Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 11/1 kur. 2-4
  • Muungano wa Ulimwengu—Je, Utapata Kuwa Uhalisi Wakati Wowote?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muungano wa Ulimwengu—Je, Utapata Kuwa Uhalisi Wakati Wowote?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Muungano wa Ulimwengu Wakaribia?
  • Faraja kwa Walioonewa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Muungano wa Ulimwengu—Utakujaje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Mwisho wa Vita Vyote—Je! Unaweza Kufikiwa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Walioungana Katika Njia Bora Zaidi ya Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 11/1 kur. 2-4

Muungano wa Ulimwengu—Je, Utapata Kuwa Uhalisi Wakati Wowote?

“TUKIWEZA kufaulu katika vizazi vichache vyenye kufuata, kuugeuza umbo ulimwengu wa mataifa huru ambamo twaishi, kuwa namna fulani ya jamii ya kweli ya kimataifa, . . . basi tutakuwa pia tumebatilisha kwa matokeo shirika la kale la shughuli za vita . . . Hata hivyo tukishindwa, labda kutakuwa . . . hakuna ustaarabu.” Hivyo ndivyo asemavyo mwanahistoria wa kijeshi Gwynne Dyer katika kitabu chake chenye kichwa War.

Rekodi za historia, asema Dyer, zajawa na masimulizi ya mataifa na vikundi vingine vyenye nguvu vilivyoishia kupigana vita ili kusuluhisha tofauti zao. Ukosefu wao wa muungano uliangamiza kabisa uhai wa mamilioni ya wahasiriwa. Ufafanuzi wa Mfalme Solomoni wa jinsi jambo hilo lilivyoathiri watu katika siku yake bado wafaa leo. Aliandika hivi: “Nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji.”—Mhubiri 4:1.

Siku hizi, kama mwanahistoria aliyetajwa juu aonyeshavyo, mbali na kuhurumia “machozi yao waliodhulumiwa,” kuna sababu zaidi ya kupata njia fulani ya kugeuza umbo ulimwengu wa mataifa huru kuwa namna fulani ya jamii ya kweli ya kimataifa: Kule kuokolewa kwenyewe kwa ustaarabu kumo hatarini! Shughuli za vita za kisasa hutoa msingi wa kutarajia kuangamizwa kwa kila taifa liishialo kwenye shughuli hizo na hazitaacha washindi wowote.

Muungano wa Ulimwengu Wakaribia?

Muungano wa ulimwengu una matazamio gani? Je, jamii ya kibinadamu yaweza kushinda kani zenye kutenganisha ambazo zatisha kuokolewa kwa dunia? Watu fulani hufikiri hivyo. Mhariri wa mambo ya ulinzi wa gazeti la habari la Daily Telegraph la Uingereza, John Keegan, aandika hivi: “Kujapokuwa vurugu na ukosefu wa uhakika, yaonekana kuwa jambo liwezekanalo kwa mmoja kuweza kuona kule kutokea hatua kwa hatua kwa kile kionekanacho kuwa ulimwengu usio na vita.”

Ni nini limtolealo mtazamo huo wenye matumaini mema? Kwa nini watu wengi waonekana kuwa wenye tumaini ijapokuwa historia ndefu ya kibinadamu ya shughuli za vita na kuonekana kwa mwanadamu kuwa bila uwezo wa kujiongoza kwa mafanikio? (Yeremia 10:23) ‘Wanadamu wanasonga mbele. Historia yaonyesha kiolezo cha maendeleo yasiyokoma,’ watu fulani walibisha wakati mmoja. Hata leo, wengi huamini kwamba wema wa asili wa mwanadamu utashinda uovu kwa njia fulani. Je, hilo ni tumaini halisi? Au ni danganyo tu litakaloongoza kwenye kukata tamaa zaidi? Katika kitabu chake History of the World, mwanahistoria J. M. Roberts aliandika hivi kwa uhalisi: “Wakati ujao wa ulimwengu haungeweza kufafanuliwa kuwa salama salimini. Wala sasa mwisho wowote wa kuteseka kwa kibinadamu hauonekani kuwa karibu, wala hakuna msingi wowote wa kuamini kwamba kutakuwa na mwisho wa kuteseka kwa kibinadamu.”

Je, kuna sababu za kweli za kuamini kwamba watu na mataifa kwa kweli watashinda kutokuwa kwao na itibari kati yao na tofauti zenye kutenganisha? Au jambo fulani zaidi ya jitihada za kibinadamu lahitajiwa? Makala yenye kufuata itazungumzia maswali hayo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Background globe on the cover: Mountain High Maps® Copyright © 1995 Digital Wisdom, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki