Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 12/15 uku. 21
  • Muono-Ndani Juu ya Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muono-Ndani Juu ya Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kakatazwa Kuoa
  • Kwa Nini Jeuri Nyingi Sana?
  • Uko Wapi “Mji wa Daudi”?
  • “Tatizo Kubwa la Kingono Kati ya Makasisi
    Amkeni!—1991
  • “Jina Jipya”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
  • Waliodhulumiwa Kingono na Mapadri Wakiwa Watoto Wateta Waziwazi
    Amkeni!—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 12/15 uku. 21

Muono-Ndani Juu ya Habari

Kakatazwa Kuoa

Likielezwa na askofu mmoja Mlutheri kuwa ni “tatizo lililofichika kwa muda wa vizazi,” mwenendo mbaya wa ngono miongoni mwa makasisi mwishowe umetokea wazi. Hata hivyo, Los Angeles Times linaripoti kwamba pamoja na huo imekuja “mambo ya kuaibisha yaliyofichuliwa peupe na kesi za gharama kubwa ambazo zimelazimisha makanisa kadhaa kufilisika.” Times linaandika kwamba mawakili wa bima wanasema kwamba zaidi ya kesi 2,000 zinangoja mahakamani zikihusisha makasisi.

Linalostahili kuangaliwa, pia, ni kwamba inaripotiwa kwamba wengine wa wakosaji wenye sifa mbaya zaidi wanaripotiwa kuwa makasisi wa Katoliki ya Kiroma. A. W. Richard Sipe, mwanatiba wa kutuliza akili aliyekuwa mtawa wa Benedictine, ameongoza mahoji na mapadri 1,000 na wanaume na wanawake wengine 500, wengi wao wakidai walishiriki katika utendaji wa ngono pamoja na makasisi. Gazeti Time linaripoti makadirio yake kwamba karibu nusu ya mapadri 53,000 wa Katoliki ya Kiroma katika United States wamevunja ahadi yao ya kutokuoa. Kulingana na Sipe karibu asilimia 28 ya mapadri wote wanaendelea kufanya ngono na wanawake, huku asilimia 10 mpaka 13 wakihusika kingono pamoja na wanaume watu wazima, na asilimia 6 wakifuatia watoto kwa ajili ya ngono, kwa kawaida wavulana. Kesi zaidi ya 100 zilizotatuliwa kwa mwenendo mbaya wa makasisi katika muda wa miaka sita iliyopita zimegharimu wenye mamlaka Wakatoliki kati ya dola milioni 100 na 300.

Watu wengi wanaona kwamba yaliyo mengi ya matatizo haya yangemalizwa ikiwa mapadri wangeruhusiwa kufunga ndoa. Huenda watu fulani wakashtuka kujua kwamba hakuna mahali popote ambapo Biblia inakataza wahudumu Wakristo wa Mungu kufunga ndoa. Hata hivyo, Kanisa Katoliki limekataza kuoa tangu karne ya 12. Kwa kupendeza, wakati wa kutaja ule uasi-imani mkubwa kutoka kwenye ibada ya kweli ambao ungeingia baada ya kifo cha mitume, Paulo aliandika kwamba “wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, . . . wakiwazuia watu wasioe.”—1 Timotheo 4:1-3.

Kwa Nini Jeuri Nyingi Sana?

Canada ilishtuka na kugutuka vibaya kwa kujua kwamba Marc Lepine wa miaka 25 alikuwa ameua watu wengi katika eneo la Chuo Kikuu cha Montreal. Akiwa mtulivu alichinja kwa ukatili kabisa wanafunzi 14 wa kike wa somo la uhandisi, akiacha 13 wengine wakiwa wamejeruhiwa, kutia na wanaume 4, kabla ya kujigeuzia bunduki yeye mwenyewe. Lilikuwa moja la machinjo mabaya zaidi katika historia ya taifa. Waziri Mkuu alieleza mauaji hayo ya kijinga kuwa “msiba wa kibinadamu wa kadiri kubwa sana.”

Kama ilivyo katika nchi nyinginezo, uuaji wa watu wengi unaongezeka katika Canada. Kulingana na The Toronto Star, “kumekuwa na mauaji zaidi ya 100 ya watu wengi tangu Vita ya Ulimwengu 2 na yaliyo mengi kati yayo yalitokea katika makumi mawili ya miaka iliyopita.” Hata hivyo, kama vile baba ya mmoja aliyepatwa na mabaya ya Lepine alivyouliza kwa majonzi: “Kwa nini kuna jeuri nyingi sana katika ulimwengu? Kwa nini wanadamu wanafanyiana jambo kama hili?”

Elezo la Biblia kwa ongezeko la jeuri katika wakati wetu linaonekana wazi. Mtume Yohana aliandika hivi: “Ulimwengu wote unatawaliwa na yule Mwovu.” (1 Yohana 5:19, HNWW) Kama vile hewa tunayopumua, roho mbaya inayotoka kwa Shetani inatawala fikira, tamaa, vitendo vyenyewe vya wanadamu. Roho yake ya uasi, ubinafsi, na kiburi ndiyo ‘inayodanganya ulimwengu wote.’ (Ufunuo 12:9) Hata hivyo, waabudu wa kweli wa Mungu wanapata faraja katika kujua kwamba “dunia [ulimwengu, NW] inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”—1 Yohana 2:17.

Uko Wapi “Mji wa Daudi”?

Kama wewe ungetembelea Yerusalemu, na uombe mtu fulani akuelekeze kwenye Mlima Sayuni, inaelekea sana ungepelekwa kwenye kigongo, au kilima, kinachoendelea kusini ya ule Mji wa Zamani. Kwa kupakana mashariki na Bonde la Tyropoeon na magharibi na Bonde la Hinomu, kilima hiki kinatiwa alama na kuwapo kwa Kanisa la Dormition, kilicho na kuba yenye umbo la pia.

Hata hivyo, ramani na picha zilizochapishwa na Watch Tower Society zinaweka Mlima Sayuni juu ya kilima kidogo zaidi mashariki ya ule ambao leo unaitwa Mlima Sayuni. Kilima hiki kimetenganishwa na kilima kingine magharibi na Bonde la Tyropoeon na kupakanwa mashariki na Bonde la Kidroni.

Kati ya mahali hapa pawili ni wapi ulipokuwa Mlima Sayuni wa asili? Gazeti Biblical Archaelogy Review (Mei/Juni 1990) linakubali kwamba “kile kigongo, au kilima, cha mashariki ndicho kilichokuwa Mlima Sayuni wa asili, . . . ambao Mfalme Daudi aliuteka kutoka kwa Wayebusi.” Baada ya anguko lake, ngome hii ya Kiyebusi ilikuja kujulikana kuwa “Mji wa Daudi,” ulioitwa “Sayuni” pia. (2 Samweli 5:7) Hilo Biblical Archaeology Review linasema kwamba “wachimbuzi wa vitu vya kale wameamua, pasipo shaka, kwamba kigongo hiki chembamba cha mlima,” ambacho mara nyingi kinaitwa kilima cha mashariki, ndicho Mlima Sayuni wa Kibiblia ambapo Daudi alisimamisha makao ya usimamizi na ya dini kwa ajili ya taifa la Israeli.—2 Samweli 6:11, 12, 17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki