Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 10/8 uku. 29
  • ”Namna Iliyopotoka Zaidi ya Utumizi Mbaya wa Watoto”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ”Namna Iliyopotoka Zaidi ya Utumizi Mbaya wa Watoto”
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Madhara ya Maisha Yote
  • Wavutaji wa Pakiti Moja kwa Siku
  • Kwa Nini Uache Kuvuta Sigareti?
    Amkeni!—2000
  • Yanayompata Mvutaji wa Sigara
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Tumbako na Afya Yako—Je! Kweli Mambo Haya Yana Uhusiano?
    Amkeni!—1990
  • Unaweza Kuyavunja Mazoea ya Tumbako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 10/8 uku. 29

”Namna Iliyopotoka Zaidi ya Utumizi Mbaya wa Watoto”

Mikono ya mwanamke huyo yazungukia koo ya mtoto mchanga kwa kuikaba. Halafu afinya—akimnyonga mtoto polepole. Kitoto kichanga hicho kisicho na kinga chatapa-tapa. Katika muda ufaao mwanamke huyo alegeza fumbato lake. Kitoto chatweta kuvuta hewa lakini chaokoka shambulio hilo. Muda si muda, mwanamke huyo akaba tena ile koo ndogo sana, akianza tena ule utesaji. Aachilia tena fumbato lake na kukiacha kitoto kichanga kikitweta-tweta kuvuta hewa . . .

ULILOSOMA sasa hivi laeleza mteseko kama ule ambao humpata mtoto ambaye hajazaliwa wakati atumiwapo vibaya na mama yake mvutaji.

Madhara ya Maisha Yote

Je! hiyo ni taarifa yenye mkazo mno? Sivyo kamwe. Makala moja ya New York Times yaripoti kwamba uchunguzi unaoongezeka wa kisayansi huonyesha kwamba mama avutaye kwa ukawaida huenda akaleta kasoro za kimwili na kiakili za maisha yote juu ya mtoto wake. Makala hiyo yasema kwamba baadhi ya majeraha hayo “huonekana mara ile ile hali mengine husitawi polepole zaidi.”

Kwa njia gani uvutaji wa mama huathiri mtoto asiyezaliwa? Dakt. William G. Cahan, mpasuaji mwenye kuhudumu kwenye Kitovu cha Kansa cha Ukumbusho wa Sloan-Kettering katika United States aliye mwandikaji wa ile makala ya Times, aeleza hivi: “Katika muda wa dakika kadhaa kila mvuto wa sigareti huingiza kaboni monoksaidi na nikotini ndani ya damu ya mama.” Kwa kuwa kaboni monoksaidi hiyo hupunguza uwezo wa damu wa kuchukua oksijeni na ile nikotini hufanya mishipa ya damu ifinyane katika plasenta (kondo la nyuma), “mtoto asiyezaliwa hunyimwa kwa muda kiasi chake cha kawaida cha oksijeni. Mnyimo huo ukirudiwa mara nyingi sana,” asema mpasuaji Cahan, “ungeweza kuwa na madhara yasiyotengenezeka kwa ubongo wa kijusi, ambao ni kiungo kisicho na kifani kwa urahisi wa kupata madhara wakati kikosapo oksijeni.”

Mathalani, uchunguzi mmoja ulifunua kwamba dakika tano baada ya wanawake wenye mimba kuvuta sigareti mbili tu, vijusi vyao vilionyesha ishara za kusononeka—ongezeko la mipigo ya moyo likiandamana na misogeo-sogeo iliyo kama upumuaji usio wa kawaida.

Wavutaji wa Pakiti Moja kwa Siku

Basi, yamaanisha nini kwa mtoto ambaye hajazaliwa ikiwa mama yake huvuta sigareti 20, au pakiti moja, kwa siku? Dakt. Cahan aona kwamba mvutaji wa wastani huvuta ndani mivuto mitano kwa kila sigareti. Hivyo, zoea la kuvuta pakiti moja kwa siku hujumlika kuwa mivuto mia moja kwa siku. Kwa kuwa mimba huendelea kwa karibu siku 270, mama hukipasha kijusi “angalau vitendo 27,000 vya kukifanyia kijusi ujeuri wa kemikali mwilini.”

Huenda hao watoto wadogo wenye kutumiwa vibaya wakalipa bei ya maisha yote kwa zoea la kuvuta tumbako la mama zao. Zaidi ya matatizo ya kimwili, asema Dakt. Cahan, huenda watoto hao wakawa na “matatizo ya kitabia, kasoro za uwezo wa kusoma, utendaji mwingi kupita kiasi na kukawia kwa ukuzi wa kiakili.” Haishangazi kwamba yeye auliza hivi: “Ni mwanamke gani mwenye kujali daraka lake awezaye kusisitiza kufuata zoea linalotisha wachanga kwa kadiri hiyo?”

Kwa kuongezea, wazazi wanaovuta ni tisho pia kwa watoto wanaokua. Kwa nini? Kijitabu Facts and Figures on Smoking, kilichochapishwa na Sosaiti ya Kansa ya Amerika, chajibu hivi: “Watoto wa wavutaji wana magonjwa zaidi ya upumuaji kuliko wa wasio wavutaji, kutia na ongezeko la kutokea-tokea kwa mchochota wa mirija ya hewa na mchochota wa pafu mapema maishani.”

Kwa hiyo Dakt. Cahan akata shauri kwamba “namna hii ya utumizi mbaya wa watoto huenda ikawa ndiyo iliyoenea zaidi ya zote.” Swali ni kwamba, Je! wewe huiepuka?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki