Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 6/22 kur. 8-10
  • Maendeleo Katika Kutibu Maumivu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maendeleo Katika Kutibu Maumivu
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mahali Ambapo Maumivu Hutibiwa
  • Jinsi Maumivu Yawezavyo Kutibiwa
  • Matazamio ya Maponyo
  • Maumivu Ambayo Hayatakuwapo Tena
    Amkeni!—1994
  • Ni Nani Anayehitaji Maumivu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Ni Zaidi ya Adui Mkatili
    Amkeni!—1994
  • Waja—Ulimwengu Usio na Maumivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 6/22 kur. 8-10

Maendeleo Katika Kutibu Maumivu

KUFIKIA hivi majuzi ni madaktari wachache tu waliojua mengi sana juu ya maumivu, na wengi bado hawajui. Dakt. John Liebeskind, aliyekuwa msimamizi wa Wakf wa Kimataifa Kwa Ajili ya Wenye Maumivu, alionelea hivi miaka michache iliyopita: “Mimi sifikiri kuna shule ya kitiba ulimwenguni ambamo zaidi ya saa nne kati ya miaka minne hutumiwa kufundisha wanafunzi kuchunguza na kutibu matatizo ya maumivu.”[1]

Hata hivyo, hatua za kuelewa maumivu zimefikiwa wakati mmoja na jitihada za kuyatibu. Hivyo, tazamio la wenye kuteswa na maumivu limekuwa jangavu. “Sote twaweza kuwa na shukrani,” likaripoti gazeti American Health, “kwa sababu sasa tiba yatambua kwamba maumivu si dalili tu, bali hayo yenyewe ni ugonjwa wenye kutibika.”[2] Maoni haya yamechangia ongezeko kubwa ajabu katika hesabu ya kliniki za kutibu maumivu.

Mahali Ambapo Maumivu Hutibiwa

Dakt. John J. Bonica alifungua kliniki ya kwanza ya kutibu maumivu ya namna nyingi katika Marekani. “Kufikia 1969 kulikuwa na kliniki 10 tu za jinsi hiyo ulimwenguni,” akaripoti.[3] Lakini hesabu ya kliniki za kutibu maumivu zimeongezeka ajabu katika miaka 25 iliyopita. Sasa kuna kliniki zaidi ya elfu moja za kutibu maumivu, na mwakilishi mmoja wa shirika la kusambaza nje huduma za kutibu maumivu ya daima alisema kwamba “[kliniki] zilizo mpya hufunguliwa kila siku.”a[4]

Fikiria hilo lamaanisha nini! “Sasa wagonjwa waliokuwa wakilazimika kusafiri mamia au maelfu ya kilometa kupata kitulizo cha maumivu makubwa waweza kuyapata karibu na nyumbani,” akasema Dakt. Gary Feldstein, mtaalamu wa kugandisha maumivu katika New York City.[5] Ikiwa wewe ndiye mwenye kuteseka, yaweza kuwa baraka iliyoje kupokea msaada kutoka kwa kikoa cha wataalamu waliozoezwa kutibu maumivu!

Linda Parsons, mke wa mwangalizi anayesafiri wa Mashahidi wa Yehova, aliteswa na maumivu ya mgongo kwa miaka mingi. Alitafuta msaada kutoka kwa tabibu hadi tabibu, na bado maumivu yake yakaendelea bila kupungua. Siku moja katika Mei mwaka uliopita, akiwa karibu kukata tamaa, mume wake alichukua kitabu cha simu akatazama orodha ya mashirika ya maumivu. Iliyoorodheshwa ilikuwa namba ya simu ya kliniki moja ya maumivu isiyo mbali sana na mahali walipokuwa wakitumikia kusini mwa California. Mpango wa kwenda huko ulifanywa, na siku chache baadaye Linda akakutana na daktari ili amchunguze akadirie hali yake kwa mara ya kwanza.[6]

Mipango ilifanywa kumtibu Linda akiwa mgonjwa wa nje. Alianza kuizuru kliniki mara tatu kwa juma ili kupata matibabu na pia akafuata programu ya matibabu akiwa nyumbani. Katika muda wa majuma machache, alianza kuhisi maendeleo makubwa. Mume wake aeleza hivi: “Namkumbuka akisema hivi jioni moja akiwa ni kama amestaajabu, ‘Nashindwa kuamini kwamba ni kama sihisi maumivu yoyote.’” Katika muda wa miezi kadhaa, ikawa aweza kuacha ziara za kawaida kwenye kliniki hiyo.[6a]

Msaada ambao Linda alipokea wa kudhibiti maumivu yake ni kama ule ulioandaliwa na kliniki za kutibu maumivu ya namna nyingi. Kliniki ya jinsi hiyo hutumia ustadi wa kikoa cha wataalamu wa afya. Kulingana na Dakt. Bonica, ustadi huo ndio “mfikio bora wa kushughulika na maumivu ya daima.”[7] Kwa kielelezo, Linda alitibiwaje maumivu yake?

Jinsi Maumivu Yawezavyo Kutibiwa

Broshua moja ya kliniki yaeleza hivi juu ya utaratibu ufuatwao mtu awasilipo: “Kila mtu huchunguzwa na tabibu kwa uangalifu ili kukadiria sababu ya maumivu kisha miradi na programu zifaazo za matibabu hupangiliwa. . . . Mbinu na mifikio ya kitaalamu hutumiwa kuusaidia mwili kufungulia ‘endofini’ (kemikali zifanyizwazo kiasili mwilini) ili kupunguza maumivu na wasiwasi na kuepuka kutegemea dawa za kupunguza maumivu.”[8]

Miongoni mwa matibabu ambayo Linda alipokea yalikuwa utibabu wa kupachikapachika visindano mwilini na TENS, ambalo lamaanisha kuingiza vichochea-hisia katika mishipa ya fahamu kwa kupitisha mikondo ya umeme katika ngozi.[8a][9] Yeye alipokea kwenye kliniki matibabu ya kuchochea hisia kwa mikondo ya umeme na kuandaliwa kipimo kidogo cha TENS akitumie nyumbani. Ule utaratibu wa kufunza mgonjwa kurekebisha maitikio ya mwili wake na kuyarekebisha ili yapunguze wingi wa maumivu ulitumiwa pia.[9a][10]

Utibabu wa kukanda mwili, kutia na kukanda tishu na misuli ya chini ya ngozi, ulikuwa sehemu ya matibabu yake. Baadaye, programu ya mazoezi katika sehemu ya kliniki ya mazoezi ya kunyosha maungo ilianzishwa, lakini baada tu ya Linda kuwa tayari kwa jambo hilo, na hiyo ikawa sehemu muhimu ya matibabu. Mazoezi ni muhimu, kwa kuwa imeonwa kuwa hayo hurudisha endofini zilizokamuliwa na maumivu ya daima.[11] Hata hivyo, tatizo huwa ni kuwasaidia watu wenye maumivu waweze kufuata programu ya mazoezi yenye manufaa.[12]

Watu wengi wanaokuja kliniki mbalimbali wakiteswa na maumivu ya daima wanatumia dawa nyingi za kupunguza maumivu, na Linda hakuwa tofauti na hao. Lakini muda si muda akawa ameachishwa dawa zake, na huo ni mradi wa maana wa kliniki za kutibu maumivu. Linda hakupatwa na zile dalili kali za kuacha kutumia dawa, hata hivyo hiyo ni kawaida. Mstadi wa maumivu Dakt. Ronald Melzack alisema kwamba katika “uchunguzi mmoja wa watu zaidi ya 10,000 waliochomwa na moto . . . , hakuna hata mtu mmoja ambaye baadaye alikuja kuwa mraibu wa kutumia dawa angeweza kusemwa alifanya hivyo kwa sababu ya dawa alizopewa kutuliza maumivu alipokuwa akikaa hospitalini.”[13]

Kwa kuwa mara nyingi maumivu ya daima huhusiana sana na hali ya mawazo ya mtu, kliniki hujaribu kusaidia wagonjwa wajifunze kuondoa maumivu hayo akilini.[14] “Lile ufikirialo,” akaeleza Dakt. Arthur Barsky, profesa mmoja kwenye Shule ya Tiba ya Harvard, “lile utarajialo, kadiri yako ya kujali hisia zako—mambo yote haya yana uvutano mkubwa ajabu juu ya lile uhisilo hasa.”[15] Kwa hiyo wagonjwa husaidiwa kukaza fikira juu ya mambo tofauti na maumivu yao.[16]

Matazamio ya Maponyo

Je! kliniki hizi mpya za kutibu maumivu ndilo jibu kwa matatizo ya maumivu ya wanadamu? Ingawa njia za kutibu maumivu zilizoelezwa hapa zaweza kusaidia, ni lazima mtu atumie uangalifu katika kuchagua kliniki hodari au mtaalamu wa maumivu. Hata hapo, ni lazima matarajio ya mtu yawe kuona mambo kihalisi.[17]

Hiki ni kielelezo cha hadithi halisi ya mafanikio: Stephen Kaufman, aliyekuwa mnyanyua-uzani wa Olimpiki, alibaki akikaribia kuwa asiyejiweza kabisa kwa sababu ya maumivu ya daima yaliyompata wakati jambazi alipompiga risasi shingoni. Baada ya miezi minane ya programu ya kutibiwa maumivu, aliweza kurudia kufanya kazi wakati wote na mwishowe hata akarudia kunyanyua uzani katika mashindano. Hata hivyo alisema hivi: “Mara nyingi, vidole vyangu vya miguu huniwasha kama kwamba vimo katika maji yanayochemka.”[18]

Kwa hiyo kujapokuwa na maendeleo yote yale ya kusisimua, ni wazi kwamba mwanadamu hawezi kuitimiza ahadi ya Biblia: “Maumivu hayatakuwapo tena.” (Ufunuo 21:4) Basi, mradi huo waweza kufikiwa jinsi gani?

[Maelezo ya Chini]

a Amkeni! haliungi mkono kliniki yoyote hususa ya kutibu maumivu au njia yoyote ya matibabu.

[Picha katika ukurasa wa 9]

Njia za kutibu maumivu, kutia na kuchochea mishipa ya fahamu kwa kutumia mikondo ya umeme

[Hisani]

Hisani ya Pain Treatment Centers of San Diego

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki