Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g00 4/8 uku. 15
  • Kifaa cha Kufunzia Haki za Kibinadamu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kifaa cha Kufunzia Haki za Kibinadamu
  • Amkeni!—2000
  • Habari Zinazolingana
  • Mataraja Kutoka Orofa ya 29
    Amkeni!—1998
  • Haki za Kibinadamu kwa Wote—Uhalisi wa Ulimwenguni Pote!
    Amkeni!—1998
  • Haki za Kibinadamu na Makosa Leo
    Amkeni!—1998
  • Je, Ni Haki Bila Madaraka?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2000
g00 4/8 uku. 15

Kifaa cha Kufunzia Haki za Kibinadamu

MWANAFUNZI aitwaye Rut Jiménez Gila, mwenye umri wa miaka 17 anayeishi huko Granada, Hispania, aliombwa na mwalimu wake aandike insha kuhusu haki za Kibinadamu. Majuma kadhaa baada ya kukamilisha mgawo huo, alifahamishwa na baraza la mitihani la Ulaya lililoko Brussels, Ubelgiji, kwamba alikuwa ameteuliwa pamoja na wanafunzi wengine kadhaa kutoka Hispania ili wawakilishe nchi yao. Baadaye aliwaandikia wachapishaji wa gazeti la Amkeni! barua ifuatayo.

“Nilihitaji habari ya karibuni zaidi kuhusu haki za Kibinadamu, na toleo la ‘Amkeni!’ la Novemba 22, 1998, ‘Je, Haki za Kibinadamu Zitawahi Kupatikana kwa Wote?,’ lilikuwa na habari hususa niliyokuwa nikitafuta. Ili kutoa mifano ya kukiukwa kwa haki za Kibinadamu, niliteua pia habari kutoka kwa makala nyingine za ‘Amkeni!’ juu ya wakati ujao wa wanawake na yale Maangamizi Makubwa. [Ona toleo la Aprili 8, 1998, na Agosti 8, 1998.] Katika utafiti wangu niligundua kwamba ‘Amkeni!’ lilikuwa na habari ambazo singeweza kuzipata katika magazeti mengine au vitabu vya marejezo. Nilivutiwa pia na picha, na nilitia baadhi yake katika ripoti yangu.

“Kwa sababu ya insha yangu iliyoshinda tuzo, nilikaa Finland kwa muda wa juma moja, na huko niliweza kuzungumza zaidi juu ya haki za Kibinadamu na kueleza thamani ya gazeti la Amkeni! katika kukazia masuala muhimu kama hilo.

“Asanteni sana, kwa sababu ya kuwa wa kwanza sikuzote kutujulisha matukio ya ulimwengu. Yehova na aendelee kuwabariki, ili mamilioni ya watu waendelee kunufaishwa na habari hiyo.”

[Picha katika ukurasa wa 15]

Rut akiwa na cheti cha kushiriki alichotuzwa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki