Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 10/1 kur. 3-4
  • Ni Nani Anayehitaji Maumivu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nani Anayehitaji Maumivu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MAUMIVU YA MWILINI YANAWEZA KUFAIDI
  • MAUMIVU AMBAYO HAKUNA ANAYEYATAMANI
  • Maumivu Ambayo Hayatakuwapo Tena
    Amkeni!—1994
  • Waja—Ulimwengu Usio na Maumivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Maendeleo Katika Kutibu Maumivu
    Amkeni!—1994
  • Dunia Isiyo na Maumivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 10/1 kur. 3-4

Ni Nani Anayehitaji Maumivu?

MWANAMKE huyo kijana alikuwa mwenye akili na alionekana kuwa bila kasoro. Hata hivyo yeye alikuwa tofauti sana na watu wengine. Akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu, aliwashangaza sana madaktari wa Kanada wanaochunguza magonjwa yanayohusu neva (mishipa ya fahamu). Hata alipochomwa mwilini kwa sindano, au aliposhtushwa kwa kutumia umeme (stimu), mwanamke huyo hakuona maumivu.

“Ndipo,” likaripoti gazeti Science Digest, “Ago. 28, 1955, alilazwa hospitalini, akiwa ameambukizwa vibaya sana; kwa mara ya kwanza katika maisha yake, akapata kuona maumivu naye akapewa dawa za kuyatuliza. Alikufa siku mbili baadaye, akiwa na umri wa miaka 29, nao uchunguzi wa maiti ulifunua kwamba alikuwa na ubongo timamu pamoja na utaratibu wa mishipa ya fahamu.”​—Julai, 1978, uku. 35.

MAUMIVU YA MWILINI YANAWEZA KUFAIDI

Duniani pote kwaweza kuwa na watu mamia, au hata maelfu, ambao hawaoni maumivu ya mwilini. Ukikumbuka mateso ambayo huenda ukayapata kutokana na maumivu ya mgongo, maumizo na mengineo, huenda ukawa unafikiri kwamba inaweza kuwa baraka ikiwa hungeweza kuona maumivu. Ni kana kwamba unasema, ‘Ni nani anayehitaji maumivu?’

Lakini namna gani kama ukiteguka kifundo cha mguu wako? Namna gani kama ukianguka na kuvunja mkono wako. Au namna gani kama ukipatwa na ambukizo baya sana? Kwa wazi, lingekuwa jambo jema kuweza kuona maumivu ya mwilini ili uweze kuitikia na kuchukua hatua za kuponya bila kukawia. Vivyo hivyo, uwezo wa kuona maumivu (kama vile unavyoweza kugusa kitu chenye moto pasipo kujua) waweza kutokeza tendo linaloweza kuzuia usiumie zaidi. Kwa kweli, kutokuona maumivu kunaweza kuhatirisha maisha yako. Maumivu yaweza kukufaidi.

MAUMIVU AMBAYO HAKUNA ANAYEYATAMANI

Ndiyo, kuweza kuona maumivu ya mwilini kwaweza kukufaidi. Walakini namna gani maumivu ya akilini na ya moyoni? Mara nyingi namna hii ya maumivu huendelea kwa muda mrefu nayo inaumiza sana. Dawa, matibabu au upasuaji vyaweza kupunguza au kumaliza maumivu ya mwilini. Walakini, maumivu ya moyoni na ya akilini yaweza kumfanya mtu akonde sana nayo yaweza kumtaabisha sana mtu kwa muda wa miaka mingi.

Bila shaka msiba huleta maumivu ya moyoni. Watu wenye kuitikia, wenye fadhili mara nyingi wanataabika sana kuona wanadamu wenzao wakitaabika, pengine kwa sababu ya umaskini, njaa na kukosa chakula chenye afya. Na, kwa hakika, ni jambo lenye kuumiza sana sana kupatwa na magumu kama hayo na kukosa vitu vya lazima sisi wenyewe.

Uonevu vilevile huleta maumivu ya moyoni na ya akilini. Kwa mfano, wenye kuonea waweza kutokeza hali yenye kuogopesha sana. Jambo hilo lenyewe laweza kutaabisha sana, achia mbali magumu makali yanayowapata kila siku wale wanaoonewa.

Ugonjwa waweza vilevile kutokeza maumivu ya moyoni, hata kwa mtu ambaye si yeye anayeumwa. Je! si jambo linaloumiza sana kumwona mtu anayependwa akifa polepole kwa ugonjwa wenye kuua? Na sana sana inakuwa hivyo ikiwa mgonjwa huyo anaona maumivu makali sana ya mwilini.

Kifo cha mshiriki wa jamaa apendwaye au rafiki chaweza vilevile kutokeza maumivu makali ya moyoni. Mfalme Daudi wa Israeli alionyesha kwamba alipatwa na maumivu kama hayo ya ndani kwa sababu ya kifo cha mwanawe, kwa kuwa baba huyo mwenye kuomboleza alilia kwa sauti, akisema hivi: “Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu!”​—2 Sam. 19:4.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetamani kuona maumivu ya akilini. Na kwa kweli hakuna mtu ambaye hutamani kuona maumivu makali ya mwilini. Ni nani atakaye kuteseka? Hata hivyo, ni nani awezaye kufanya jambo lo lote juu ya maumivu ambayo yamekuwa sehemu kubwa sana ya maisha ya wanadamu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki