Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 30 uku. 76
  • Rahabu Awaficha Wapelelezi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Rahabu Awaficha Wapelelezi
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Rahabu alimwamini Yehova
    Wafundishe Watoto Wako
  • Rahabu Alisikiliza Habari
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Rahabu Anaficha Wapelelezi
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • ‘Alitangazwa Kuwa Mwadilifu kwa Matendo’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 30 uku. 76
Rahabu anawalinda wapelelezi kwa kuwaelekeza askari upande mwingine

SOMO LA 30

Rahabu Awaficha Wapelelezi

Wapelelezi Waisraeli walipoenda kwenye jiji la Yeriko, walikaa katika nyumba ya mwanamke aliyeitwa Rahabu. Mfalme wa Yeriko akatambua jambo hilo na kuwatuma askari kwenye nyumba ya Rahabu. Lakini Rahabu akawaficha wapelelezi hao wawili kwenye dari la nyumba yake na kuwaelekeza askari upande mwingine. Kisha Rahabu akawaambia wapelelezi hao hivi: ‘Nitawasaidia kwa sababu ninajua kwamba Yehova yuko upande wenu na kwamba mtaishinda nchi hii. Tafadhali mniahidi kwamba mtaiokoa familia yangu.’

Wapelelezi wakamwambia Rahabu hivi: ‘Tunaahidi kwamba hakuna mtu ndani ya nyumba yako atakayeumia.’ Walimwambia hivi: ‘Funga kamba nyekundu dirishani, na watu wa familia yako wataokolewa.’

Nyumba ya Rahabu, ikiwa na kamba nyekundu iliyofungwa dirishani, inaendelea kusimama huku kuta za Yeriko zikianguka

Rahabu akawashusha wapelelezi hao kwa kamba kupitia dirisha lake. Wakaenda milimani na kujificha kwa siku tatu kabla ya kurudi kwa Yoshua. Kisha Waisraeli wakavuka Mto Yordani na kujitayarisha kuishinda nchi. Yeriko lilikuwa jiji la kwanza walilolishinda. Yehova aliwaambia walizunguke jiji mara moja kila siku kwa siku sita. Siku ya saba, walilizunguka jiji mara saba. Kisha makuhani wakapiga tarumbeta, nao askari wakapaaza sauti kwa kelele kadiri walivyoweza. Kuta za jiji hilo zikaanguka chini! Lakini nyumba ya Rahabu, ambayo ilikuwa kwenye ukuta, ikaendelea kusimama. Rahabu na familia yake wakaokolewa kwa sababu alimtegemea Yehova.

“Vivyo hivyo, je, Rahabu . . . hakutangazwa pia kuwa mwadilifu kwa matendo, baada ya kuwakaribisha wale wajumbe na kuwatoa nje kupitia njia nyingine?”​—Yakobo 2:25

Maswali: Kwa nini Rahabu aliwasaidia wapelelezi? Waisraeli walishambuliaje jiji la Yeriko? Ni nini kilichompata Rahabu na familia yake?

Yoshua 2:1-24; 6:1-27; Waebrania 11:30, 31; Yakobo 2:24-26

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki