Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 1/1 kur. 3-4
  • Je! Waweza Kuwa Adui Yako Wewe Mwenyewe?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Waweza Kuwa Adui Yako Wewe Mwenyewe?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nani Anayehitaji Maumivu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Dunia Isiyo na Maumivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Waja—Ulimwengu Usio na Maumivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Maumivu Ambayo Hayatakuwapo Tena
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 1/1 kur. 3-4

Je! Waweza Kuwa Adui Yako Wewe Mwenyewe?

“Moyo uliotulia ndio uzima wa nyama ya mwili, lakini wivu ni ugonjwa mifupani.”​—Mit. 14:30, NW.

MWANAMKE mmoja alianza kupatwa na magumu makubwa katika kusikia. Daktari wake alishindwa kuona jambo lo lote ambalo lingeonyesha kwamba sababu ilikuwa kasoro yo yote ya mwilini. Alikuwa akipatwa na hali ya kuwa kiziwi kwa sababu gani? Kwa sababu nyakati nyingi walikuwa wakipigiana kelele nyingi na binti yake, yeye alikuwa ameanza kujizuia kusikia sauti. Kwa njia hiyo, kwa wazi alijaribu kujilinda asipatwe na hali isiyopendeza. Mara moja alipotambua tatizo lake, hali yake ya kusikia ikarudia ukawaida wake.

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 29 alianza kuumwa karibu na moyo wake. Hali hiyo yenye kusumbua iliendelea ikaongezeka kwa muda wa miaka 10. Hali hiyo iliendelea ajapopata matibabu mengi na vipindi virefu vya mapumziko. Tatizo hilo la afya lilimzuia kufanya kazi yake na kumnyang’anya furaha yake.

Je! kweli kweli yeye alikuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo? Hapana. Alipokuwa na umri wa miaka 21, alikuwa amepatwa na ugonjwa mbaya, lakini alikuwa amepona kabisa. Walakini, kwa kufikiria mambo aliyokuwa amesoma yeye mwenyewe pamoja na mambo aliyokuwa amesikia kutoka kwa wengine, alikuwa amesadikishwa kwamba ugonjwa huo ulikuwa umemletea ugonjwa wa moyo. Na kama matokeo, ijapokuwa hakuna sehemu yo yote ya mwili wake iliyokuwa na ugonjwa, akawa anaumwa kama ambavyo imeelezwa hapo juu. Baadaye, wakati alipopata msaada kutoka kwa mtaalamu mmoja uliomsaidia kuhusiana na tatizo lake la maono ya moyoni akaanza kuishi maisha yaliyomwezesha kutimiza mambo.

Akiwa mshiriki wa jamaa ambayo tatizo la kuumwa mgongo lilikuwa tatizo la kawaida, mwanamke mmoja kijana alianza kuumwa mgongo. Akasumbuka sana juu ya jambo hilo walakini akaogopa kumwendea daktari, akifikiria kwamba jambo baya zaidi limempata. Kadiri alivyozidi kuwa na wasiwasi, ndivyo maumivu yalivyozidi kuongezeka. Mwishowe, akamwendea daktari, lakini akaambiwa kwamba daktari haoni sababu ya tatizo lake. Tatizo lilikuwa nini? Mwanamke huyo alianza kuumwa mgongo kwa mara ya kwanza wakati alipopatiwa madaraka zaidi kuhusiana na kazi yake ya kimwili. Yeye alipatwa na wasiwasi kwa kufikiri kwamba huenda akakosa kufaulu katika kazi yake hiyo. Kisha ule wasiwasi uliompata juu ya maumivu ukazidisha kuumwa mgongo. Baada ya kujua cha tatizo lake, mwanamke huyo aliacha kuwa na wasiwasi, nayo maumivu yake yakakoma.

Hiyo ni mifano michache tu inaoonyesha kwamba maono ya moyo yana matokeo yenye nguvu sana katika hali ya afya ya mwili wa mtu. Hata bila kujua, mtu anaweza kuwa adui yake yeye mwenyewe. Kulingana na kitabu Encyclopedia Americana (chapa ya 1977, Kitabu cha 22, uku. 732), ‘inakadiriwa kwamba 50 kwa mia ya wagonjwa wote wanaopata matibabu wana magonjwa yanayoweza kuitwa, kwa sehemu au kwa kamili, magonjwa yanayosababishwa, au kuendelezwa na maono ya moyoni.’ Inaelekea kwamba moyo unakuwa mwepesi sana katika kupatwa na mikazo ya maono ya moyoni.

Imekuwa wakati wa karne hii ya 20 tu ambapo madaktari wamekubali maoni ya kwamba matatizo ya maono ya moyoni huenda yakawa ndiyo yanayosababisha magonjwa mengi. Walakini, Yehova Mungu, Muumba wanadamu, alifunua jambo hilo katika Neno lake, Biblia. Kwa mfano, humo twasoma hivi: “Moyo ulioyotulia ndio uzima wa nyama ya mwili, lakini wivu ni ugonjwa mifupani.” (Mit. 14:30, NW) Hali roho iliyotulia ina matokeo mema juu ya moyo, kuwaonea wengine wivu kwaweza kuharibu hali njema ya mwili wa mtu.

Kwa kuwa maono mengine ya moyoni yaweza kuwa yenye kuharibu, tunahitaji kuyazuia. Kutenda kupatana na Maandiko kwaweza kutusaidia. Lakini namna gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki