Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/8 kur. 15-17
  • Kwa Nini Nina Hisia Hizi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Nina Hisia Hizi?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Asili au Malezi?
  • Visababishi vya Kimazingira
  • Baba na Mwana
  • Suala la Maadili
  • Ugoni-Jinsia-Moja—Je, Kweli Ni Mbaya Hivyo?
    Amkeni!—1995
  • Naweza Kuzifanyaje Hisia Hizi Ziondoke?
    Amkeni!—1995
  • Je, Kuna Sababu Zinazotetea Ushoga?
    Amkeni!—2012
  • Nifanye Nini Ikiwa Ninavutiwa na Watu wa Jinsia Yangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 2/8 kur. 15-17

Vijana Huuliza. . .

Kwa Nini Nina Hisia Hizi?

“Nahisi ni kama vita fulani inaendelea ndani yangu. Sijui pa kugeukia.”—Bob.

VIJANA wengi huugua mateso kama hayo ya kiakili. Wakiwa tofauti na marika zao waonekanao kumezwa na upendezi katika jinsia tofauti, wao hujipata wakizidi kuvutiwa na washirika wa jinsia yao wenyewe. Kwa wengi, huu ni utambuzi wenye kulemea sana hisia.

Mwanamke mmoja alisema hivi juu ya binti yake: “Yeye alianza kuwa na afya mbaya, akawa hawezi kula wala kulala, na akashuka moyo na kuwa na tabia-moyo zenye kubadilika-badilika. Hata alijaribu kujiua.” Kisababishi kikubwa cha msononeko huu kilikuwa nini? “Alikuwa na hisia za Mlawiti wa Kike.” Kwa watu fulani huenda isiwe rahisi kushinda mielekeo kama hiyo. “Nilipokuwa sijafikia utineja,” akiri mwanamume kijana tutakayemwita Mark, “nilianza kupatwa na mielekeo ya ugoni-jinsia-moja nikiwa na baadhi ya marafiki zangu. Niliendelea na jambo hili hadi ubalehe mpaka nilipoanza kujifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova. Lakini nyakati fulani nilikuwa bado na hisia mbaya zikibaki ndani yangu.”

Ni nini husababisha kijana avutiwe na jinsia yake mwenyewe? Na kijana apaswa kufanya nini ikiwa yeye asumbuliwa na hisia kama hizo?

Asili au Malezi?

Siku hizi watu wengi hupenda kusema kwamba wagoni-jinsia-moja walizaliwa hivyo na kwamba mwelekeo wa tamaa ya ngono hauwezi kubadilishwa. Kwa kielelezo, gazeti Time lilitangaza kwa njia ya kutazamisha hivi: “Uchunguzi mpya wadokeza kwamba kuna tofauti ya muundo kati ya bongo za wagoni-jinsia-moja na wanaume wafanyao ngono na jinsia tofauti.” Hata hivyo, uchunguzi huu ulifanywa katika bongo za wanaume waliokuwa wamekufa kwa UKIMWI. Hakika hili halithibitishi jambo hilo!

Nadharia nyingine yahusisha homoni. Wanasayansi walionelea kwamba panya wa maabara walionyimwa homoni za kiume walionyesha tabia “za kike” za kutafuta wenzi wa kuingiliana. Walikata shauri kwamba vivyohivyo huenda ikawa wagoni-jinsia-moja wana kasoro ya kimwili—kuwa na homoni nyingi mno au chache mno za kiume kabla ya kuzaliwa. Ingawa hivyo, wanasayansi wengi huamini kwamba tabia ya kiajabu miongoni mwa panya ni kitabia tu—wala kwa kweli si ‘ugoni-jinsia-moja.’ Zaidi ya hilo, wanadamu si panya. The Harvard Medical School Mental Health Letter yatoa hoja hii: “Haielekei kabisa kwamba homoni za kabla ya uchukuaji mimba huathiri . . . ujinsia wa kibinadamu kwa njia ileile ya moja kwa moja ambayo hizo hupanga vitabia vihusikavyo katika tabia ya panya ya kutafuta wenzi wa kuingiliana.”

Uangalifu mwingi umefanywa pia katika machunguzi ya jeni. Miongoni mwa wanaume na wanawake wagoni-jinsia-moja walio na mapacha-fanani, karibu nusu ya mapacha wao ni wagoni-jinsia-moja vilevile. Kwa kuwa mapacha-ukuzi-mmoja [walio wafanani] ni walandana-jeni, lilionekana kuwa jambo la kimantiki kukata shauri kwamba jeni fulani ya kifumbo ndiyo iliyosababisha ule mwachano. Hata hivyo, angalia kwamba nusu ya watoto mapacha hawakuwa wagoni-jinsia-moja. Kama kweli tabia hii ingekuwa imeimarishwa thabiti katika jeni, je, mapacha wote hawangekuwa nayo? Ni kweli, jeni na homoni huenda zikashiriki sehemu fulani. Hata hivyo, Scientific American liliripoti yaliyoonwa na watu fulani kuonyesha kwamba ushuhuda ‘wadokeza kwa uthabiti kwamba mazingira huchangia sana mwelekeo wa tamaa ya ngono.’

Visababishi vya Kimazingira

Fikiria mazingira ya Ugiriki wa kale. Kwa kuchochewa na hadithi za mapenzi juu ya miungu yao ya kingano, maandishi ya wanafalsafa kama Plato, na utamaduni wa michezo ya kukaza maungo ambako vijana walicheza bila kuvaa nguo, ugoni-jinsia-moja ulikuwako kwa fujo miongoni mwa watu maarufu katika ulimwengu wa wasema-Kigiriki. Kulingana na kitabu Love in Ancient Greece, “ilionwa kuwa aibu katika Krete kwa mvulana kabaila kutokuwa na mpenzi [wa kiume].” Hakuna jeni wala homoni ya kifumbo iliyosababisha mzoroto kama huo. Ulisitawi sana kwa sababu utamaduni wa Kigiriki uliuruhusu, naam, ukautia moyo! Hii yatoa kielezi vema jinsi mazingira yawezavyo kushiriki fungu kubwa.

Bila shaka furiko la propaganda za kupendelea ugoni-jinsia-moja zimeeneza sana maoni hayo leo. Madokezo ya ugoni-jinsia-moja ni tele katika televisheni, sinema, muziki, na magazeti. Televisheni ya kebo imewapa vijana fulani upataji rahisi wa ponografia sugu. Mitindo ya mavazi ya jumla-jinsia imekuwa ikipendwa sana. Wastadi fulani huhisi pia kwamba zile propaganda za baadhi ya wanawake kupinga wanaume zimechangia ongezeko la ulawiti wa kike. Huenda vijana pia wakapata nafasi za mavutano mabaya ya ushirika wa wanadarasa wenzao wateteao waziwazi mtindo-maisha wa ugoni-jinsia-moja.—1 Wakorintho 15:33.

Baba na Mwana

Nyakati fulani, mazingira ya familia yenye kasoro huonekana pia kushiriki sehemu kubwa, hasa miongoni mwa wanaume.a Baba huchangia sana katika ukuzi wa kihisia-moyo wa mtoto. (Waefeso 6:4) Kitabu Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha husema: “Zile sifa za kiume za baba zinaweza kumsaidia asitawishe utu kamili, uliosawazika.”b Mvulana ahitaji pia kutambuliwa, kupendwa, na kukubaliwa na baba yake. (Linganisha Luka 3:22.) Tokeo laweza kuwa nini baba akishindwa kumpa mtoto wake uangalifu huu uhitajiwao? Ni msononeko wa kihisia-moyo. Mwandikaji wa afya ya akili Joseph Nicolosi adai kwamba ugoni-jinsia-moja wa kiume “karibu sikuzote [ni] tokeo la matatizo katika mahusiano ya familia, hasa kati ya baba na mwana.”

Huenda ikawa kwamba mama bila kujua huongezea ubaya wa hali kwa kumshusha mume wake au kwa kummiliki mwana wake kupita kiasi. Uchunguzi mmoja wa wavulana wenye tabia za kike ulitoa oneleo hili: “Baadhi ya wazazi walikuwa wametamani kupata msichana badala ya mvulana na kwa njia isiyoonekana wazi sana wakatia moyo mwana wao mchanga avalie kama msichana au wakamvalisha hivyo.”

Hii si kusema kwamba hisia za ngono zilizopotoka zaweza moja kwa moja tu kulaumiwa juu ya wazazi wa mtu. Wanaume wengi ambao wamekua wakawa watu wazima wakiwa na akina mama wenye kuwamiliki na akina baba wasiojali, wasiokuwapo, au wenye kuwatenda vibaya bado wamekuza nyutu za kiume. Zaidi ya hilo, si wote wenye mielekeo ya ugoni-jinsia-moja huwa kwa lazima wametoka katika familia zenye kasoro. Ingawa hivyo, yaonekana kwamba wavulana fulani hujeruhiwa kwa njia fulani hususa. “Kutokana na hisia yake ya mapema ya kukataliwa na baba . . . ,” adai Dakt. Nicolosi, “mgoni-jinsia-moja hutembea akiwa na hisia ya udhaifu na ya kutoweza mambo kuhusiana na sifa zile zihusishwazo na hali ya kiume, yaani, mamlaka, kukazania mambo, na kuwa mwenye nguvu. Yeye huvutiwa na nguvu ya kiume kutokana na jitihada afanyayo bila kujifahamu kwamba anataka kujipatia hali ya kiume.”

Mwanamume kijana Mkristo jina lake Peter aandika hivi: “Baba yangu alikuwa mraibu wa alkoholi na alipiga mama yangu kwa ukawaida, na nyakati fulani, alitupiga sisi sote. Nilipokuwa na miaka 12, alitoka nyumbani akaenda zake. Nilihisi kumkosa baba. Sikuzote nilitamani sana kuwa na mtu fulani wa kujazia pengo nililohisi kila siku. Mwishowe nilipokuza urafiki pamoja na mwanamume mzuri Mkristo ambaye nilifikiri angeweza kujazia uhitaji huo, nilianza kumwonea hisia za ngono.”

Kwa kupendeza, idadi kubwa za wagoni-jinsia-moja ni majeruhi wa kusumbuliwa utotoni.c Kusumbuliwa huko kwaweza kutokeza madhara ya kudumu ya kimwili na ya kihisia-moyo. Kwa wengine huenda kukafanyiza kile ambacho mwandikaji mmoja alikiita “utu mpotovu wa kingono.” Kwa wazi jambo hili lilitukia katika Sodoma la kale, ambako wavulana wachanga walidhihirisha hamu yenye pupa kali ya ngono zilizopotoshwa. (Mwanzo 19:4, 5) Kwa wazi, wao walikuwa zao la kutumiwa vibaya wa watu wazima.

Suala la Maadili

Huenda wanasayansi wasije kamwe kujua kabisa ni kwa kadiri gani asili na malezi yahusika katika kuvutiwa na watu wa jinsia ileile. Lakini jambo moja ni wazi: Wanadamu wote huzaliwa wakiwa na elekeo la kujiacha washindwe na kufikiri kubaya na mielekeo mibaya.—Warumi 3:23.

Kwa hiyo ni lazima kijana atamaniye kumpendeza Mungu ajipatanishe na viwango Vyake vya maadili na kuepuka mwenendo wa kukosa adili, ingawa huenda kufanya hivyo kukawa na ugumu wenye kuumiza. Ni kweli, huenda watu mmoja-mmoja wakawa sana na elekeo la ugoni-jinsia-moja, sawa na vile watu mmoja-mmoja, kulingana na Biblia, walivyo sana ‘wepesi wa hasira.’ (Tito 1:7) Lakini bado Biblia hushutumu maonyesho ya hasira isiyo ya uadilifu. (Waefeso 4:31) Vivyohivyo, Mkristo hawezi kutoa udhuru wa tabia ya kukosa adili kwa kusema ‘alizaliwa hivyo.’ Wenye kusumbua watoto hutoa udhuru uohuo wa kutojali wasemapo kwamba tamaa yao kwa watoto ni ‘ya kuzaliwa nayo.’ Lakini je, mtu yeyote aweza kukana kwamba hamu yao ya ngono ni ya upotovu? Ndivyo na tamaa kwa mtu wa jinsia ileile.

Kwa hiyo ni lazima vijana wajikutao wakivutiwa na jinsia ileile waepuke kujiacha washindwe na hisia zao. Ingawa hivyo, kwa nini Biblia hushutumu wazi hivyo ugoni-jinsia-moja? Je, mtindo-maisha huo ni wa kiugonjwa na mpotovu? Ikiwa ndivyo, kijana aweza kufanya nini ajiepushe nao kabisa? Maswali haya yatazungumziwa katika toleo la wakati ujao la Amkeni!

[Maelezo ya Chini]

a Ni utafiti kidogo kwa kulinganisha ambao umefanywa juu ya ukuzi wa ugoni-jinsia-moja wa kike. Ingawa hivyo, bila shaka mavutano ya kifamilia hushiriki pia sehemu humo.

b Kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

c Kwa wazi kutumia watoto vibaya kulikuwa kisababishi katika ukuzi wa ugoni-jinsia-moja katika Ugiriki wa kale. Watongozi wazee zaidi wa wavulana wachanga walikuwa kwa kawaida wakirejezewa kuwa “mbwa-mwitu”—“ishara ya pupa na ukali mfidhuli.” Majeruhi wao wachanga waliitwa “wana-kondoo.”y

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki