Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 4/8 kur. 3-4
  • Miujiza na Mizuka ya Wakati Uliopita na ya Sasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Miujiza na Mizuka ya Wakati Uliopita na ya Sasa
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mizuka—Je! Ni ya Kweli au Si ya Kweli?
  • Mizuka Iliyo ya Ki-Siku-Hizi Zaidi
  • Miujiza na Mizuka— Je! Ni Ishara Zitokazo kwa Mungu?
    Amkeni!—1990
  • Miujiza na Mizuka—Kwa Nini Haihitajiwi
    Amkeni!—1990
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kuabudu Katika Maeneo Matakatifu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Kanisa—Mabadiliko na Mvurugo
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 4/8 kur. 3-4

Miujiza na Mizuka ya Wakati Uliopita na ya Sasa

Na mleta habari za “Amkeni”! katika Ufaransa

GUADALUPE, Fátima, na Lourdes—majina hayo yamaanisha nini kwako? Kwa watu wengi hiyo ni miji tu katika Meksiko, Ureno, na Ufaransa. Lakini kwa mamilioni ya Wakatoliki wenye moyo mweupe, hapo ni mahali patakatifu, na ni matatu kati ya maabadi (sehemu za ibada) ya Kimaria yaliyo maarufu zaidi ulimwenguni. Ujitoaji wa Wakatoliki kwa sehemu hizo haujafifia kamwe katika karne hii ya 20. Mathalani, katika 1982 wageni kama 4,500,000 wenye kuzuru walimiminika katika Lourdes, huku masongamano makubwa hata zaidi yakijazana Guadalupe.

Kwa Kanisa Katoliki, maabadi haya ni mahali ambapo yasemekana palitokea maponyo ya kimuujiza. Ndivyo ilivyo kuhusu Lourdes hasa, ambayo ilielezwa na Papa Pius 10 kuwa “kitovu cha ibada ya Kimaria na milki ya fumbo la Kiekaristi, ambacho chaonekana kama chenye utukufu mwingi kuliko vitovu vyote vyenye kufanana nacho katika sehemu zote za ulimwengu wa Kikatoliki.” Maelfu ya watu wamedai kuwa waliponywa wakati wa safari ya kuhiji Lourdes au baada ya hapo. Hata hivyo, kufikia sasa kanisa limetambua “miujiza” 65 tu.

Uwe waamini au huamini katika Mungu, una haki ya kuuliza maswali. Namna gani kuhusu mizuka hii, sana-sana ya Mariamu, ambayo hutukia sehemu zote za ulimwengu? Je! yale maponyo ya kimuujiza na matukio mengine yenye kushirikishwa nayo ni uthibitisho wa kibali cha kimungu? Kwenye mkutano mmoja uliofanywa katika Lourdes katika 1986, askofu wa Tours aliwatia moyo wasikiaji wake ‘watafakari juu ya maana ya ile mizuka’ ili ‘kuthibitisha mambo ya maana ambayo hupambanua kati ya mizuka isiyo ya kweli na iliyo ya kweli.’ Ikiwa wewe ni Mkatoliki, wewe pia ungeweza kupendezwa kuitazama habari hii kwa ukaribu zaidi.

Mizuka—Je! Ni ya Kweli au Si ya Kweli?

Kanisa Katoliki la Kiroma halisemi kwa uhakika kabisa kuhusu mizuka hiyo, wala halishurutishi washirika walo kuiamini. Lakini Wakatoliki wenye moyo mweupe watakata shauri gani waonapo Papa John Paul 2 akinywa maji kutoka kwenye kile kipango cha Lourdes au akiongea na Lucie, mtu mmoja pekee aliye hai ambaye aliona mzuka wa Fátima? Je! huu si wonyesho wazi kwamba yeye (na kanisa) huyakubali rasmi mambo hayo? Zaidi ya hilo, wakati wa safari zake, papa hashindwi kamwe kuzuru patakatifu mbalimbali pa Kimaria, kama lile abadi la Bikira Mweusi wa Czestochowa katika Polandi.

Sehemu nyingine zaidi za hali ya kiasi zimekubaliwa na kanisa, kama Beauraing na Banneux katika Ubelgiji. Nyakati fulani ibada huruhusiwa kwa wenyeji tu, kama ilivyo katika Tre Fontane, Italia, na Marienfried, Ujeremani.

Hata hivyo, tangu mwisho wa karne ya 19 wengi wameshikilia dai la kwamba waliona mizuka. Kitabu Vraies et fausses apparitions dans l’Église (Mizuka ya Kweli na Isiyo ya Kweli Katika Kanisa) chakadiria kwamba kulikuwako visa zaidi ya 200 kuanzia 1930 hadi 1976. Kwa nini visa vichache kadiri hiyo vilitambuliwa, hali kulingana na mtungaji wa kitabu hicho “ujumbe huo mbalimbali, isipokuwa katika visa vichache, haukuwa wa kipuuzi na, ulipochunguzwa, ulionekana kuwa ukielekea kufanana kabisa”?

Gazeti la Kifaransa L’Histoire latoa elezo kuhusu jambo hilo katika makala moja inayoshughulika na mizuka ya Mariamu ya karne ya 19 katika eneo la Loire la Ufaransa ya mashariki ya kati. Kulingana na mtungaji, kanisa halikupeleleza matukio haya na liliyaacha yakiwa yamefichamana ili kuepuka “ushindani” pamoja na maabadi ambayo yalikuwa tayari yakitambuliwa.

Leo, watu fulani wana maoni ya kwamba kitu chenye kusababisha kanisa lisitake kwa sasa kuongea juu ya habari hizo ni hangaikio lao la hivi majuzi la kutaka kupata uthibitisho halisi wa “kisayansi.” René Laurentin, mtungaji aliye Mkatoliki Mfaransa kuhusu mambo haya, hata asema kwamba mizuka kama ile iliyotukia Lourdes ingekuwa vigumu sana kutambuliwa rasmi leo. Lakini je! ishara—ikiwa kweli zimethibitishwa kuwa zimetoka kwa Mungu—hazipasi kukubaliwa kuwa za kweli wakati wowote katika historia?

Mizuka Iliyo ya Ki-Siku-Hizi Zaidi

Mizuka ingali inatukia. Kule San Damiano, Italia, umati wa mahujaji husongamana kwenye mahali ambapo Mamma Rosa (aliyekufa katika 1981) alidai alikuwa ameona “yule Bikira.” Kanisa labaki bila kusema lolote kuhusu habari hiyo, lakini baadhi ya waaminifu watumainia kwamba kutakuwako badiliko la mtazamo wa mambo baada ya uongofu wa watu ambao wasemwa ulitukia huko.

Katika kile kijiji kidogo cha Medjugorje, Yugoslavia, hivi majuzi watoto na vijana-matineja waliripoti mizuka zaidi ya elfu moja ya yule “Bikira.” Hapa tena, ijapokuwa Kanisa latumia uangalifu mwingi, vikundi fulani hupigania kwamba ajabu hizo zitambuliwe rasmi. Hata hivyo, Wakatoliki hata wangeweza kushangaa ni mtazamo gani wapaswao kufuata wanapongoja uamuzi wa wenye mamlaka kidini. Je! kwa sasa yawapasa waamini shuhuda hizo?

Kwa kumalizia, pia kuna mizuka iliyokataliwa na Kanisa, kama ile ya kule Palmar de Troya, Hispania. Kuhusu hii iliyotajwa sasa, askofu wa Seville alionya waaminifu ‘wasilishe watu imani ya mambo yasiyo na msingi kuhusu ajabu ambazo kanisa halizitambui na hata lazilaani vikali.” Ijapokuwa onyo hilo lilitolewa, mgawanyiko bado ulitukia, ukafanya askofu mkuu mmoja na mapadri kadhaa waondoshwe katika ushirika, nao wakakaidi kanisa kwa kushikilia kwamba mizuka hiyo ilikuwa ya kweli.

Yawezekanaje kuamua kama mizuka ni ya kweli au si ya kweli? Makala inayofuata itashughulika kirefu na swali hilo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki