Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 9/15 kur. 3-4
  • Onyo Ambalo Hawakutii

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Onyo Ambalo Hawakutii
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Maonyo Yanayopaswa Kufuatwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Uko Macho Kuelekea Nyakati Zetu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Wanasarakasi wa Majabali ya Milima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Barafu Juu ya Ikweta
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 9/15 kur. 3-4

Onyo Ambalo Hawakutii

SIKU ya Mei 18, 1980, Mlima St. Helens katika United States ulilipuka baada ya kutulia kwa miaka 123. Mlipuko huo mkubwa uliruka juu futi 1,300 kutoka kilele cha mlima, ukaharibu mailia za mraba karibu 230 za eneo zuri la nchi, na kuua watu zaidi ya 60.

Mlipuko huo haukutokea pasipo onyo. Karibu miezi miwili mapema, tetemeko kubwa la ardhi lilitikisa eneo hilo, na matetemeko zaidi yakafuata yakiongezeka-ongezeka. Siku ya Machi 27, mlima ulirusha majivu na mvuke wenye joto uliopanda juu maili 4 hewani.b Ingawa mlima ulikuwa umetulia kwa kiasi fulani kufikia mwezi Aprili, sehemu moja ilionekana ikifura katika uso wa kaskazini wa mlima, na ilikuwa ikiongezeka kwa kiasi cha futi 5 kwa siku.

Kwa wanasayansi, ishara hizo zilionyesha wazi kwamba mlipuko ulikuwa karibu. Maonyo yalitolewa ili watu watoke karibu na mlima huo. Lakini watu wengi hawakutii maonyo hayo.

Harry Truman, mtu mwenye kukodishia watu mahali pa kulala kwenye Ziwa Spirit karibu na sehemu ya chini ya mlima, alikataa kuondolewa hapo. Alikuwa ameishi hapo kwa miaka 50 naye akakataa kuamini kwamba mlima wake mpendwa ungeondoa utulivu wa mazingira yake. Watu wengine waliendesha magari yao kwa kuviepa vizuizi vilivyowekwa katika barabara za kuingia mbali msituni kwenye miti ya kukatwa ili wakapige kambi kule na kuutazama mlima katika mwitu huo uliowadanganya kuwa ni wenye amani.

Mlipuko ule mkubwa sana ulipotukia, gesi na majivu yenye moto yalirushwa kutoka mlimani kwa miendo ya maili 200 kwa saa! Misunobari ilitandazwa chini kwa mamilioni, na maisha za watu hao wasiotii zikafagiliwa mbali. Wengine walikufa wakiwa wameshika kamera zao kupiga picha. Harry Truman na makao yake ya kukodisha wenye kulala humo alizikwa chini ya matope yenye kuchemka ya futi 40.

Mitiririko ya matope ilitoka mlimani kwa mwendo wa kasi kufikia maili 50 kwa saa. Rubani mmoja wa helikopta alipoonya watu waliokuwa mahali ambapo matope hayo yangepita, wengine walikataa kutii maneno yake. Yeye alisema: “Walinishangaza sana. Mimi niliwaambia ni kitu gani kinakuja nao wakacheka tu na kunipungia mikono niende zangu.” Muda mfupi baadaye kicheko chao kikawa bumbuazi.

Jambo hilo la kukataa kuamini maonyo yanayotegemeka ni la kawaida, hasa wakati maonyo yenyewe yanapohusu jambo ambalo watu hawajapata kuona kwa macho yao wenyewe. Wao wanawaza kwamba hakuna kitu kitakachobadilika kwa sababu hali zinazowazunguka zimeendelea kuwa ivyo hivyo tangu siku za babu zao. Kuwa na mwelekeo huo kutaleta msiba ikiwa kutafanya mtu apuuze onyo fulani la kale linalohusu maangamizi yanayokuja yatakayoupita kwa mbali mlipuko ule wa Mlima St. Helens. Hayo ni maangamizi gani? Nawe una mwelekeo gani kuhusu onyo hilo? Je! Utalipungia mkono onyo hilo ukilipuuza kwa kutokuamini, au wewe una nia ya kulitii uishi? Ona ni mambo gani yaliyo katika makala inayofuata.

[Maelezo ya Chini]

a Futi moja ni meta 0.3; maili 1 ya mraba ni kilometa za mraba 2.6

b Maili moja ni kilometa 1.6.

[Picha Credit Line katika ukurasa wa 3]

H. Armstrong Roberts

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki