Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 12/8 kur. 3-4
  • Ule Mgongano wa Wakwe wa Tangu Zamani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ule Mgongano wa Wakwe wa Tangu Zamani
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wazee-Wazee Wataka Nini?
  • Kuzikubali Faida na Hasara
  • Utunzaji wa Wazee-Wazee Tatizo Lenye Kukua
    Amkeni!—1991
  • Nawezaje Kupatana na Wazazi Wangu?
    Vijana Huuliza
  • Familia ya Kikristo Huwasaidia Wazee-Wazee
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Kupata Shangwe ya Uhusiano Mchangamfu Kati ya Wakwe
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 12/8 kur. 3-4

Ule Mgongano wa Wakwe wa Tangu Zamani

“MIMI nachukizwa sana kuona uso wako!” Fujiko akamfokea mama-mkwe wake, Tomiko. Fujiko alikuwa amechoka kuamrishwa-amrishwa. Ingawa alikuwa ameweza kudumisha utulivu kwa nje, alikuwa akiishi katika udhia mkali. “Ndani yangu mwenyewe nilihisi uchungu,” asema. “Sikuwa hali yangu ya kawaida. Sikutaka tena kuishi hivyo kila siku.”

Mwanamke mzee anayeishi peke yake katika Japani ataarifu hivi: “Mwanangu na mkeye waliniacha. Sasa si lazima mimi nihangaikie wengine, nami huishi maisha yangu nitakavyo, lakini huwa nahisi upweke jua lishukapo.”

Ule mgongano wa tangu zamani kati ya mama-mkwe na binti-mkwe ni wa kila mahali. “Kwa kusikitisha,” asema Dulcie Boling, mhariri wa gazeti katika Australia, “sikuzote wanawake fulani huwaonea wivu binti-wakwe zao. . . . Huna la kufanya, isipokuwa kucheka kihoi tu na kuhimili.” Katika Mashariki, hata kuna hekaya juu ya wanawake wazee wakiachwa peke yao milimani, kitendo ambacho huchochewa na mabinti-wakwe zao.

Leo, mgongano huu umetatanika zaidi ya nyakati zote. Kulingana na takwimu, tarajio la muda wa maisha linaongezeka, familia zinakuwa ndogo zaidi, na pengo kati ya kadiri za kufa kwa wanaume na wanawake linapanuka. Tokeo limekuwa nini? Kadiri kuzidivyo kuwa na wanawake wengi waishio kufikia miaka yao ya 70 na 80, mgongano kati ya akina mama na mabinti-wakwe zao umekuwa mbio ndefu ya jasho, si ule mfyatuko mfupi wa meta 100 kama ilivyokuwa zamani.

Wazee-Wazee Wataka Nini?

Kujapokuwa na migongano hiyo, wazazi wenye umri mkubwa hutaka watunzweje iwapo wana hiari ya kuchagua? “Muda wa miongo miwili iliyopita,” wasema Jacob S. Siegel na Cynthia M. Taeuber, watafiti wa takwimu za vifo, “wanaume na wanawake pia hawana mbetuko mwingi wa kuishi pamoja na watu wengine ikiwa hawana tena mwenzi wa ndoa.” Elaine M. Brody, aliyekuwa mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kibinadamu, aongezea kwamba katika United States, “kuishi bila watu wa ukoo wa mtu ndio mpango upendelewao miongoni mwa wazee-wazee.” Mara nyingi, watoto wao huishi karibu, huzuru, na kuwatunza.

Watu wa Mashariki hupendelea jambo hilo lifanywe kwa njia nyingine. Kulingana na uchunguzi wa kimataifa uliofanywa na Shirika la Usimamizi na Uratibu katika Japani, wazee-wazee walio wengi katika Japani na Thailandi wataka kuishi pamoja na jamaa zao. Uchunguzi huo wapata kwamba asilimia 61 ya walio wazee-wazee katika Thailandi na asilimia 51 katika Japani kwa kweli hufanya hivyo.

Bila shaka, chaguo hili ni la kawaida pia katika Magharibi. Mara nyingi wazazi walio wazee sana au wasiotoka vitandani huishi pamoja na watoto wao. Katika Ufaransa ni kawaida kwa wale wenye miaka zaidi ya 75 waishio baada ya kifo cha wenzi wao wa ndoa kuishi pamoja na mmoja wa watoto wao.

Kuzikubali Faida na Hasara

Vizazi viwili au vitatu viamuapo kuishi chini ya paa moja, bila shaka kuna faida fulani. Walio wazee-wazee huhisi kuwa salama zaidi na kuwa wamepungukiwa na upweke. Kizazi cha walio wachanga chaweza kujifunza kwa ujuzi wa hao wenye umri mkubwa zaidi, na kuna manufaa za kiuchumi pia.

Kwa upande mwingine, kuishi pamoja kwaweza kuchachisha uhusiano wa kiukwe ambao tayari umekwisha tatanika. Kwa kielelezo, katika Japani ambako wazazi wenye umri mkubwa wameishi kimapokeo pamoja na mwana aliye na umri mkubwa zaidi na familia yake, mgongano kati ya akina mama na mabinti-wakwe ni wa kawaida sana.

Ukikabiliwa na hali hiyo, waweza kufanya nini? Katika kitabu chake America’s Older Population, Paul E. Zopf, Jr., profesa wa somo la ujamii kwenye Koleji ya Guilford, asema hivi: “Familia pia huchochea mgongano na fursa ya kuweza kudhibiti mgongano vizuri. Uwezo wa kudhibiti mgongano na kuhusiana kwa matokeo mazuri pamoja na washiriki wazee-wazee huenda ukawa ni ustadi ambao hufuliza kuingia katika mahusiano mengineyo.”

Hivyo basi uwe na maoni chanya juu ya jambo hili. Ukijifunza kudhibiti magongano ya kifamilia, labda utakuwa stadi zaidi kusimamia hali nyingine zenye kutatiza pia. Ukubali kuwa wito wa ushindani, nawe utakuwa mtu bora kwa kufanya hivyo. Acheni tuchunguze matatizo ya kuishi pamoja na wakwe na tuone jinsi matatizo hayo yaweza kushughulikiwa kwa mafanikio. Na hata ikiwa kwa sasa wewe hauishi chini ya mpango huo, waweza bado kunufaika kwa kufikiria kanuni zihusikazo.

[Sanduku katika ukurasa wa 4]

Wazazi Wengi Kuliko Watoto

Sasa, kwa mara ya kwanza katika historia, kulingana na mtafiti wa takwimu za vifo Samuel Preston, mume na mke wa wastani waliofunga ndoa wana wazazi wengi kuliko watoto. Suala linalokabili wengi wa waume na wake wa leo ni jinsi ya kusawazisha madaraka yao ya kutunza mafungu mawili ya wazazi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki