Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 2/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • SHERIA MPYA YA DAMU
  • JE! WAUGUZI WANA HAKI YA KUCHAGUA?
  • ULIMWENGU WOTE MZIMA ULIO MGUMU KUELEWEKA
  • “UDHOOFU WA
  • UKIMWI KATIKA INDIA
  • RELI ZA CHINI YA ARDHI ZENYE UBAGUZI
  • MASKINI WA MASKINI WOTE
  • KILEO NA WANAWAKE
  • TATIZO LA KUNYWA
  • JAMBO BAYA KULIKO UNENE WA KUPITA KIASI
  • UGONJWA WA KARNE YA 20
  • Utiaji-damu Mishipani—Ni Salama Kadiri Gani?
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
  • Zawadi ya Uhai au Busu la Kifo?
    Amkeni!—1991
  • Jinsi Madaktari Hukabiliana na UKIMWI
    Amkeni!—1992
  • “Masuala ya Kisheria Katika Tiba ya Kutia Damu Mishipani”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 2/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

SHERIA MPYA YA DAMU

Katika Januari 1, 1990, Kalifornia ilipata kuwa mkoa wa kwanza katika United States kufikiliza sheria inayotaka matabibu na wapasuaji wawapashe habari wagonjwa wao juu ya hatari za kutiwa damu mishipani “wakati wowote kunapokuwa na uwezekano wa kwamba kutiwa damu mishipani huenda kukahitajiwa kabisa kutokana na hatua ya upasuaji.” Kulingana na sheria mpya hiyo, mgonjwa anapasa pia kuambiwa kwa barua juu ya hatari na pia faida za njia nyingine mbalimbali zilizo badala ya kutiwa damu ya mtu mwingine. Wapasuaji na matabibu ni lazima waandike katika rekodi ya kitiba ya mgonjwa kwamba mgonjwa alipashwa habari hivyo. Ingawa hivyo, hatua hizi hazitumiki kukiwa na ile inayosemwa kuwa “dharura yenye kutisha uhai.” Ikiitwa Kifungu cha Paul Gann cha Usalama wa Damu, hatua hii imepewa jina la mpiganiaji maarufu wa marekebisho ya kodi aliyekufa kutokana na UKIMWI alioupata kutokana na kutiwa damu mishipani. Kulingana na maandishi ya ujulisho wa kifo chake yaliyochapwa katika gazeti Time, “Gann aliamini kwamba watu wanaoambukiza [UKIMWI] kwa kujua ‘wanapaswa kufanyiwa kesi ya kuua kimakusudi.’”

JE! WAUGUZI WANA HAKI YA KUCHAGUA?

Ingawa wanaopendelea utoaji mimba wanadai kwamba kila mwanamke anapaswa kuwa na haki ya kuchagua utoaji mimba, wauguzi wengi katika Kanada wanaona kwamba wananyimwa haki yao wenyewe ya kuamua—uhuru wa kukataa kusaidia madaktari katika visa vya utoaji mimba. Kulingana na The Globe and Mail la Toronto, Kanada, wauguzi wengi katika nchi hiyo wanaambiwa watie sahihi taarifa zinazojulisha rasmi kwamba imani zao za kidini na za kibinafsi hazitawazuia wasiendeshe wajibu wowote ambao huenda wakagawiwa. Wakikataa kusaidia katika visa vya utoaji mimba, “wanapaswa kutafuta kazi nyingine,” kulingana na msemaji mmoja kwa ajili ya Shirika la Hospitali ya Ontario. Nchi nyinginezo zinaruhusu mambo fulani kwa ajili ya dhamiri ya mwuguzi. Koleji Royal ya Uuguzi Uingereza hata inadokeza ushauri wenye kuendelea kwa ajili ya wauguzi wanaosaidia katika visa vya utoaji mimba, kwa kuwa huenda wauguzi wakaamua kuacha zoea hilo baada ya kujionea visa vya utoaji mimba.

ULIMWENGU WOTE MZIMA ULIO MGUMU KUELEWEKA

Kugunduliwa kwa maumbo makubwa sana katika anga za juu huenda kukalazimisha wanasayansi kukadiria upya nadharia zao. Umbo moja la jinsi hiyo, linalotajwa kuwa “ule ukuta mkubwa,” linaelezwa kuwa utandao mkubwa sana wa tambarare ulio na magalaksi yenye kuenea nje umbali wa milioni elfu moja ya miaka-nuru. Umbo jingine linatajwa kuwa “kile kivutiaji kikubwa” kwa sababu linavuta magalaksi mengi, kutia na letu wenyewe, yalielekee hilo lenyewe. The New York Times linasema kwamba maumbo hayo, ambayo “si magalaksi tu au mafungu yayo, bali ni ‘kontinenti za magalaksi’” zilizo kubwa sana, yanahakikisha nadharia za kwamba “vitu vilivyo vya msingi katika ulimwengu wote mzima ni vikubwa na vigumu kueleweka kuliko vile wanaanga walivyokuwa wamewazia.” Mfizikia-anga mmoja aliambia gazeti Times kwamba watunga nadharia wengi walikuwa wakitumaini kwamba kile kivutiaji kikubwa kingeenda mbali. Kwa nini? “Sisi tunashindwa kabisa kuelewa umbo kubwa jinsi hiyo linaweza kufanyizwaje,” akasema.

“UDHOOFU WA

MAISHA YA KIDINI”

Je! dini ni ya maana kwa watu wa Italia? Si kulingana na uchunguzi mmoja wa hivi majuzi kwa Waitalia 2,008 wa kuanzia umri wa miaka 14 kufika 70. Kati ya wale waliohojiwa, asilimia 61.5 walisema hawakusali kamwe au walisali kidogo sana. Ni asilimia 0.5 tu waliokuwa wakiendea padri kwa ushauri. Asilimia 8 tu iliyo kidogo sana ndio walioona kwamba imani inahitajiwa ili kuendeleza mahusiano ya kibinadamu. Kulingana na gazeti la Kiitalia Il Corriere della Sera, “asilimia 45 [ya watu Waitalia] wanadai ni waamini, lakini hawana uhakika ni [waamini] katika kitu gani.” Na Il Giornale linasema kwamba imani ambazo Waitalia wanazo ni kama tu “ukubali mlegevu wa mambo yaliyopita badala ya kuwa chaguo lenye kufanywa kwa kujitakia.” La Stampa lilieleza hali hiyo kuwa “udhoofu wa maisha ya kidini” katika Italia. Ni nini kimechukua mahali pa zile dini zenye kugawanyikana? Il Corriere della Sera linajibu hivi: “Katika mahali pazo, kwa sasa, mna utupu.”

UKIMWI KATIKA INDIA

Mwanzoni mwa 1990, viliripotiwa visa 41 tu vya UKIMWI uliokomaa katika India; hata hivyo taifa hilo huenda likawa ndilo la kwanza katika Esia kupatwa na kipuku kikubwa cha UKIMWI, kulingana na The Toronto Star. Serikali ya India inakadiria kwamba malaya kama 10,000 kati ya wale 100,000 katika Bombay tayari wana ambukizo la ile vairasi yenye hatari ya kifo. Kikundi hicho pekee huenda kikaweza kuambukiza wanaume 20,000 kwa mwaka mmoja tu. Malaya wengi wanakataa kuacha biashara yao hata baada ya kujua kwamba wana ambukizo, wakidai kwamba hawana njia nyingine ya kupata riziki. Mamia ya wenye kawaida ya kuuza damu katika India pia wana ile vairasi ya UKIMWI; hata hivyo wengi wanaendelea kuuza damu yao ili kupata riziki. Wakati vairasi hiyo inapoenea sehemu zote za nchi, ofisa mmoja wa tiba katika Bombay anatoa muhtasari wa hali katika jiji hilo: “Hili ni kombora linaloendelea kuhesabu wakati likisonga mbele likafyatuke.”

RELI ZA CHINI YA ARDHI ZENYE UBAGUZI

Ule mfumo mpya wa reli za chini ya ardhi katika Cairo, Misri, umesifiwa mahali pengi kwa usafi, utendaji mzuri, na usalama wao. Hata hivyo, wanawake wa Cairo wameomba ufanyiwe maendeleo. Behewa moja la kila gari-moshi limewekwa kando kwa ajili ya abiria wa kike tu. Mwongozo mpya huo uliungwa mkono na Thuraya Labna, mshiriki mtetezi wa haki za kike wa bunge la Misri, aliyedai kwamba wanawake Wamisri walihitaji njia salama ya kutumia usafiri wa umma bila kufanyiwa usumbuaji wa kingono ulioenea sana katika Cairo. Ingawa mpango huo umetokeza uchambuzi fulani (kwa mfano, behewa la wanawake la chini ya ardhi limedhihakiwa kuwa ni ‘nyumba-magurudumu ya kuhifadhi wanawake’), unaripotiwa kuwa umepata mafanikio fulani kuelekea mradi wao wa kulinda wanawake.

MASKINI WA MASKINI WOTE

Katika Februari 1990, wawakilishi kutoka mataifa 42 yaliyo maskini zaidi ya yote ulimwenguni walikutana kwa mwisho-juma mmoja katika Bangladesh ili kufikiria njia mpya za kusadikisha mataifa ya ulimwengu yaliyo matajiri zaidi kwamba watu kama milioni 500 wamo katika uhitaji wa kusaidiwa haraka. Mkutano kama huo ulifanywa katika 1981, lakini hakuna wowote wa miradi yao mikubwa uliotimizwa. Kwa uhakika, The New York Times linaripoti kwamba “miaka ya 1980 imeleta umaskini wenye kushusha heshima zaidi, mzoroto wa kutojua kusoma, afya yenye kuwa mbaya zaidi na viwango vya maisha ambavyo kwa ujumla ni vya hali ya chini zaidi.” Wastani wa mapato kwa kila mtu katika mataifa hayo 42 ni dola 200 tu (za United States) kwa mwaka. Ishirini na nane za nchi hizo zimo katika Afrika, tisa katika Esia, nne ni mataifa ya visiwani katika bahari kuu za Pasifiki na Hindi, na moja limo katika Bahari Karibbea ya kontinenti za Amerika.

KILEO NA WANAWAKE

Kwa muda mrefu imeonwa kwamba kileo kina nguvu nyingi zaidi juu ya wanawake kuliko kilivyo juu ya wanaume. Elezo moja maarufu limekuwa kwamba wanaume wana uzito mwingi zaidi, hivyo basi wanaweza kufyonza kileo kingi zaidi. Lakini sasa wanasayansi Waitalia na Waamerika wamepata kwamba mwili wa kike unafanyiza kiasi kipungufu kwa asilimia 30 cha kimeng’enya kimoja kinachoitwa kiyeyusha-kileo kuliko vile mwili wa kiume unavyofanya. Kileo kikiwa kingali tumboni, kimeng’enya hicho kinavunja kiasi fulani cha kileo hicho kabla hakijaweza kuingia katika mkondo wa damu na kusafiri kwenye ubongo, ini, na viungo vingine. Wanaume wanywaji vileo wanaendelea kufanyiza karibu nusu ya kiasi chao cha kawaida cha kimeng’enya hicho, hali wanawake wanywaji vileo ni kama hawafanyizi chochote.

TATIZO LA KUNYWA

“Kuweka maji ya kunywa yakiwa safi ni tatizo katika Ulaya yote na ng’ambo yake,” linaripoti The German Tribune. Kulingana na gazeti la Kijeremani Deutsches Allgemeines Sonntagsblatt, Shirika la Kijeremani la Mabaraza ya Gesi na Maji linakadiria kwamba kati ya vituo 6,300 vya kueneza maji katika Jamhuri ya Mwungano ya Ujeremani, kati ya asilimia 10 na 20 vinashindwa kufikia kiwango cha Ulaya kwa maji ya kunywa. Serikali inaruhusu kutumia karibu dawa 1,400 za kuua vijidudu, ambazo zina vikemikali kama 240. Kufikia hapo, dalili za vikemikali angalau 40 kati yavyo zimepatikana katika maji ya kunywa ya nchi hiyo, maji yayo ya chini ya ardhi, na hata, kwa kadiri yenye kuongezeka, katika maji yayo ya mvua. Zaidi ya hilo, maji ya kunywa ya Ujeremani yangali yakipatwa na matokeo yaliyobakia kutokana na Vita ya Ulimwengu 2. Katika mji mdogo mmoja, uliokuwa mahali pa kiwanda cha marisau hapo zamani, ilikuwa lazima visima sita vifungwe; vilichafuliwa na mabaki ya utokezaji wa TNT.

JAMBO BAYA KULIKO UNENE WA KUPITA KIASI

Inajulikana sana kwamba kuacha kuvuta sigareti huenda kukachangia kuongezeka uzito wa mwili na kwamba unene wa kupita kiasi ni hatari ya afya. Lakini mambo mawili hayo hayaungi mkono fikira ya wavutaji fulani wa sigareti kwamba ni jambo la kiafya zaidi kuendelea kuvuta sigareti na kubaki mwembamba kuliko kuacha na kuongezeka uzito. Kulingana na Economist la Uingereza, mwanatakwimu mmoja na mchunguzi mmoja wa mweneo na udhibiti wa magonjwa wamechanganua tarakimu kutokana na uchunguzi mrefu kwa wanaume Waingereza zaidi ya 7,000. Wachunguzi hao walikata shauri kwamba ingawa kwa kweli ni hatari kuwa mnene kupita kiasi, kuvuta sigareti 20 kwa siku ni hatari hata zaidi. Linasema hivi The Economist: “Hata unene wa kupita kiasi sana ulionwa kuwa afadhali kuliko kuvuta sigareti (si kwa sababu unene wa kupita kiasi si mbaya kamwe, bali kwa sababu kuvuta sigareti ni kubaya kweli kweli).”

UGONJWA WA KARNE YA 20

Uchafuzi wa ki-siku-hizi umezalisha ugonjwa mpya usio wa kawaida. Ukiitwa ugonjwa wa kimazingira, wepesi wa kupatwa na matokeo mabaya ya mazingira, au ugonjwa wa karne ya 20, unaripotiwa kuwa unasumbua watu kama 30,000 katika Ontario, Kanada, pekee. Wasumbukaji ni wepesi sana mno kupata madhara kutokana na kemikali na vichafuzi vingi sana vinavyofanyizwa na binadamu, kuanzia moshi wa sigareti kufikia wino iliyo katika vichapo. Katika visa vya kupita kiasi, wasumbukaji wanakuwa mahoi wasioweza kutoka nyumbani, wakipumua kupitia kivaliwa-usoni cha kuvutia oksijeni. The Toronto Star linasema kwamba wastadi fulani wanaamini kwamba usumbukaji wa wachache hawa “ni onyo kwamba kumekuwa na kasoro fulani mbaya sana.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki