuwa ni kwamba haikuchomeka kwa wepesi.

‘Kuupanda Mgongo wa Kondoo’

Na hivyo, kwa karne moja na nusu baada ya merino za kwanza kuwasili katika 1797, Australia ilidumu kiuchumi hasa kwa sababu ya kusafirisha sufi nje ya nchi. Hata hivyo, kufuatia vita ya ulimwengu ya 1, kukiwa na maendeleo ya polepole ya viwanda vya baadaye, pamoja na utumizi wa kuongezeka wa vifaa vya kutengenezwa badala ya sufi, ule msemo wa kwamba Australia ilikuwa “inapanda mgongo wa kondoo” haukutumika sana. Yaani, hadi nusu ya mwisho wa miaka ya 80, wakati biashara ya sufi ya Australia iliingia katika usitawi wa ghafula usio na kifani. Wakati huo idadi ya kondoo za Australia ilifikia kuwa karibu milioni 166—zaidi ya kondoo 10 kwa kila mtu nchini, na utolewaji wa sufi wa kila mwaka ulikuwa umefikia zaidi ya tani 950,000.

Kufikia 1990, hata hivyo, usitawi huo ulipunguka. Uhitaji wa sufi ulipungua na ukaacha wafugaji kondoo wa Australia 70,000 wakiwa na kondoo wengi sana—karibu 20,000,000 zaidi ya kiasi, kulingana na gazeti Sunday Correspondent la London, England.

Kwa Nini Ni ya Ajabu Sana?

Kufaa kwa sufi kwa kazi yoyote katika mambo mengi na matumizi yake kwa hakika yanatokeza mshangao, kama vile sifa yazo kunavyoonyeshwa kifupi kwa thamani zayo. Sufi hukua katika njia ile ile ya nywele za kibinadamu, na aina nyingi za kondoo huwa na nywele ndefu zilizochanganyika pamoja na sufi yao. Hilo limetokezwa katika aina ya merino, ikiacha tu funiko la manyoya lenye kuenea mpaka chini ambalo ndilo lenye kutakwa sana. Ingawa sufi ni ngumu kuliko pamba au kitani, uzito wake wa chini hutoa nafasi ya mfanyizo wa nyuzi nyepesi. Uvutio wake mzuri wa rangi pia huongeza kufaa kwake kwa kazi yoyote. Ukimwona mwanamke mchanga amevaa kitambaa cha shingoni cha rangi ya nyekundu-nyangavu kinachopepeya vyepesi kwenye upepo, huenda kikawa cha sufi halisi.

Lakini je, umewahi kujaribu kukata kamba ya sufi kwa vidole vyako? Ngumu, sivyo? Ndiyo, uzi mmoja tu wa sufi waweza kukinza mvunjo wenye nguvu za kuanzia gramu 14 hadi 28—hivyo utahitaji makasi ili kukata nyuzi za sufi. Uzi wa sufi pia huwa na mikunjo, vipande vipande, ambavyo vinaifanya iwe yenye kupindika sana, na inaponyooshwa hadi asilimia 30 ya urefu wake, itarudia urefu wa kawaida inapoachiliwa. Ni sifa hii inayoifanya sufi iwe yenye kukinza makunjo inapokauka.

Zaidi ya hilo, ni ile hewa inayoshikiliwa ndani kati ya nyuzi za kipekee za sufi ambayo huiandalia sifa ya kuzuia joto kupita, ikiifanya iwe yenye ujoto wakati wa kipupwe lakini yenye ubaridi wakati wa kiangazi. Sehemu yake ya juujuu pia ni yenye kukinza maji ili kwamba fulana ya sufi yenye uchepechepe haitakufanya uhisi baridi sana kwa kukauka upesi sana, kama vile vitambaa vingine vingefanya. Zaidi ya yote, kondoo huivaa kila wakati katika hali zote za hewa na hawapatwi na mafua.

Huenda usitambue kwamba kitambaa gandamizo—kilicho na mamia ya matumizi, kutoka zulia hadi mipira ya kuchezea tenisi—kwa kweli ni sufi ambayo imegandamizwa chini ya joto na mbano. Na kitambaa cha sufi, kinachotumiwa kwa suti za wanaume na wanawake pamoja na nguo laini nzuri, hufanywa kutoka kwa sufi iliyosokotwa kwa njia fulani.

Kutoka kwa Kondoo Hadi Kwako

Katika nchi zenye kutoa sufi kwa wingi zaidi, vibanda vya kukata manyoya ni sehemu muhimu ya eneo la mashambani. Kwa kawaida, kondoo hukatwa mara moja kwa mwaka, lakini wakati wa kiangazi, kukata kwaweza kufanywa mara mbili kwa mwaka.

Wakataji manyoya ya kondoo ni wafanyakazi wenye nguvu, wenye mikono yenye misuli ya nguvu na migongo imara. Wakitumia makasi makubwa yenye nguvu, mkataji manyoya hunuia kuondoa funiko la manyoya likiwa sehemu moja. Mnyoaji stadi aweza kunyoa kondoo 200 kwa siku. Kwanza aondoa sufi ya tumboni, akianzia ndani ya miguu, kisha anasongea mgongoni, shingoni, na mabegani na chini kwenye upande ule mwingine. Sufi bora hutoka mabegani na sehemu za upande-upande za kondoo.

Kondoo waliokatwa manyoya karibuni wanapoachwa kutoka kibandani, ni jambo lenye kupendeza kuwaona wakiruka-ruka kwa shangwe wakiwa na uhuru mpya baada ya kutolewa makoti yao mazito.

Halafu, funiko la manyoya hupembuliwa na kupangwa kulingana na uzuri. Wapembuaji husimama kwenye vibao vya kufikia urefu wa kiunoni, wakichunguza sufi kuona uangavu, mikunjo, usafi, ulaini, wororo, na urefu. Mwainishaji stadi wa sufi aweza kupitia karibu kilo 4,500 za manyoya kwa juma. Halafu manyoya husafishwa na kukaushwa, na nta, au lanolini huondolewa. Sufi iliyokatwa kutoka kwa kondoo aliye hai ndiyo bora.

Utunzi Mzuri kwa Maisha Marefu

Labda hauhitaji kukumbushwa kwamba nondo hupenda sufi. Wao huzaa mayai yao ili kwamba viwavi waliotagwa karibuni wawe na chakula kingi. Wanapendelea sufi iliyo na ladha ya jasho au dutu zilizomwagika juu yayo. Kwa hiyo usiweke kabatini sufi au nguo za sufi zilizo chafu. Ikiwa unaweza kununua mavazi yasiyoweza kuathiriwa na nondo, huo ni ulinzi zaidi. Weka nguo za sufi mahali panapozuia hewa kuingia wakati huyavai mavazi hayo kwa ukawaida. Na hata nguo za sufi unazovaa mara nyingi zapasa kupanguswa kwa brashi na kukung’utwa kwa ukawaida, kwa kuwa sufi hupenda hewa.

Tekinolojia ya ki-siku-hizi imesaidia sana, kwa sababu leo sufi ambayo inauzwa na huwa imetibiwa ili kuzuia wadudu na kuvu na mara nyingi huwa imekung’utwa na haiwezi kushika moto. Bado, unahitaji kuwa mwangalifu unapoifua. Mashine nyingi za ki-siku-hizi za kufua nguo zina mzungusho wa sufi. Lakini ikiwa unaifua kwa mikono, suka-suka vazi hilo polepole mpaka liwe safi, ukifanya hivyo hali mikono yako ikiwa ndani ya maji, ambayo yapasa kuwa moto kidogo au baridi. Vifaa vya kufulia sufi kwa wazi ni vizuri kuliko sabuni, lakini ikiwa havipatikani, mumunyisha unga-unga wa sabuni yako kabla hujaanza. Usitumie dutu za kuondoa uchafu, kwa kuwa hizo kwa kawaida huwa za kialkali na zaweza kuharibu vazi. Tumia kadiri ya joto hiyohiyo kwa kusuza, ukihakikisha kwamba sabuni yote imetoka kwa kutumia maji safi mengi sana. Fingirisha vazi hilo lenye maji katika taulo na ukamue unyevu huo.

Mojapo ya faida za mavazi ya sufi ni kwamba mara nyingi hazihitaji kupigwa pasi. Hata hivyo ikiwa unataka umalizio wa ziada mwororo, tumia ama pasi ya mvuke au pasi pamoja na kitambaa chepechepe lakini tu baada ya vazi hilo kukauka kabisa. Mipigo myepesi ya pasi huzuia mng’aro asiotaka mtu yeyote na ni afadhali kuinua na kushusha pasi badala ya kuisukumiza.

Sufi ni ya Ajabu

Ni lazima kwa hakika ukubali kwamba sufi ni nguo yenye kusisimua. Kuanzia makoti hadi mipira ya tenisi, inatuandalia vifaa vyenye kudumu. Wakazi wa Australia wa mapema kwa kweli walifanya uchaguzi wa hekima kuchagua kondoo. Tunawashukuru sana kwa hilo tunapoendelea kufurahia karibu unamna-namna usio na mwisho wa vitu vinavyotengenezwa kwa kifaa hiki cha ajabu, sufi.

[Picha katika ukurasa wa 24]

Kabla ya kukata manyoya

Wakati wa kukata manyoya

Baada ya kukata manyoya

Kufurahia matokeo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki