Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 11/8 uku. 31
  • “Imara Kama Mwamba wa Gibraltar”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Imara Kama Mwamba wa Gibraltar”
  • Amkeni!—1990
  • Habari Zinazolingana
  • “Kushinda Mwelekeo wa Kuwa na Ubinafsi”
    Amkeni!—2010
  • “Uthibitisho wa Roho ya Ushirikiano”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Nyani Walifikaje Gibraltar?
    Amkeni!—2008
  • “Kwa Kuwa Tuna Huduma Hii . . . , Hatuachi”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 11/8 uku. 31

“Imara Kama Mwamba wa Gibraltar”

Kwa kuinuka ukiwa wima sana kutoka kwenye maji ya samawati yenye joto ya Mediterania na kufikia kimo cha meta 424, hakika mwamba wa Gibraltar huonekana imara. Katika siku isiyo na mawingu, mtu akiwa kilometa nyingi pande zote kusini mwa Hispania na akiwa Morocco, hadi kule ng’ambo Mediterania, aweza kuona kwa urahisi kileleta cha Gibraltar.

Historia ya Gibraltar yarudi nyuma kwenye vile vipindi vyenye ukungu wa kukosa maarifa ambapo mabaharia wa kale, kwa kuamini kwamba dunia ilikuwa tambarare, walifikiri kwamba kupita katika Mlangobahari wa Gibraltar kungewaongoza kwenye ukingo wa ulimwengu na shimo lisilo na mwisho la uharibifu. Pia ulionwa kuwa mmoja wa Nguzo za Hercules, ile nyingine ikiwa Jebel Musa kule Ceuta, katika pwani ya Afrika ng’ambo ya mlangobahari huo. Hadithi ya ubuni ilisema kwamba yule shujaa Mgiriki Hercules alikuwa ameigawanya milima ikatengana.

Jiji la Gibraltar lipo kwa sababu ya Waarabu waliokuja kutoka Afrika Kaskazini katika karne ya nane W.K. na baadaye wakaweka msingi wa jiji hilo katika 1160. Jina Gibraltar hutokana na jina la Kiarabu Djabal-Tarik, au Mlima wa Tarik. Ṭāriq ibn Ziyād alikuwa kiongozi Mwarabu aliyemshinda mfalme wa mwisho Mgothi katika 711 W.K.

Wahispania walishinda Gibraltar katika 1462, lakini wakapokonywa na Waingereza katika 1704. Hadi leo hii, ingali ni kimoja cha vituo vya nje vilivyo vya mwisho vya iliyokuwa Milki ya Uingereza. Lakini Mwamba wa Gibraltar waendelea kuwa kifananisho cha kitu imara chenye kudumu.

Makundi mawili (ya Kiingereza na Kihispania) ya Mashahidi wa Yehova wapatao 120 katika Gibraltar wanawatolea Wagibraltar ahadi juu ya utawala wa Ufalme wa Mungu, ahadi ambayo ni imara hata zaidi ya Mwamba huo!—Tito 1:1, 2; Waebrania 6:17-19.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki