Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/8 kur. 3-4
  • Mtoto Wako Yumo Hatarini!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtoto Wako Yumo Hatarini!
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tatizo la Kale
  • Tatizo Zito
  • Kuzuia Nyumbani
    Amkeni!—1993
  • Kunyanyasa Watoto Kingono—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—1997
  • Mashaka Yako Ulimwenguni Kote
    Amkeni!—1999
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/8 kur. 3-4

Mtoto Wako Yumo Hatarini!

Kutenda watoto vibaya kingono ni jambo halisi linalokirihisha katika ulimwengu huu uliogonjweka. Gazeti Lear’s lilisema hivi: “Kunaathiri wengi wetu kuliko kansa, wengi wetu kuliko ugonjwa wa moyo, wengi wetu kuliko UKIMWI.” Hivyo Amkeni! lahisi likiwa na jukumu la kujaribu kuwatahadharisha wasomaji walo juu ya hatari hii na mambo yanayoweza kufanywa juu yayo.—Linganisha Ezekieli 3: 17-21; Warumi 13:11-13.

KATIKA miaka ya hivi karibuni kumekuwa kilio cha tufeni pote juu ya kutenda watoto vibaya kingono. Lakini uangalifu wa vyombo vya habari, vilivyojaa watu mashuhuri ambao wamefunulia umma jinsi walivyotendwa vibaya wakiwa watoto, umesababisha kuwe na maoni yasiyofaa yanayopendwa na wengi. Watu fulani waamini kwamba habari hiyo yote juu ya mashambulizi ya watoto ni mtindo tu wa kisasa zaidi. Hata hivyo, ni kweli, hakuna jambo jipya katika kutenda vibaya kingono. Kumekuwa kukiendelea kwa muda mrefu kama historia yenyewe ya binadamu.

Tatizo la Kale

Miaka ipatayo 4,000 iliyopita, majiji ya Sodoma na Gomora yalijulikana kwa upotovu wayo. Ni wazi kwamba kuvutiwa na watoto kingono kulikuwa miongoni mwa maovu mengi humo. Mwanzo 19:4 laeleza juu ya genge lililowaka tamaa kingono la Wasodoma “vijana kwa wazee” waliotaka kunajisi wageni wanaume wawili wa Lutu. Fikiria hili: Kwa nini wavulana tu wangewaka tamaa kwa wazo la kunajisi wanaume? Kwa wazi wao walikuwa tayari wamezoezwa upotovu wa ugoni-jinsia-moja.

Karne nyingi baadaye, taifa la Israeli lilihamia eneo la Kanaani. Bara hili lilijiingiza sana katika kufanya ngono za kiukoo, usodoma, kufanya ngono na wanyama, ukahaba, na hata kudhabihu kidesturi watoto wadogo kwa miungu mashetani hivi kwamba ilibidi matendo hayo yote machafu yakatazwe waziwazi katika Sheria ya Kimusa. (Mambo ya Walawi 18:6, 21-23; 19:29; Yeremia 32:35) Yajapokuwa maonyo ya kimungu, Waisraeli waasi, kutia ndani watawala fulani wao, walizoea mambo hayo yenye kukirihisha.—Zaburi 106:35-38.

Hata hivyo, kwa habari hii, Ugiriki na Roma za kale zilikuwa mbaya sana zaidi ya Israeli. Uuaji wa vitoto vichanga ulikuwa jambo la kawaida kwa zote mbili, na katika Ugiriki zoea la watu wenye umri mkubwa zaidi kuwa na uhusiano wa kingono na wavulana wachanga lilikuwa jambo lililokubaliwa na wengi. Majumba ya wavulana makahaba yalisitawi katika kila jiji la kale la Ugiriki. Katika Milki ya Roma, ukahaba wa watoto ulienea sana hivi kwamba kodi na sikukuu za kipekee zilianzishwa kihususa kwa ajili ya biashara hiyo. Katika wanja za michezo, wasichana walinajisiwa na kulazimishwa wafanye ngono na wanyama. Ukatili mwingine kama huo ulikuwa mwingi katika mataifa mengine mengi ya kale.

Namna gani nyakati zetu za kisasa? Je! ainabinadamu imestaarabika sana hivi kwamba matendo hayo maovu ya kingono hayawezi kusitawi leo? Wanafunzi wa Biblia hawawezi kukubali wazo hilo. Wao wajua vema kwamba mtume Paulo aliona kipindi chetu kuwa ‘nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.’ Yeye alieleza kirefu juu ya kujipenda mwenyewe, kupenda anasa, na kuvunjika kwa upendo wa asili wa familia ambako kumeenea katika jamii ya kisasa na akaongeza hivi: “Watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu.” (2 Timotheo 3:1-5, 13; Ufunuo 12:7-12) Je! kutenda watoto vibaya kingono, ambako mara nyingi huchochewa na “watu wabaya na wadanganyaji,” kumekuwa kubaya zaidi?

Tatizo Zito

Mara nyingi kutenda watoto vibaya hufichwa kwa usiri sana, hivi kwamba kumeitwa labda uhalifu usioripotiwa zaidi ya mwingineo wowote. Hata hivyo, kwa wazi uhalifu huo umeongezeka sana katika miongo ya hivi karibuni. Katika United States, uchunguzi juu ya habari hiyo ulifanywa na Los Angeles Times. Lilipata kwamba asilimia 27 ya wanawake na asilimia 16 ya wanaume walikuwa wametendwa vibaya kingono wakiwa watoto. Hata ingawa takwimu hizo zinashtua, makadirio mengine ya uangalifu ya United States yamekuwa ya juu zaidi.

Katika Malaysia, ripoti za kutenda watoto vibaya kingono zimeongezeka mara nne kwa muda wa mwongo uliopita. Katika Thailandi, katika uchunguzi mmoja wanaume wapatao asilimia 75 walikiri walilala na watoto makahaba. Katika Ujerumani, maofisa wanakadiria kwamba watoto wapatao 300,000 hutendwa vibaya kingono kila mwaka. Kulingana na Cape Times ya Afrika Kusini, hesabu ya ripoti za kutenda vibaya huko iliongezeka kwa asilimia 175 katika kipindi cha miaka mitatu cha hivi karibuni. Katika Uholanzi na Kanada, watafiti walipata kwamba karibu theluthi moja ya wanawake wote walikuwa wametendwa vibaya kingono wakiwa watoto. Katika Finlandi, asilimia 18 ya wasichana wa darasa la tisa (wa miaka 15 au 16) na asilimia 7 ya wavulana waliripoti kwamba walikuwa wamekuwa na uhusiano wa kingono na mtu fulani aliye mkubwa zaidi yao kwa angalau miaka mitano.

Katika nchi mbalimbali ripoti zenye kusikitisha zimefunuliwa kuhusu madhehebu za kidini zinazowatenda vibaya watoto kwa mazoea ya kingono yenye ukatili na utesaji. Mara nyingi, wale wanaoripoti kwamba walitendwa vibaya katika uhalifu huo hutiliwa shaka, badala ya kuonyeshwa huruma.

Kwa hiyo kutenda watoto vibaya kingono si jambo jipya wala jambo lisilo la kawaida; ni tatizo la muda mrefu ambalo limeenea sana leo. Tokeo lalo laweza kusononesha sana. Waokokaji wengi hupatwa na hisia nyingi za kutostahili na kutojistahi. Wastadi katika uwanja huo wameorodhesha baadhi ya matokeo ya baadaye yaliyo ya kawaida ya ngono za kiukoo kwa wasichana, kama vile kutoroka nyumbani, kutumia vibaya madawa na kileo, mshuko wa moyo, kujaribu kujiua, utovu wa nidhamu, ngono za ovyo-ovyo, kukosa usingizi, na kutoweza kujifunza. Matokeo ya muda mrefu yaweza kutia ndani stadi duni za kuwa mzazi, ubaridi, kutowaamini wanaume, kuoa mtu anayevutiwa na watoto kingono, ugoni-jinsia-kike, ukahaba, na kutenda watoto vibaya kingono kwenyewe.

Si kwamba matokeo hayo ya baadaye hayawezi kuepukwa na mtendwa vibaya; wala mtu yeyote hawezi kutoa udhuru kwa haki kwa ajili ya mwenendo mbaya eti kwa sababu alitendwa vibaya zamani. Kutendwa vibaya hakuwafanyi kimbele watendwa vibaya wawe wakosefu wa adili au watovu wa nidhamu; wala hakuondoi madaraka yao yote ya kibinafsi kwa mambo wanayochagua baadaye maishani. Lakini matokeo hayo yaliyo ya kawaida kwa watendwa vibaya ni hatari kwelikweli. Yanaongeza uzito wa swali, Twaweza kuwalindaje watoto wasitendwe vibaya kingono?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki