Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 1/8 kur. 3-5
  • Je! Maadili Yanarudi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Maadili Yanarudi?
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Ni Kurudi kwa Maadili?
  • Mazoea Ndiyo Yamebadilika—Si Maadili
  • Je! Somo la Maadili Limesomwa?
  • Naweza Kuepukaje Kupata UKIMWI?
    Amkeni!—1993
  • UKIMWI—Je! Nimo Hatarini?
    Amkeni!—1993
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 1/8 kur. 3-5

Je! Maadili Yanarudi?

NYUMBA hizo ni tupu. Ishara zasema kwamba ni za kukodishwa. Wakati mmoja nyumba hizo katika Hamburg, Ujeremani, zilikuwa kimoja cha vitovu vikubwa zaidi vya umalaya ulimwenguni. Kwa nini zilifungwa?

Ni kwa sababu ile ile iliyofanya mahali mbalimbali maarufu pa mikutano ya wagoni-jinsia-moja wa San Francisco pawe patupu. Kotekote katika United States, klabu nyingi na mabafu-stimu ya wagoni-jinsia-moja yalifungwa moja baada ya jingine.

Ni nini hasa kilichosababisha mabadiliko haya? Ni mweneo wa UKIMWI, ile vairasi hatari ambayo imekuwa moja ya tauni mbaya zaidi za karne ya 20.

UKIMWI tayari umechukua uhai wa makumi kwa maelfu. Na ikiwa makadirio ya sasa ni sahihi, hivi karibuni ungeweza kuchukua uhai wa mamilioni mengine zaidi.

Je! Ni Kurudi kwa Maadili?

Katika miaka ya 1960 na ya ’70, mabadiliko makubwa ya kingono yalikumba nchi nyingi za Magharibi. Mapenzi ya kihiari yalikubalika mahali pengi. Hesabu ya visa vya kuzaa nje ya ndoa iliongezeka. Umri wa wenye kufanya ngono kwa mara ya kwanza ulishuka sana. Thamani za kidesturi zilibomolewa katika maisha za mamilioni, na hesabu yao ilikuwa ikiongezeka haraka sana.

Likisema juu ya roho iliyokuwapo wakati huo, gazeti la Kanada L’Actualité lilijulisha rasmi hivi: “Kile kitendo cha ngono kikawa kama mchezo wa aina fulani isiyoudhi.” Wakati uo huo, kulipoinuka harakati zenye kupigania “haki” za wagoni-jinsia-moja, ugoni-jinsia-moja ulipata kuwa suala kuu, na mabadiliko yalifanywa katika sheria ambazo hapo kwanza zilikuwa zimepiga marufuku mahusiano ya ugoni-jinsia-moja.

Ndipo UKIMWI ukatokea katika mandhari ya ulimwengu. Vifo vilipozidi kutokana na tauni hii ya ki-siku-hizi na tiba isipatikane, mtazamo wa watu kuelekea ngono ulibadilika sana. Kama lilivyoeleza L’Actualité: “UKIMWI ulipotokea, michezo ya mapenzi imekuwa hatari kabisa.” Mwanajarida Mwamerika Ellen Goodman alieleza juu ya badiliko la mtazamo ambalo lilidokezwa na jambo hilo: “Wakati ambapo—si iwapo bali wakati ambapo—UKIMWI waenea katika idadi ya watu, itakuwa kawaida zaidi kutoa jibu la ‘hapana’ kwa ngono.”

Mazoea Ndiyo Yamebadilika—Si Maadili

Je! hii yamaanisha kwamba tunashuhudia aina fulani ya mgutuko wenye kurudisha maadili? Je! huko ni “kurudi kwa maoni ya kuhifadhi mila nzuri za kale” au “tabia za utakato,” kama vile vyombo vya habari vimedai nyakati fulani?

Mazoea fulani yamebadilika kwa sababu ya uhitaji tu, lakini fikira za msingi hazikubadilika. Kwa kielelezo, wagoni-jinsia-moja ambao wameacha kufanya ngono na wenzi wengi na wakajiwekea mipaka kuwa na mwungano “wa mwenzi mmoja” hawawezi kusemwa kuwa wanarudia maadili. Zaidi ya hilo, ingekuwaje kama chanjo ya UKIMWI ingevumbuliwa? Kuna sababu ya kuamini kwamba wengi wangerudia mazoea yao ya zamani na kwamba makao maalumu yangefunguliwa yaanze kazi tena.

Katika ulimwengu wa ngono za jinsia tofauti, mabadiliko katika mwenendo, lakini si katika fikira za msingi, yaweza kuonwa pia. Felice, mwanafunzi kwenye Chuo Kikuu cha Kalifornia katika Los Angeles, U.S.A., asikitika kwamba hakuupata uhuru wa ngono uliokuwako sana katika chuo kikuu. Alisema hivi: “Kidogo ni jambo lenye kuamsha kasirani. . . . Hakika mimi naona ni laiti ningalikuwa na uhuru wa kufanya maamuzi yangu mwenyewe.” Na mwanajarida mmoja Mwamerika alieleza kwamba viwango vya kiadili vya hapo kwanza havitatokea tena, akisema hivi: “Ingawa huenda yale mabadiliko makubwa ya kingono yakawa yakipungua, hakuna mrudio wa ujumla kwenye ule uakili wa miaka ya 1940 na ya ’50 juu ya kufunga ndoa kabla ya kulala pamoja.”

Kwa kielelezo, katika Kanada gazeti Maclean’s liliripoti yanayofuata kuhusu uchunguzi wa wanafunzi wa koleji uliochangiwa fedha na serikali: “Watu wazima walio vijana huwa na habari za kutosha juu ya magonjwa yaambukizwayo kupitia ngono, kutia na UKIMWI, kaswende na kisonono. Lakini kwa wazi maarifa hayo yameshindwa kuwafanya wawe na nadhari zaidi. Walio wengi wa wanafunzi waliochunguzwa maoni walisema kwamba wao hufanya ngono, lakini walikiri kwamba ni wazembe juu ya kuchukua ile tahadhari moja ya wakati wa kufanya ngono ambayo husaidia kuzuia ugonjwa: kutumia mpira.”

Ripoti hiyo ilisema hivi pia: “Wanamamlaka wengi wa afya wasema wanahangaishwa na jambo la kwamba, kujapokuwa na utangazaji mwingi juu ya ngono salama, ujumbe huo hauathiri kile kisehemu cha watu walio watendaji wa ngono.” Dakt. Noni MacDonald, mtaalamu wa Ottawa kuhusiana na magonjwa yenye kuambukiza, alisema hivi: “Kampeni zilizo nyingi za kuelimisha na kujulisha mambo kupitia vyombo vya habari ili kuwe na ongezeko la kutumia mpira zimekuwa hoi kabisa.”

Maclean’s liliongezea hivi: “Uchunguzi katika vyuo vikuu 54 ulipata kwamba robo tatu za wanafunzi walikuwa tayari wamefanya ngono. Karibu nusu ya wanaume walidai kwamba walikuwa wamekuwa na wenzi watano au zaidi, robo moja wakidai walikuwa na jumla ya 10 au zaidi. Miongoni mwa wanawake wa koleji walioombwa maoni, asilimia 30 walisema walikuwa wamefanya ngono na angalau wenzi watano; asilimia 12 walidai walifanya hivyo na angalau wanaume 10. Hata hivyo, mipira haikupendwa na wengi. . . . Wale walio katika hatari zaidi hawakuelekea sana kutumia mipira.”

Je! Somo la Maadili Limesomwa?

Wengi hukataa kujifunza somo la maadili kutokana na linalotukia. Madaktari fulani huagiza kuwe na badiliko la mazoea, wakipendekeza kuwa na mwenzi mmoja tu wa ngono na kutumia mipira ili kuepuka UKIMWI. Lakini wao huepuka kulaani vikali mwenendo mlegevu. Alan Dershowitz, profesa wa sheria kule Harvard, ni kiwakilishi cha elekeo hili wakati adokezapo kwamba watafiti hawapaswi kutilia shaka upande wa maadili wa mwenendo wa ngono ambao huambukiza UKIMWI. Alitaarifu hivi: “Wanasayansi wapaswa kutenda kana kwamba ugonjwa huo huambukizwa kwa mwenendo wa kutogusana.”

Hata hivyo, gazeti la habari la Kifaransa Le spectacle du monde lahisi kwamba hiyo haitoshi. Lilisema hivi: “Hakuna sera yoyote ya kupambana dhidi ya UKIMWI itakayokuwa na matokeo yoyote isipoandamana na mrudio wa haraka sana, wa tufe lote, na wa hiari ya kufuata namna bora ya maadili. (Haipasi kusahauliwa kwamba uendekevu wa ngono, umalaya, na uzoelevu wa dawa za kulevya ni vigezo vikuu vya mwenendo wa kijamii uletao mweneo wa ugonjwa huu.) Huku kurudia maadili kungeweza kufanyika ikiwa tu mazingira ya utamaduni mpya yataibuka. . . . Maadili hayaletwi kwa kushikilia mawazo ya namna fulani tu. Kwa kukabiliwa na tisho la UKIMWI, ni lazima yafasiriwe kuwa uhitaji mkubwa kwa maisha ambao ndio tegemeo la kuhifadhiwa hai kwa jamii ya kibinadamu.”

Je! maadili yapasa kurudishwa yakiwa “uhitaji mkubwa kwa maisha”? Je! kufuata mfumo wa thamani za kiadili kwapasa kuamuliwe na hali tu? Je! sheria zote za tabia zina thamani ile ile? Acheni tuone ni masomo gani ambayo historia yaweza kutufundisha.

[Blabu katika ukurasa wa 5]

“HAKUNA MRUDIO WA UJUMLA KWENYE ULE UAKILI WA MIAKA YA 1940 NA ’50”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki