Muono-Ndani Juu ya Habari
Wagoni-Jinsia-Moja—Je! Wako Sawa Mbele za Mungu?
Katika mkoa wa Australia wa Queensland, vitendo vya ugoni-jinsia-moja—hata vikifanywa faraghani na wenzi wenye kukubaliana—si halali. Hivi majuzi, kikundi kimoja kikuu cha kanisa katika mkoa huo kilitoa maoni thabiti dhidi ya sheria hizo; wao wataka ugoni-jinsia-moja uache kuonwa kuwa ni uhalifu.
Kulingana na gazeti The Courier-Mail, hiki Kikundi cha Kudai Haki kwa Ushirikiano wa Kanisa na Jamii ni cha washiriki wa makanisa ya Anglikana, Katoliki ya Kiroma, Lutheri, Baptisti, na Uniting na Wakweka (Sosaiti ya Friends). Kikidai kwamba sheria zilizopo dhidi ya wagoni-jinsia-moja zina msingi wa kukosa maarifa na maoni ya ubaguzi, kikundi hicho kilitaarifu hivi: “Tegemezo letu kwa maoni haya lina msingi wa ile imani ya kwamba watu wote ni sawa mbele za Mungu na wapaswa kuwa sawa mbele ya sheria. Sisi twaamini mtu aliye mgoni-jinsia-moja si mtu-binadamu amzidiye wala kumpungua mtu afanyaye ngono na jinsia tofauti.
Ingawa ni kweli kwamba wanadamu wote huzaliwa wakiwa sawa, maoni ya Mungu ni nini juu ya ugoni-jinsia-moja? Katika Biblia, vitendo vyote vya ugoni-jinsia-moja hushutumiwa kuwa visivyo vya kiasili na vyenye kustahili kukosa kibali cha Mungu, vikiongoza kwenye kifo. Ilikuwa hivyo si katika Israeli ya kale tu bali pia katika nyakati za Kikristo. (Walawi 18:22; Warumi 1:26, 27) Laana kali i wazi na haihitaji fasiri yoyote: “Waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, . . . wala wafiraji, wala walawiti [wanaume ambao hulala na wanaume, NW].”—1 Wakorintho 6:9, 10.
Badala ya kupiga makelele wakidai ugoni-jinsia-moja uache kuonwa kuwa ni uhalifu, Wakristo wa kweli huhimiza wale waliofanywa watumwa wa zoea hili lenye kuvunjia Mungu heshima waachane nalo kwa kugeukia Neno la Mungu la ukweli.
Hatari za Damu Zaendelea
Uchunguzi mmoja wa hivi majuzi ulifunua kwamba mamia ya makosa yamefanywa na Msalaba Mwekundu wa Amerika katika kushughulikia damu yenye viini vibaya. Karibu nusu ya yuniti milioni 12 hadi milioni 15 za damu itumiwayo katika United States kila mwaka hugawanywa na Msalaba Mwekundu wa Amerika. Wakati yuniti zozote za damu zenye kupelekwa nje zipatikanapo kuwa na viini vibaya, shirika FDA (Food and Drug Administration), la serikali ya mwungano lapasa kujulishwa. Hata hivyo, The New York Times yataarifu kwamba mkaguzi wa serikali ya mwungano ashikilia kwamba Msalaba Mwekundu haukufanywa hivyo mara nyingi. Adai kwamba ukaguzi wa rekodi zao ulifunua visa 380 ambamo utumizi usiofaa wa damu yenye viini vibaya haukuripotiwa kwa serikali. Kwa kuongezea, kati ya visa 228 vya UKIMWI ambavyo huenda vikawa vilisababishwa na visa vya kutiwa damu mishipani, mkaguzi huyo aligundua kwamba Msalaba Mwekundu uliripoti 4 tu kwa FDA.
Ingawa wengi wangali waiona kuwa yenye kuokoa uhai, damu yenye kutiwa mishipani husababisha kifo cha maelfu kila mwaka. Hata hivyo, waabudu wa kweli wa Mungu, kwa kutii sheria zake kwa habari ya damu hulindwa wakati ule ule na hatari za kutiwa mishipani. Mungu aliamuru hivi: “Ni lazima wewe usiile damu; imwage juu ya ardhi kama maji . . . ili kwamba mambo yaende vema kwako wewe na kwa watoto wako baada yako, kwa sababu utakuwa unafanya lifaalo.”—Kumbukumbu 12:23-25, New International Version.
Papa Katika Utumishi wa Kijeshi
Mwaka uliopita papa alikutana na makadeti wa kijeshi (wanajeshi wasiohitimu bado) zaidi ya 7,000 kwenye makao-jeshi ya Cecchignola huko Roma. Wakati huo maofisa vijana wanne wenye kuwakilisha makao-jeshi hayo walimwuliza papa kama utumishi wa kijeshi wapatana na dhamiri ya Kikristo. Kihususa, kulingana na gazeti la Jiji la Vatikani L’Osservatore Romano, waliuliza hivi: “Je! mtu aweza kuwa Mkristo mwaminifu na, wakati ule ule, awe askari-jeshi mwaminifu?” Kwa kujibu papa alisema hivi: “Hakuna ugumu wa msingi wala kutowezekana katika kuungamanisha wito kwenye kazi ya Kikristo na ule wa utumishi wa kijeshi. Tukiutazama huu wa pili kwa maoni chanya, waweza kuonwa kuwa jambo lenye upendezi, lenye ustahili na linalofaa kulifanya.”
Hata hivyo, je! maoni ya jinsi hiyo yapatana na kutokuwamo kulikodumishwa na Wakristo wa mapema? Katika kitabu chake An Historian’s Approach to Religion, Arnold Toynbee ataja kisa cha Maximilianus, mfia-imani mmoja wa karne ya tatu ambaye, alipotishwa kuuawa na mahakama ya Kiroma kwa kukataa kuingizwa jeshini, alisema hivi: “Mimi sitatumikia. Mwaweza kunikata kichwa, lakini mimi sitatumikia mamlaka za Ulimwengu Huu; mimi nitatumikia Mungu wangu.” Kwa nini, ijapokuwa kukabiliwa na kifo hakika, yeye alikataa kushiriki katika utumishi wa kijeshi? Kwa sababu aliwachukua wafuasi wa kweli wa Yesu kuwa “si sehemu ya ulimwengu” kama vile Yesu hakuwa sehemu ya ulimwengu. Zaidi ya hilo, aliiona vita ya Kikristo kuwa ya kiroho, kupatana na maneno ya mtume Paulo: “Hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili . . . maana silaha za vita vyetu si za mwili.”—Yohana 17:16, NW; 2 Wakorintho 10:3, UV.