Jinsi Madaktari Hukabiliana na UKIMWI
HATARI ya kupatwa na UKIMWI kupitia damu imefanya madaktari-wapasuaji waanze kutumia kile gazeti The New York Times linachokiita “deraya mpya ya upasuaji kwa enzi ya UKIMWI.” Kwa daktari-mpasuaji deraya hiyo inatia ndani “viatu vikubwa vya raba (mpira), aproni ndefu isiyoweza kupenywa na maji, glovu mbili za mikononi, vifuniko vya mikono ya vazi visivyoweza kupenywa na maji na miwani.” Na hasa kwa visa vyenye umwagikaji mwingi wa damu, lasema Times, “kofia yenye kifaa kilichoviringishwa kinachofunika uso.”
Jambo kuu ni kwamba, kuelekea mwishoni mwa 1990, kituo Federal Centers for Disease Control kilisema kwamba kati ya visa 153,000 vilivyoripotiwa vya UKIMWI, 637 walikuwa matabibu, 42 madaktari-wapasuaji, 156 madaktari wa meno na wenye kushughulikia usafi wa afya, na 1,199 walikuwa wauguzi wa kike.
UKIMWI ulitambuliwa kwa mara ya kwanza katika 1981. Kwa wakati fulani ulikuwa hasa miongoni mwa wagoni-jinsia-moja wa kiume na miongoni mwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao waliambukizwa kwa kutumia sindano chafu. Lakini mweneo wao kwa wanawake umekuwa wa haraka sana. World Health, gazeti la WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni), liliripoti katika makala yalo ya Novemba-Desemba 1990 hivi: “Hesabu ya wanawake [ulimwenguni pote] wanaotazamiwa kupatwa na ugonjwa wa UKIMWI kwa miaka miwili ijayo itapita ile jumla yote ya visa vya UKIMWI vilivyoripotiwa katika mwongo wa kwanza wa tauni hiyo.”
Kituo Federal Centers for Disease Cntrol katika United States kiliripoti kwamba kufikia mwishoni mwa 1990, kulikuwako watu 15,696 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ambao walikuwa na dalili za UKIMWI. Hiyo ni hesabu kubwa ikilinganishwa na visa 2,686 vya UKIMWI katika watoto wa umri wa chini ya miaka 13, kikundi cha wagonjwa wa UKIMWI ambacho kimepewa utangazaji mwingi zaidi.
Wenye umri mkubwa wanapataje UKIMWI? Wengi wanaupata kwa sababu ya vitendo vya ugoni-jinsia-moja. Hata hivyo, kulingana na gazeti New York Times, “karibu asilimia 17 ya wagonjwa hao waliambukizwa virasi hiyo kwa kutiwa mishipani damu yenye viini.” Hiyo ni hesabu ya visa vya UKIMWI miongoni mwa wenye umri mkubwa kwa sababu ya kutiwa damu mishipani inayokaribia kuwa sawa na jumla hesabu ya visa vya UKIMWI miongoni mwa watoto wa umri wa chini ya miaka 13!