Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 8/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Jeuri Iathiripo Nyumbani
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Ni Nini Husababisha Jeuri ya Nyumbani?
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 8/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Umaskini wa Magharibi Katika toleo lenu la Desemba 22, 1992, Kiingereza, makala moja katika “Kuutazama Ulimwengu” (“Watoto Maskini Katika Amerika”) ilisema hivi: “United States, mojapo nchi zenye utajiri zaidi katika ulimwengu, pia ni makao ya baadhi ya watoto maskini zaidi.” Hilo linapotosha. Kuna watoto maskini katika nchi nyingi ambao wangeona wengi wa watoto maskini wa Amerika kuwa matajiri. Kwa kweli ni msiba kwamba watoto wengi katika Amerika wanaumia. Lakini kukiwa na mali nyingi inayopatikana, ni kwa sababu ya kupuuzwa kwao kwenye aibu na wazazi wao.

W. H., United States

Ingawa hali mbaya sana za umaskini zaweza kuonekana katika United States, hatukumaanisha kudokeza kwamba kiwango cha maisha miongoni mwa wale wanaoonwa kuwa maskini katika nchi hiyo kwa ujumla ni kama kile cha walio maskini katika nchi nyinginezo. Jambo la kwamba umaskini wa kila aina upo katika nchi tajiri linashtua. Ni kweli kwamba watoto fulani huteseka kwa sababu ya kupuuzwa na wazazi. Hata hivyo, wazazi wengi hawana stadi zinazohitajika ili kufanya hali yao kuwa bora wala hawana namna ya kutafuta mali inayofurahiwa na wengine.—MHARIRI.

Jeuri ya Familia Nataka kuwashukuru sana kwa mfululizo “Je! Jeuri ya Familia Itakwisha Wakati Wowote?” (Februari 8, 1993) Kwa miaka 10 ambayo imepita ya ndoa yangu ya miaka 22, nimevumilia jeuri ya nyumbani. Kutendwa vibaya kiakili ndiko kubaya zaidi. Kwa njia iliyofichika, lakini yenye utaratibu, utu wako unaharibiwa kwa kiwango ambacho huwezi kuomba msaada. Nilifikia hatua ambayo hata niliwazia kujiua. Hatimaye nilimwacha mume wangu, nami naishi peke yangu. Lakini nimetiwa nguvu na kufarijiwa na makala katika gazeti lenu.

B. S., Ujerumani

Mama yangu hutendwa vibaya kimwili na baba yangu, na jambo hilo linatuhuzunisha sana sisi watoto watatu. Kila wakati anapompiga mama yangu, ni kana kwamba anatupiga. Ni wachache ambao kwa kweli wanaelewa jinsi ilivyo kuishi katika familia inayotawalwa na jeuri na chuki, ambamo hamna uelewano au upendo tena. Tunatiwa moyo kwa kujua kwamba kuna mtu anayetuelewa.

T. G. D. A., Italia

Inatia moyo sana kuona suala hilo likizungumzwa waziwazi. Nilivumilia miaka 14 nikiwa na mwenzi aliyekuwa akinitenda vibaya na aliyedai kuwa Mkristo. Mara nyingi niliambiwa kwamba nilihitaji kuepuka kumkasirisha. Hilo lilikuwa ni kuniuliza nifanye jambo lisilowezekana! Hatimaye, ilinibidi nimwache. Asanteni sana kwa makala hizo; zilikuwa zenye kutia moyo na zinaweza kusaidia wengine ambao hawajapata kupigwa, kupigwa teke, au kutemewa mate kuelewa makovu ya kihisia-moyo tunayobeba.

L. T., United States

Makala hizo zapenya moja kwa moja kwenye mioyo ya wanawake wengi ambao wamehisi upweke na kutengwa na wengine; hisia za woga na aibu zilitufanya tunyamaze. Mmetusaidia tuelewe kwamba tofauti na yale ambayo tumeshawishwa tuamini, hatukujiletea jambo hilo sisi wenyewe.

B. A., United States

Majuma kadhaa yamepita tangu nakala yangu ya Amkeni! ifike. Ilinibidi nisali mara nyingi ili niweze tu kulitoa gazeti hilo ndani ya kifuniko chalo na ikanichukua siku kadhaa kabla sijaweza kujilazimisha kulisoma. Asanteni sana kwa kuzungumzia suala hilo! Nilikuwa nikipatwa na jeuri ya nyumbani. Pindi moja mume wangu alinipiga kikatili nikiwa nimelala; ilihitaji nifanyiwe upasuaji wa kurekebisha umbo la vitefute vyangu. Niliweza kuponyoka kwa msaada wa polisi na familia moja ya Kikristo yenye fadhili iliyoishi karibu. Alihukumiwa kifungo cha miezi kadhaa katika jela. Sasa nimeolewa tena na mwanamume mzuri Mkristo.

P. H., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki