Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Amkeni! Imeboreshwa Hivi majuzi nilipata nakala ya Amkeni! la Aprili 8, 1994, katika mlango-wavu wangu. Ala! Ni nini kimetukia? Mmebuni kichapo kilichofanywa kuwa cha karibuni, chenye kuelimisha. Naona badiliko hilo likiwa lenye kushangaza sana, na kwa mara ya kwanza, kwa kweli nilisoma makala hizi. (Kwa kawaida ningefikiri, ‘Ah! . . . , walikuwa hapa tena,’ na kulitupa gazeti hilo.) Kulikuwa na jambo fulani katika gazeti hilo kwa kila mtu. Nilifurahia hasa makala zile juu ya kansa na juu ya “‘Barabara Isongayo’ ya Kanada Yenye Kuvutia.” Mnaendelea katika njia ifaayo. Endeleeni na kazi hiyo nzuri, nami naahidi sitatupilia mbali nakala zozote zaidi hadi nizisome.
D. G., Marekani
Mchanganyo wa Kijiografia Katika makala zenu za Oktoba 22, 1994, kuhusu wamishonari, zilizokuwa na kichwa “Kuhama Magharibi Kuingia Ulaya,” mwataarifu kwamba Boniface “alithubutu kuangusha mti mtakatifu wa oki wa Thor” kule Geismar, karibu na Göttingen, Ujerumani. Kwa kadiri nijuavyo, Geismar inayotajwa hapo haiko karibu na Göttingen bali iko karibu na Fritzlar.
A. L., Ujerumani
Uko sahihi kabisa. Ilikuwa kwamba pana mahali pawili panapoitwa Geismar, na tulipachanganya. Asante kwa kutujulisha kasoro hiyo.—Mhariri.
Dini na Vita Mfululizo wenu wa Oktoba 22, 1994, “Wakati Dini Ijiungapo na Vita” ulizungumzia kile mnachofahamu kuwa kupungukiwa kwa upande wa viongozi wa Katoliki kushtumu vita moja kwa moja. Lakini historia yafunua tofauti. Kwenye mwanzo wa mnyanyaso wa Hitler kwa Wayahudi Wajerumani, Kadinali Faulhaber wa Munich alitoa mahubiri ambayo katika hayo alitetea Wayahudi. Makasisi wengine mashujaa walishutumu moja kwa moja sheria za Nazi ambazo zilikataza ndoa kati ya “Waarya” na Wayahudi. Baada ya kufyatuka kwa Vita ya Ulimwengu 2 katika Ulaya, Hitler alifunga shule za Katoliki, akakandamiza shirika la habari la Katoliki, na katika Poland, akafunga makao yote ya watawa, na seminari.
J. L., Marekani
Makala hizo zilitegemea vyanzo visivyo na upendeleo na vinavyoaminika. Kwa kielelezo, kitabu “German Catholics and Hitler’s Wars” kiliandikwa na Gordon C. Zahn, ambaye ni profesa Mkatoliki. Kwa wazi, ule uthibitisho ni mwingi kwamba, angalau katika hatua za mapema, baraza la Kikatoliki lilipatia chama cha Nazi utegemezo wa ujumla. Hii haimaanishi kwamba hakukuwa na makasisi mmoja-mmoja ambao walipinga kwa ujasiri chama cha Wanazi. Lakini hawa kwa wazi walikuwa wachache.—Mhariri.
Kunyonyesha Maziwa ya Mama Makala yenu “Mambo ya Msingi ya Kunyonyesha Maziwa ya Mama” (Agosti 22, 1994) iliandaa habari ya ndani zaidi kuliko makala zenu zilizotangulia juu ya jambo hilo. Nyakati nyingi, akina baba huwaachia wake zao wafaulu au wasifaulu. Lakini makala yenu kwa kweli iliwaeleza akina baba na washirika wengine wa familia kile wangefanya ili kusaidia kufanikisha kunyonyesha maziwa ya mama.
D. D., Marekani
Nilikuwa na ono zuri ajabu la kunyonyesha maziwa ya mama kila mmoja wa watoto wangu wawili. Kulikuwa na matatizo ya mwanzoni, kama vile maumivu, lakini kwa kitia-moyo kutoka kwa dada yangu na shauri kutoka kwa daktari wangu nilishinda tatizo hilo. Ningetia moyo kila mama anayeweza anyonyeshe mtoto wake, kwa kuwa ushikamano wa kina kati ya mama na mtoto ni ono linalovutia ambalo mtu hawezi kusahau.
U. B., Ujerumani
Ugonjwa wa Kifumbo Nikiwa nimekuwa msomaji wa magazeti yenu tangu umri wa miaka mitano, nilithamini kwelikweli ile makala “Maradhi ya Kifumbo ya Guam.” (Agosti 8, 1994) Mama yangu, aliyekuwa mtumishi mwaminifu wa Mungu hadi kifo chake katika 1972, alikuwa jeruhi wa maradhi haya. Nataka kuwashukuru kwa ajili ya habari na yale maelezo ya kina mliyotoa. Nimeshiriki toleo hili pamoja na familia yangu na marafiki ili kuonyesha thamani ya magazeti yenu.
W. A., Marekani