Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 8/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mchezo wa Hesabu
  • Pandikizi Linaloishi
  • Kamwe Si Mzee Mno
  • Kuondoa Barafu na Uchafuzi
  • Kioo cha Angani
  • Mahakama ya Ulaya Yaamua kwa Kupendelea Mashahidi Wagiriki
  • Ukoma Katika Italia
  • Misa kwa Ajili ya Wanyama
  • Deni la Usingizi
  • Dawa za Kuua Wadudu Zatisha Nchi ya Divai
  • “Kuishi Pekee”
  • Kwa Nini Kuna Mahakama ya Kimataifa Ulaya?
    Amkeni!—1996
  • Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Ugiriki
    Amkeni!—1997
  • Kulinda Kisheria Habari Njema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 8/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Mchezo wa Hesabu

Kwa miongo mingi ya miaka, vikundi vyenye kupigania haki za wagoni wa jinsia moja katika United States vimeshikilia kwamba wagoni wa jinsia moja wanafanyiza asilimia 10 ya idadi. Asilimia hiyo ya juu imekuwa msingi mzuri wa kutumia msongo wa kisiasa. Lakini hesabu ya asilimia 10, inayotegemea uchunguzi wa Alfred Kinsey juu ya ugoni wa kibanadamu katika miaka ya 1940 na 1950, hivi karibuni umekuja kuchunguzwa hata zaidi. Gazeti Newsweek laripoti hivi: “Uchunguzi wa karibuni zaidi waweka wagoni wa jinsia moja wa kiume na wa kike kuwa karibu katikati ya asilimia 1 na 6 ya idadi ya watu.” Ni kwa nini hesabu ya Kinsey ilikuwa ya juu sana? Inaonekana kwamba uchunguzi wake ulifanywa kwa sehemu kubwa katika mahali kama shule, magereza, na mahospitali, ambazo huenda zisiweze kuwakilisha idadi yote ya watu. Newsweek lamnukuu mwanasosholojia wa Chuo Kikuu cha Washington, Pepper Schwartz akisema hivi juu ya hesabu ya asilimia 10, “Hiyo si hesabu ya kweli.”

Pandikizi Linaloishi

Ni kitu gani ambacho ndicho kikubwa zaidi kinachoishi katika dunia yetu? Katika 1992 wengine walifikiri walikuwa wamepata kitu hicho: pandikizi la ukungu unaoenea katika eneo la hektari 12 kwenye sakafu ya msitu mmoja katika Michigan, U.S.A. Hata hivyo, jarida Nature hivi karibuni liliripoti juu ya kitu kingine ambacho huenda hata kingechukua nafasi ya kwanza: kikundi cha miti aspeni katika Utah. Miti hiyo yote hufanana, ikiwa na chembe za urithi zinazofanana. Kila moja ya mashina 47,000 hutokea kwenye mfumo mmoja wa mzizi. Dakt. Jeffry Mitton, mwanasayansi katika Chuo Kikuu cha Kolorado aeleza juu ya kikundi hicho kuwa kitu kimoja kinachoishi “ambacho kinaweza kihalisi kupanda juu ya milima na kuvuka mashamba ya majani.” Kinakadiriwa kuwa kinaenea eneo la hektari 43 na kuwa na uzani wa kilogramu milioni 6. Ingawa miti moja-moja katika kikundi hicho inaweza kuishi kwa wastani wa miaka 65, kiumbe hicho chenyewe kinaweza kuwa na umri wa maelfu ya miaka.

Kamwe Si Mzee Mno

‘Wewe si mzee mno usiweze kusoma.’ Kama kutoa kielelezo cha usemi huo wa zamani, Bernabé Evangelista, mwenye umri wa miaka 93, na mwenye uchangamfu, anatazamia kumaliza masomo yake ya chuo kikuu katika miaka miwili inayokuja. Anasomea usanii katika Chuo Kikuu cha Valencia, Uhispania, na ujitoaji wake kwa masomo yake tayari umempa tuzo la timizo kubwa la kimasomo. “Kujifunza ndiko kitu kizuri zaidi kilichopo,” aeleza Bernabé, anayefika katika chuo kikuu saa mbili ya asubuhi kila siku na mara nyingi huendelea na masomo yake ya jioni mpaka saa tatu ya usiku. Bernabé anaamini kwamba wazee wana nafasi nzuri sana ya kujifunza. “Ndiyo pindi ya maisha ambayo una wakati wa kufanya hivyo,” yeye asema. Mke wake aongezea kwamba kuendelea na utendaji kunampa kusudi katika maisha.

Kuondoa Barafu na Uchafuzi

Kuondoa barafu katika ndege na njia za ndege, jambo muhimu sana kwa urukaji salama wa safari za ndege, huleta matokeo yasiyo mazuri: uchafuzi. Gazeti la Uingereza New Scientist laripoti kwamba zaidi ya lita milioni 50 ya umaji-maji wa kuondolea barafu hutumiwa katika viwanja-ndege vya ulimwengu kila mwaka, na umaji-maji unaoenda kando mara nyingi huchafua maji ya chini na vijia vya maji, ukisababisha kuchanuka kwa mimea alga yenye sumu inayopunguza oksijeni na kuua samaki. Viwanja-ndege kadhaa vya Ulaya vimebuni njia zenye werevu za kukabili uchafuzi huo. Katika kiwanja-ndege cha Stockholm, magari yanayofanya kazi yakiwa kama visafishi vya kuvuta uchafu huondoa umaji-maji mwingi kupita kiasi kutoka kwenye ndege. Kiwanja-ndege cha Munich hutumia mashine kubwa sana inayopitia ndege kana kwamba inaiosha, ikinyunyiza umaji-maji huo na kukusanya umaji-maji unaokuwa mwingi kupita kiasi, ambao hutumiwa tena. Njia za ndege za Munich hukusanya masalio ya kikemikali, na kuzipitisha kupitia vijiwe na ukingo wenye changarawe uliofunikwa chini ya ardhi, ambapo masalio hayo huwekwa vijidudu vinavyoyavunja-vunja na kuyafanya yasidhuru.

Kioo cha Angani

Wazo linaloonekana kuwa hadithi ya kisayansi iliyotungwa tu kuliko kuonekana kuwa sayansi lilitokea kweli mwezi wa Februari uliopita wakati wanaanga wa Urusi walipoweka na kukunjua kioo chenye meta 20 katika kituo cha angani cha Mir chenye kuzunguka dunia. Baadhi ya wanasayansi wanapendekeza kwamba vioo katika anga vinaweza kutumiwa kuangaza nuru ya jua duniani wakati wa usiku, na hivyo kuokoa fedha za matumizi ya umeme na hata kuongeza wakati wa ukuzi wa mimea. Kioo hicho, kilichotengenezwa na Mylar (nyuzi za poliyesta ngumu), kiliangaza nuru ya jua duniani, ambapo watazamaji katika Urusi, Ufaransa, na Kanada waliripoti kuiona. Wanaanga Warusi waliona na kufuata nuru pana yenye kilometa nne iliyokuwa imeangazwa na kile kioo kwenye dunia yenye giza chini. Mhandisi mmoja katika mradi huo alitaja jaribio hilo kuwa fanikio na akapendekeza kwamba hatua nyingine iwe kioo cha meta 200 chenye mfumo wacho wenyewe wa kukiongoza.

Mahakama ya Ulaya Yaamua kwa Kupendelea Mashahidi Wagiriki

Mnamo Mei 25, 1993, Mashahidi wa Yehova walipata ushindi mkubwa wa kisheria katika uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, ambayo hukutana katika Strasbourg, Ufaransa. Kesi hiyo ilihusu Shahidi mmoja mwenye umri wa miaka 83, Minos Kokkinakis, ambaye alikuwa amehukumiwa kwa mashtaka ya kugeuza watu kidini kinyume cha sheria. Mnamo Machi 20, 1986, alihukumiwa kifungo cha miezi minne gerezani na mahakama ya jinai ya Lasithi katika Crete. Hata hivyo, maamuzi ya Mahakama ya Ulaya yalibadili hukumu hiyo kwa uamuzi wa mahakimu sita kwa tatu. Kwa miongo ya miaka mingi serikali ya Ugiriki, ikishawishwa sana na Kanisa Orthodoksi la Kigiriki, imefanya maelfu ya Mashahidi wa Yehova washikwe kwa mashtaka ya kugeuza watu kidini kinyume cha sheria. Katika kesi hiyo, Mahakama ya Ulaya ilipata kwamba serikali ya Ugiriki ilikuwa imevunja haki za Bw. Kokkinakis kinyume cha Mkataba wa Ulaya. Wale Mashahidi zaidi ya 26,000 katika Ugiriki wanatumaini kwamba uamuzi huo utamaliza mnyanyaso wao na kuwaruhusu waendelee na huduma yao kwa amani.

Ukoma Katika Italia

Ugonjwa wa kale wa ukoma, au ugonjwa wa Hansen, ungali unaendelea kuua watu katika Ulaya ya kisasa. Tarakimu za Wizara ya Afya zaonyesha kwamba katika Italia pekee, kuna watu wapatao 410 wanaougua ugonjwa huo, huku kukiwa na visa vipya vinne au vitano vikitokea kila mwaka. Katika mkutano mmoja juu ya utunzaji wa afya uliofanywa katika Lecco, Italia, ilifunuliwa kwamba katika miezi ya karibuni visa 20 vya ugonjwa huo vimepatikana miongoni mwa wahamiaji wanaotoka nchi zinazoendelea ambako ukoma umeenea. Kulingana na Antonio Sebastiani, mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na ya Kitropiki katika Chuo Kikuu cha La Sapienza, Rome, “bado kuna sehemu fulani katika Sardinia, Tuscany, na Liguria ambako ugonjwa huo bado unaendelea.”

Misa kwa Ajili ya Wanyama

Inaonekana kwamba wanyama wanapewa uangalifu zaidi na makasisi wa Italia. Kikundi cha kidini cha Wafransiska hivi karibuni kilishtaki Wayesuiti kuwa “wazushi” na “maadui wa vitu vilivyoumbwa” kwa sababu hao walisema kwamba wanyama “hawana uwezo wa kuonyesha upendo.” Askofu wa Katoliki Mario Canciani ataja maoni ya kanisa hivi: “Kanisa [Katoliki] linakaribisha viumbe vyote vilivyo hai.” Kwa hiyo, kulingana na gazeti la Italia La Repubblica, waenda-kanisani katika Rome kwa muda mrefu wameweza kupata baraka kwa ajili ya “rafiki zao wadogo wa nyumbani.” Likitangaza kisa kama hicho, gazeti hilo laeleza kwamba “pamoja na wale wanaoweza kuitwa kwa kufaa kuwa Wakristo, paka, mbwa, kasuku, sungura na jamii yote ya wanyama ambao kwa ajili yao baraka yatamaniwa wanaweza pia kuhudhuria misa.”

Deni la Usingizi

“Watu wanaokosa usingizi wanaweza kutembea, kusikia, na kuona kama watu wengine pia. Hata hivyo, utafiti waonyesha kwamba uwezo wa kutoa sababu, uwezo wa kufanya maamuzi na kubaki na akili iliyo chonjo hupunguzwa,” lasema gazeti Veja. Makala hiyo yananakili wastadi wanaoonya juu ya hatari ya kukosa usingizi unaohitajika. Uchunguzi uliofanywa na Dakt. Denis Martinez, msimamizi wa Shirika la Usingizi la Brazili, unaonyesha kwamba “aksidenti 2 kati ya kila 10 husababishwa na kutopata usingizi wa kutosha wakati wa usiku.” Dakt. Martinez aonya kwamba wale wasiopata usingizi wa kutosha, “kwa kielelezo, wale wanaofanya kazi tatu, . . . wanahatarisha tu afya yao kwa ajili ya kazi.”

Dawa za Kuua Wadudu Zatisha Nchi ya Divai

Katika eneo la Moselle la Ujerumani ya kati, linalotoa divai inayojulikana uliwenguni mzima, wafanyakazi wengi zaidi na zaidi wanaugua magonjwa ya neva. Kulingana na Peter Binz, mstadi wa neva kutoka Trier, watunza bustani, wakulima, na wafanyakazi wa misitu wanaonyesha dalili zilezile za ugonjwa huo. Pia kuna visa vingi vya kansa ya umio katika mwendo wa Bonde la Moselle. Ni kwa nini? “Kulingana na maoni ya Binz, kisababishi katika visa vingi ni matumizi ya dawa za kuua wadudu katika mashamba,” laripoti gazeti la Ujerumani Süddeutsche Zeitung. Uchunguzi mbalimbali umeonyesha kwamba “kufikia asilimia 90 ya madawa ya kuua wadudu yanayotawanyishwa kwa kunyunyizwa au kwa helikopta hugeuka kuwa hewa kwa muda wa saa chache na kupumuliwa na watu katika eneo hilo.”

“Kuishi Pekee”

“Wakanada wanaendelea kupendelea kuishi peke yao,” ladai The Toronto Star. “Kwa wazi wengi wanapendelea kuishi peke yao,” ripoti ya 1992 ya Takwimu za Kanada ilionyesha. Kati ya miaka 1981 na 1991, tamaa ya kuishi pekee iliongezeka kwa asilimia 43 kwa waseja, asilimia 16 kwa watu waliotalikana, na asilimia 18 kwa wajane wa kiume na wa kike. Wakati wa kipindi icho hicho, “kuishi pamoja bila ndoa . . . kuliongezeka kwa asilimia 111,” kulingana na Star. Familia zenye mzazi mmoja sasa ni asilimia 20 ya familia za Kanada. Kuishi pekee kujapovutia hivyo, kiwango cha uzazi kiko juu zaidi ya wakati mwingine wowote kwa miaka 14 iliyopita.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki