Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w01 9/1 uku. 13
  • Tulikuwa Mbwa-Mwitu—Sasa Sisi Ni Kondoo!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tulikuwa Mbwa-Mwitu—Sasa Sisi Ni Kondoo!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Mwishowe Mbegu Ilichipuka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Kutoka Mshuko wa Moyo Hadi Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutatua Matatizo ya Vijana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • “Kutoka Kinywani mwa Watoto Wachanga”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
w01 9/1 uku. 13

Tulikuwa Mbwa-Mwitu—Sasa Sisi Ni Kondoo!

Mimi na Sakina tulikuwa majirani tulipokuwa wasichana wadogo. Sakina alikuwa mkubwa na mwenye nguvu, ilhali mimi nilikuwa mdogo na mwembamba. Tulikuwa tukizozana mara nyingi, lakini siku moja tukapigana sana. Kuanzia siku hiyo na kuendelea hatukuzungumziana wala kusalimiana. Hatimaye, sote tulihama mahali hapo na hakuna aliyejua mwenzake alienda wapi.

Katika mwaka wa 1994, nilianza kujifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova, na hatua kwa hatua utu wangu ukabadilika. Miaka minne baadaye nilipokuwa nikihudhuria siku ya kusanyiko la pekee huko Bujumbura, Burundi, nilishangaa kukutana na Sakina. Nilifurahi kwamba alikuweko kwenye kusanyiko hilo, lakini hatukusalimiana kwa shauku. Baadaye siku hiyo, singeweza kuamini macho yangu nilipomwona miongoni mwa waliotaka kubatizwa! Yeye pia alikuwa amebadilika sana. Alikuwa tofauti na yule mtu mgomvi niliyezozana naye mara nyingi. Lilikuwa jambo lenye kupendeza kama nini kumwona akidhihirisha hadharani kwamba amejiweka wakfu kwa Mungu kupitia ubatizo wa maji!

Alipotoka majini, nilifanya haraka kwenda kumkumbatia na kumnong’onezea kwenye sikio hivi: “Unakumbuka jinsi tulivyopigana?” “Naam, ninakumbuka, lakini hayo ni mambo ya zamani. Sasa mimi ni mtu tofauti,” akasema.

Sote wawili tuna furaha kwamba tumepata kweli ya Biblia inayofanya watu wawe na umoja na kwamba tulibadili nyutu zetu zilizokuwa kama za mbwa-mwitu zikawa kama za kondoo wa Mchungaji Mkuu, Yehova Mungu. Kwa kweli, kweli ya Biblia hubadili watu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki