Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 5/8 kur. 22-24
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • UKIMWI—Je! Nimo Hatarini?
    Amkeni!—1993
  • UKIMWI— Lile Wazazi na Watoto Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—1992
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • UKIMWI—Matokeo Yenye Msiba Mkubwa kwa Watoto
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 5/8 kur. 22-24

UKIMWI— Shida kwa Matineja

UGONJWA wenye kuenea wa UKIMWI haujui umri au kizazi. Ripoti za ulimwenguni pote zatoa uthibitisho wenye kuhuzunisha kwamba “UKIMWI Unasambaa miongoni mwa Matineja, Mwelekeo Mpya Unaowagutusha wataalamu,” kama ilivyotangazwa katika kichwa cha makala ya New York Times juu ya UKIMWI. Mweneo wa ambukizo la UKIMWI miongoni mwa matineja ndio shida kubwa itakayofuata,” akasema Dakt. Gary R.  Strokash, mkurugenzi wa dawa za wabalehe kwenye kituo maarufu cha kitiba Chicago. “Ni wenye kuogofya na utakuwa wenye uharibifu,” akasema. “Hakuna shaka,” akaomboleza Dakt. Charles Wibbelsman, mkuu wa kliniki ya matineja katika kituo cha kitiba cha Kaiser Permanente katika San Francisco, “mweneo wa ugonjwa wa UKIMWI katika miaka ya 1990, ikiwa hakuna dawa yoyote, utakuwa miongoni mwa . . . matineja.” Akisema juu ya matineja waambukizwa UKIMWI, maoni ya mwelimishaji mashuhuri wa habari za UKIMWI wa New York City yalikuwa haya: “Tunafikiri kuwa ni shida ya hali ya dharura.”

The Toronto Star la Kanada, lilikuwa na kichwa kikuu cha habari kikionyesha tazamio baya kwa kadiri UKIMWI unavyoenea miongoni mwa matineja. “Kwa sasa, mambo ni mabaya sana kuliko anavyoweza mtu kutambua,” akasema daktari mmoja. “Nafikiri ni tatizo ambalo hatuliwezi. Tutaona jinsi lilivyo baya mwishowe.” Usemi huo sahili wa daktari unakuwa maoni ya maofisa wote wa afya na viongozi wa serikali kwa Ujumla kuzunguka ulimwengu kadiri pigo la UKIMWI linavyoongezeka.

Hadi hivi majuzi, wataalamu wa UKIMWI hawakukaza fikira juu ya wabalehe kuwa wamo katika hatari kubwa ya kuambukizwa HIV (vairasi inayopunguza kinga ya mwili wa kibinadamu), ambayo huleta UKIMWI. “Tunazungumzia jambo ambalo mwaka mmoja tu uliopita lilikuwa la kuwazia tu,” akasema daktari mmoja wa New York City. Hata hivyo, “Madaktari ambao mwaka mmoja tu uliopita [sasa ni miwili iliyopita] hawakuwa na mgonjwa tineja hata mmoja aliyeambukizwa, sasa wana dazani au zaidi,” likaripoti gazeti The New York Times.

Wachunguzi wanahisi kwamba ingawa habari ya kutosha juu ya matineja wenye kuambukizwa vairasi ya UKIMWI Ni yenye kugutusha, hiyo ni dalili ndogo sana ya jinsi mambo yalivyo hasa, kwa vile dalili za ugonjwa kwa kawaida hazionekani mpaka wastani wa kuanzia miaka saba hadi kumi baada ya ambukizo. Kwa hiyo wale wenye kuambukizwa HIV katika utineja wa mapema huenda wasitokeze dalili zilizokomaa za UKIMWI hadi miaka ya mwisho ya utineja wao au miaka yao ya mapema ya 20.

Kwa mfano, katika uchunguzi wa karibuni wa wazaliwa wote katika jimbo tangu 1987, Idara ya Afya ya Jimbo la New York iliripoti kwamba 1 kati ya 1,000 waliozaliwa na vijana wenye umri wa miaka 15 walikuwa na vijasumu kwa vairasi ya UKIMWI, ikionyesha kwamba mama ya mtoto alikuwa ameambukizwa. Kwa kugutusha, uchunguzi uo huo ulifunua kwamba 1 kati ya 100 waliozaliwa kutokana na vijana wenye umri wa miaka 19 walikuwa na vijisumu kwa vairasi ya UKIMWI. Uchunguzi zaidi wa CDC (Vitovu vya Kudhibiti maradhi vya U.S.) ulionyesha kwamba asilimia 20 ya wanaume Waamerika na asilimia 25 ya wanawake Waamerika waliopimwa kuwa na UKIMWI wako kwenye miaka yao ya 20. Uchunguzi wa CDC waripoti kwamba katika hali nyingi za visa hivyo, waliambukizwa ugonjwa wakati ubalehe.

Hili lawezekanaje, hata hivyo, hali watoto wanaozaliwa na vairasi ya UKIMWI ni mara chache, au wakiwapo, wao huishi hata kuwa matineja? Sababu zinashtua!

Wachunguzi na madaktari wanaonyesha kwamba matineja wa leo ni “watendaji wa ngono sana, kama vile wingi wa magonjwa ya kuambukizwa kingono unavyoonyesha,” likaripoti The New York Times. Kituo cha Hiari za watu charipoti kwamba kila mwaka 1 kati ya matineja 6 hupata ugonjwa fulani wenye kuambukizwa kingono na kwamba 1 kati ya kila wasichana 6 wa shule za sekondari walio watendaji wa ngono amekuwa na angalau wenzi wanne tofauti-tofauti.

“Kujapokuwa sihi za ‘kataa kabisa,’ tineja wa kawaida Mwamerika hupoteza ubikira katika umri wa miaka 16,” likaripoti News & World Report. “Kwa vile ni matineja wachache hupimwa kujaribiwa ugonjwa, wengi wa wale walioambukizwa hawajui wanabeba vairasi HIV,” gazeti likasema. Kuwe au kusiwe kufanya ngono za ovyoovyo ambako hushirikishwa na utumizi wa dawa ya kulevya ya kokeni, wawe ni watoro au sivyo, “matineja Waamerika ni shabaha za UKIMWI,” akaandika mtaalamu mmoja juu ya UKIMWI. “Tayari wanaona visa vya magonjwa ya kuambukizwa kingono milioni 2.5 kila mwaka.” Dakt. Gary Noble wa CDC alitoa maoni haya: “Tunajua mwenendo wao wa ngono unatokeza hatari kubwa ya ambukizo.”

Kuongezea hesabu inayokua haraka ya njia za kusambaa kwa vairasi ya UKIMWI ni wabalehe, wengine ambao bado hawajafikia miaka yao ya utineja, wengi wakiwa watoro kutoka wazazi wenye kuumiza watoto. Miongoni mwao kumekuwa na ongezeko kubwa katika hesabu ya wale ambao wamegeukia matumizi ya dawa ya kulevya ya kokeni. Wengi wamegeukia ukahaba ili kutegemeza tabia yao au kupata mahali pa kulala. Katika Amerika Kusini, kwa mfano, “ Wasichana wachanga wa miaka tisa na 10 hufanya kazi ya kuwa makahaba, wakati mwingine ili wapate sahani moja tu ya chakula,” akasema mshauri wa watoto wa Brazili. “Wengi wanajua machache tu kuhusu UKIMWI au ngono. Nimepata wasichana ambao walikuwa na mimba na wakafikiria ‘waliambukizwa,’ kama homa,” akasema.

Dakt. Philip Pizzo, mtaalamu wa UKIMWI na mkuu wa matibabu ya magonjwa ya watoto katika Taasisi ya Kitaifa ya Kansa, alisema kwamba kadiri ya ambukizo la vairasi HIV katika matineja watoro ni dalili mbaya kwa mweneo wa kikumbo cha UKIMWI. “Kuna watoro zaidi ya milioni moja wanaojipatia riziki yao kupitia ngono. Bila shaka, wengine watarudishwa wawe tena sehemu ya jamii.”

Je! basi ni ajabu kwamba ugonjwa wa UKIMWI unaongezeka mbiombio miongoni mwa matineja ulimwenguni pote? Je! hauwezi kukomeshwa? Itakuwa hivyo maadamu kutojali na kupuuza mambo kutaendelea kudhihirishwa na wale walioambukizwa vairasi ya UKIMWI na wale wasioweza kusema la kwa ngono kabla ya ndoa. Fikiria, kwa mfano, ripoti hii kutoka The Sunday Star la Johannesburg, Afrika Kusini. Katika uchunguzi wa karibuni uliofanywa miongoni mwa wagonjwa 1,142 wenye ugonjwa wa kuambukizwa kingono, asilimia 70 walikubali kuwa na wenzi wa ngono kuanzia 3 hadi 80 kwa mwezi. Wengine wangali watendaji ngono na wenye kuambukiza wengine.

Kwa kusikitisha, matineja wengi hawahangaishwi sana na UKIMWI. Kwao kila siku ni ya kupigania njia za uokokaji—njia tele za kufa barabarani—hivi kwamba hawawezi kukaza fikira juu ya kitu ambacho kingeweza kuwauwa miaka mingi kuanzia sasa. Kwa sasa, wao wanaona kwamba hakika matibabu yatapatikana ili kuwaokoa. “Wabalehe ni mfano wa kwanza wa kikundi ambacho hakiangalii miaka 10 ijayo,” akasema mtaalamu mmoja wa UKIMWI.

Pia kuna dhanio la wasiwasi baya la siri miongoni mwa wengi kwamba wenzi wao wa ngono hawawadanganyi wanaposema hawana vairasi ya UKIMWI. Mara nyingi hiyo si kweli. Hata katika hatua za kuendelea za ugonjwa huo, wengi huambukiza wengine kwa kupenda kwa sababu ya hasira au kulipiza kisasi.

Wasio wa kusahauliwa ni wale wanaoambukizwa na vairasi hiyo kupitia sindano zinazotumiwa kwa dawa za kulevya—njia ambayo tayari imeua wengi. Na, hatimaye, kuna lile tisho la daima la kupata UKIMWI kupitia kutiwa damu mishipani. Watu wengi wasio na hatia tayari wamekufa kutokana na ugonjwa huo, na wengine bado watakufa kutokana na damu iliyochafuliwa na vairasi HIV. Madaktari wengi na wauguzi wa kike wanaogopa kujidunga na sindano ambazo zimechafuliwa na vairasi ya UKIMWI, jambo ambalo laweza kugeuza maisha zao kabisa kabisa. Je! ni ajabu kwamba UKIMWI unasemekana kuwa shida kubwa ya miaka ya 1990 na kuendelea?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki