Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/8 uku. 19
  • Mdundo wa Kifo Una Ujumbe Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mdundo wa Kifo Una Ujumbe Gani?
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Raha Isiyodhuru au Sumu ya Akili?
    Amkeni!—1993
  • Vyombo vya Ushetani Dawa za Kulevya na Muziki wa Vyuma Vizito
    Amkeni!—1994
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/8 uku. 19

Mdundo wa Kifo Una Ujumbe Gani?

MWANAMUME mchanga, mwenye macho ya kutisha, nywele ndefu, asimama mbele ya halaiki inayopiga vifijo na nderemo. Yeye achukua ndoo ikiwa imejaa damu na matumbo ya mnyama na kumwaga kwenye safu chache za kwanza. Mashabiki wacheka, nao wajipangusa, na kurushiana vipande vyayo. Mandhari hii, kulingana na St. Petersburg Times la Florida, ilitukia katika tafrija ya roki na bendi iitwayo Deicide, ambayo inamaanisha ‘uuaji wa mungu.’ Aina hii ya muziki inaitwa mdundo wa kifo, kwa kudhaniwa ndiyo aina ya mdundo mzito wa roki unaopita kiasi. Katika miaka ya karibuni umependwa sana katika Florida na kimataifa, tangu kufanikiwa kwa ile albamu yenye kichwa Scream Bloody Gore, na bendi iitwayo Death.

Bendi ya Deicide inaongozwa na Mwabudu wa Shetani aliyejitangaza wazi anayedai kuwa alimchukia Mungu tangu alipopata aksidenti iliyomwacha akiwa na kovu lililo na muundo wa J, ambalo ana uhakika kwamba lasimamia ama Jesus ama Jehovah. Yeye adai kusikia sauti zikimrairai ili ajiue, na alijichomelea alama ya kishetani katika kipaji chake.

Hata vikundi vya mkondo wa mdundo mzito hutoa jumbe zinazoashiria unyama. Gazeti la Time liliripoti kwamba albamu mbili za rekodi za kikundi cha mdundo mzito cha Guns N’ Roses ziliuza zaidi ya nakala milioni 1.5 kwa siku tatu. Walakini albamu hiyo yaendeleza kile Time yakiita “maneno ya bendi yasiyovumilika ya kingono na ujeuri” na “huendeleza ubaguzi wa wageni, ubaguzi wa rangi, na utesaji au ujitesaji wa kimwili ama kiakili.” Pia huimba nyimbo kama vile ngono ya mdomoni, uuaji wa binadamu, kuendeleza uchafu wa kiadili. Msururu wa maduka kadhaa yamekataa kuuza rekodi hizo.

Roki ya mdundo mzito, sawa na vile muziki wa rapu, zimeshutumiwa vikali—na si kutoka kwa washupavu wa kidini pekee na vikundi vya kisiasa vinavyoshikilia mambo mno; American Medical Association (AMA) na American Academy of Pediatrics pia yamezungumza dhidi ya hatari inayosababishwa na mitindo yote miwili ya muziki. Kulingana na gazeti la American Health, AMA laarifu hivi: “Jumbe zinazoonyeshwa na aina hususa za muziki wa roki huenda ziwe na madhara ya afya ya kimwili na hali njema ya kihisia-moyo kwa watoto na wabalehe wanaoweza kupatwa na madhara.”

Je, kweli aina hizi za muziki ni hatari? Ebu, fikiria vichwa vikuu sita vya habari vya rapu na midundo mizito vilivyo vya kawaida ambavyo AMA huona kuwa vyaelekea kudhuru: utumizi mbaya wa madawa na alkoholi, kujiua, jeuri, ibada ya shetani, kutumiwa vibaya kingono, na ubaguzi wa rangi. Je, vichwa kama hivyo vyaweza kuwa vyenye kujenga?—Linganisha Mithali 6:27, 28; Wafilipi 4:8.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki