Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Mambo Ambayo Wanawake Wapaswa Kujua Juu ya Kansa ya Matiti
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Njia za Kuokoka Kansa
    Amkeni!—1994
  • Kansa ya Matiti Utazamie Nini? Ukabiliane Jinsi Gani?
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Maisha Maradufu Nataka kuwashukuru nyinyi kwa ile makala “Vijana Huuliza . . . Maisha Maradufu—Ni Nani Apaswa Kujua?” (Januari 8, 1994) Nilipokuwa na umri wa miaka 16, nilianza kulewa, kuvuta sigareti, na kufanya miadi ya kijinsia bila wazazi wangu kujua. Makala hizi hakika zilinisaidia kuona kwamba hakuna kilichofichika kutoka kwa macho ya Mungu yenye uangalifu.

T. T., Fiji

Kufuatia Fedha Ndio tu nimesoma ule mfululizo “Kufuatia Fedha—Kutaishia Wapi?” (Machi 22, 1994) Makala hizo ziliipa habari hiyo maelezo bora zaidi. Sikujua kwamba hali kama hizo mbaya bado zingaliko kwa wafanyakazi wahamaji na familia zao. Mimi nawahurumia sana.

G. M., Marekani

Jinsi mlifafanua zile hali mbaya za kazini na mishahara ya chini ni sahihi. Ni maelezo yenye huzuni ya jinsi wengine huwaona wafanyakazi hawa—si kama binadamu walio na hisia kama zetu. Kweli, “mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasara yake”!—Mhubiri 8:9.

K. V., Marekani

Kansa ya Matiti Katika mfululizo wenu “Kansa ya Matiti—Hofu ya Kila Mwanamke” (Aprili 8, 1994), hamkutaja yale machunguo yanayoonyesha kunyonyesha kwaweza kupunguza ule uwezekano wa kansa ya matiti.

B. J. M., Ujerumani

Twasikitikia mwacho huu. Ingawaje, jambo hilo lilitajwa katika makala “Uthibitisho wa Mafaa ya Maziwa ya Mama,” iliyotokea katika makala yetu ya Septemba 22, 1993.—Mhariri.

Mimi nilitumia wakati fulani pamoja na dada Mkristo aliyetolewa titi. Alikuwa na umri wa miaka 62 na alishuka moyo sana. Nakumbuka nikiwa sina neno la kumtegemeza nalo. Kwa msaada wa maelezo mliyonukuu katika makala hizo, sasa naweza kumtegemeza ifaavyo.

D. H., Marekani

Karibu miaka miwili iliyopita, nilifanyiwa upasuaji kwa sababu ya kansa ya matiti. Ili kupata habari kuhusu kansa, nilinunua ensaiklopedia ya kitiba, lakini sikupata mengi. Hata hivyo makala yenu ilijibu maswali yangu. Hakika ilinifariji.

M. G., Italia

Miaka tisa iliyopita mama yangu alikufa kwa kansa ya matiti. Wakati huo nilikuwa nina umri wa miaka tisa tu, na kamwe sikuelewa aliyoyakabili. Niliposoma makala hizo haikuwa vigumu kwangu kulia nilipomfikiria mama. Sitaweza kamwe kuwashukuru vya kutosha kwa ufahamu mlionipatia mimi kuhusu miaka ya mwisho-mwisho ya maisha yake.

K. F., Marekani

Walio na UKIMWI Nilisoma makala yenu “Kusaidia Wale Walio na UKIMWI.” (Machi 22, 1994) Mimi nina virusi ya HIV na nilipata makala hiyo kuwa ngumu sana kuikubali. Familia yangu walilia kwa sababu ya umizo hilo na zile hisia za kukataliwa.

B. J., Marekani

Kwa hakika mioyo yetu ina huruma sana kwa nyote mnaotaabika sana miongoni mwetu. Makala yetu ilijitahidi kusawazisha matakwa yao pamoja na mahangaiko ya walio wengi. Kwa sababu Sheria ya Mungu kwa Israeli ilichukua hatua madhubuti ili kulinda afya ya taifa kwa ujumla, tulihisi inafaa kupendekeza tahadhari za kiasi kwa afya. (Linganisha Walawi 13:21, 33.) Tulikubali kwamba “mtu asiwe akiogopa-ogopa kuwa karibu na watu wenye UKIMWI.” Hata hivyo, wengi waendelea kuwa na hofu licha ya kuhakikishiwa na madaktari. Hivyo basi tunawatia moyo walio na UKIMWI waheshimu hisia za wale wengine ambao huenda wasijihisi salama kwa kuonyesha shauku ya kimwili. Kile wasioambukizwa wanachochagua kufanya kuhusu hili ni maamuzi yao ya kibinafsi. Katika tukio lolote lile, Wakristo wote wapaswa kuwa na tamaa ya kutoka moyoni kuonyesha fadhili na huruma kwa walioambukizwa.—Mhariri.

Nimetiwa moyo sana kwamba makala kama hiyo yenye huruma na iliyoandikwa vizuri imeandaliwa. Hasa nilithamini yale madokezo kwamba tujapopaswa kuchukua “tahadhari kwa wote” twapaswa kuonyesha huruma na tuandae msaada msikitikivu.

M. H., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki