Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 10/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Ile Harakati ya Muhula Mpya Ni Nini?
    Amkeni!—1994
  • Harakati ya Muhula Mpya Ipendwayo na Wengi
    Amkeni!—1994
  • Ule Muhula Mpya wa Halisi Utakujaje?
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 10/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Muhula Mpya Asanteni sana kwa ule mfululizo juu ya harakati ya Muhula Mpya. (Machi 8, 1994) Hapo kwanza nilipekua habari juu ya vyombo visivyotambulikana virukavyo angani (UFO), uhai ulio nje ya ulimwengu huu, na mtu kuzaliwa tena akiwa na umbo tofauti. Nilifuata mitaala ya kufundishwa Yoga na utafakari na nikapokea matibabu yanayohusu usingizi wa mazingaombwe. Hatimaye niliingia katika matatizo mazito ya kiroho, ya kiakili, ya kihisia-moyo, na ya kimwili na hata nikaja chini ya mshiko wa roho waovu. Utopia (hali kamilifu kimawazo) niliyotamani sana ilionekana ikizidi tu kusonga mbali. Miaka mitano na nusu baadaye, sasa mimi ninamtumikia Yehova na nimekombolewa kutoka giza la ile harakati ya Muhula Mpya.

E. D., Uholanzi

Kabla ya kuwa Mkristo, nilihusika na namna ya kufikiri na njia ya maisha ya Muhula Mpya. Hivi majuzi dada yangu mdogo zaidi ameonyesha tamaa ya kuhusika na kikundi cha watetezi wa Muhula Mpya. Kwa hiyo niliipitia makala hii pamoja naye. Aligutuka kuona kwamba Muhula Mpya una uhusiano wa wazi na siri na mafumbo ya ulimwengu wa pepo. Sasa yeye amepiga moyo konde kujiepusha na fikira ya Muhula Mpya.

L. S., Uingereza

Makala yenu ilianza vema. Ingawa hivyo, muda mfupi baada ya hapo mwataarifu kwamba “njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake.” Mwishoni, mwataarifu kwamba imani za Muhula Mpya zaweza kuleta giza zaidi tu. Je, mnasema kwamba twapaswa kuacha maoni yote ya kuwazia hali bora na eti tutumaini kwamba mambo yote yatajitengeneza yenyewe tu? Mmefikiaje mkataa wa kwamba si fungu la mwanadamu kujaribu kujitengenezea mwenyewe ulimwengu mzuri zaidi?

A. L., Marekani

Ni Biblia—si “Amkeni!”—isemayo “njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake.” (Yeremia 10:23) Hivyo jitihada za kibinadamu za kuleta Muhula Mpya ni za ubatili. Hata hivyo, Wakristo wa kweli hawapuuzi matatizo ya leo. Kwa kufundisha wengine kanuni za Neno la Mungu, Mashahidi wa Yehova wamesaidia mamilioni ‘wajinufaishe’—kiuchumi, kimwili, na kiroho. (Isaya 48:17, NW; Mathayo 28:19, 20) Wakati huohuo, sisi huelekeza watu kwenye tumaini halisi la “mbingu mpya na dunia mpya” zinazokuja—jambo ambalo ni Mungu, si mwanadamu, ataleta. (2 Petro 3:13, NW)—Mhariri.

Maisha Maradufu Makala zenu juu ya kuishi maisha maradufu (Desemba 22, 1993, na Januari 8 na 22, 1994) zilichochea mwanangu wa miaka 17 afunue dhambi aliyohusika nayo kwa muda wa zaidi ya miaka minne. Juujuu, alionekana kuwa akifanya maendeleo mazuri ya kiroho. Sisi tulishtushwa sana na kuchukizwa na dhambi hii, lakini tuliweza kutenda kwa njia yenye upendo na msamaha kwa sababu ya makala zenu.

J. P., Marekani

Niliacha kushirikiana na kutaniko la Kikristo kwa zaidi ya mwaka mmoja. Lakini makala hizo zilikuwa zenye kutia moyo sana na kujaa upendo. Kama mlivyosema, hatua ya kwanza ilikuwa kumfikia Yehova kwa sala. Ni jambo gumu sana, lakini limeniletea baraka nyingi.

M. G., Ufaransa

Vijana Wakinza Kutiwa Damu Mishipani Nina miaka 12, na sasa tu ndio nimesoma ule mfululizo “Vijana Ambao Hutanguliza Mungu.” (Mei 22, 1994) Nilivutiwa sana na moyo mkuu ambao ndugu na dada hawa wachanga Wakristo walionyesha, kukubali kifo wakiwa na uhakika mwingi hivyo katika Yehova na katika ufufuo. Moyo wao mkuu na imani katika Yehova zilinifanya nilie machozi kwa shangwe.

B. C. R., Hispania

Tumepokea maelezo mengi kama hayo ya uthamini. Hata hivyo, jambo moja lahitaji sahihisho. Tuliripoti kwamba Ernestine Gregory hakutiwa damu mishipani. Imekuwa kwamba dakika chache baada ya agizo la mahakama kutolewa, kwa kweli alitiwa damu mishipani kinguvu. Aliokoka usumbufu mkali huo.—Mhariri.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki