Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 1/15 uku. 21
  • Ngoma Zisemazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ngoma Zisemazo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Kweli Ngoma za Kiafrika Huzungumza?
    Amkeni!—1997
  • Kuwaelimisha Wasikilizaji
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Sanduku La Swali
    Huduma Yetu ya Ufalme—2000
  • Kuwatazama Wasikilizaji
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 1/15 uku. 21

Ngoma Zisemazo

●Je! wewe umepata kuona katika sinema au kusoma katika vitabu juu ya ujumbe unaopelekwa katika mapori kwa njia ya kupiga ngoma? Je! ujumbe unaweza kupelekwa kwa usahihi kwa kugeuza namna ya kupiga ngoma na mlio wake?

Wakati wa Desemba 1970 kusanyiko kubwa la mataifa yote la Mashahidi wa Yehova lilifanywa Lagos, Nigeria. Asubuhi moja kipindi cha pekee kilifanywa kwa ajili ya wajumbe waliokuwa wakizuru kutoka Amerika ya Kaskazini na Ulaya. Historia ya Mashahidi wa Yehova ilizungumzwa katika Nigeria. Wasikilizaji walifurahishwa pia na wonyesho wa “ngoma zisemazo.”

Alitokea mpiga ngoma. Shahidi mmoja akamnong’onezea ujumbe aliopaswa atoe. Ndipo ule ujumbe ulipopigwa mara tatu katika ngoma. Wasikilizaji waliulizwa hivi, “Je! mtu ye yote wa kabila la Yoruba aliye kati ya wasikilizaji aweza kufahamu ujumbe huo?” Mara hiyo mkono ulisimamishwa juu na ule ujumbe ukatolewa katika Kiyoruba na kutafsiriwa hivi katika Kiingereza: “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.” (Mt. 6:9) Lo! kulitokea vifijo wee! Tena, ujumbe mwingine ukapigwa katika ngoma. Mtu tofauti wa kabila la Yoruba katika wasikilizaji akaufahamu mara hiyo, ukisema: “[Yehova] ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.” (Zab. 23:1) Maonyesho hayo mawili yaliondolea wasikilizaji wote mashaka wapate kusadiki kwamba kweli ngoma za Kiyoruba zaweza ‘kusema.’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki