Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 2/8 uku. 4
  • Karne za Mitengano

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Karne za Mitengano
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Mtengano Mpya
    Amkeni!—1991
  • Kwa Nini Ule “Wasiwasi Mwingi”?
    Amkeni!—1991
  • Sehemu ya 15: 1095-1453 W.K.— Kugeukia Upanga
    Amkeni!—1990
  • Kwa Nini Ile Migawanyiko?
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 2/8 uku. 4

Karne za Mitengano

NENO “mtengano” limefafanuliwa kuwa “utaratibu ambao kwao kikundi cha kidini kinagawanyika kuwa vikundi viwili au zaidi vilivyo tofauti, vyenye kujitegemea.”

330 W.K. “Mtengano kati ya Jumuiya ya Wakristo Wagiriki na Walatini. . . . Kuwekwa msingi kwa Konstantinopo, ile ‘Roma mpya’ (330), kuchukua mahali pa ile ‘Roma ya zamani’ ikiwa mji mkuu wa milki, kulipanda mbegu za ushindani wa wakati ujao kati ya maongozi ya kikanisa ya Mashariki ya Wagiriki na Magharibi ya Walatini.”—The Encyclopedia of Religion.

330-867 W.K. “Kutoka mwanzo wa Jimbo la Askofu wa Konstantinopo kufika kwenye ule mtengano mkubwa katika 867 orodha ya hii miachano ya muda ya ushirika ni mikubwa ajabu. . . . Kati ya miaka hii 544 (323-867) ni miaka isiyopungua 203 iliyotumiwa na Konstantinopo katika hali ya mtengano [pamoja na Roma kuhusiana na magombano ya kitheolojia yanayohusu Utatu na ibada ya mifano].”—The Catholic Encyclopedia.

867 W.K. “Jimbo la Askofu wa Konstantinopo lilishikilia msimamo walo wa kupinga Roma wakati wa ule ulioitwa Mtengano Kuhusu Photiu. Papa Nicholas 1 alipotoa ubishi juu ya kupandishwa cheo cha Photiu awe katika uzee wa kanisa, . . . huyo mzee wa kanisa wa kutoka Byzantine alikataa kutii. . . . Nicholas . . . alimwondosha Photius katika ushirika; baraza moja huko Konstantinopo lilijibu (867) kwa kumwondosha Nicholas naye katika ushirika. Mizozo iliyotokea mara hiyo kati ya majimbo yote mawili ya maaskofu ilihusu maongozi ya kikanisa, liturjia [kawaida rasmi ya ibada], na nidhamu ya kikasisi.”—The New Encyclopædia Britannica.

1054 W.K. “MTENGANO WA MASHARIKI NA MAGHARIBI, tukio lililoharakisha mtengano wa mwisho kati ya makanisa ya Ukristo wa Mashariki [ya Kiorthodoksi] . . . na Kanisa la Magharibi [Katoliki ya Kiroma].”—The New Encyclopædia Britannica.

1378-1417 W.K. “MTENGANO [MKUBWA] WA MAGHARIBI—Kipindi . . . ambamo Jumuiya ya Wakristo ya Magharibi iligawanyika kati ya pande mbili, na baadaye tatu, za kutii [kukiwa na mapapa washindani katika Roma, Avignon (Ufaransa), na Pisa (Italia)].”—New Catholic Encyclopedia.

Karne ya 16 W.K. “Kwa habari ya ule Mrekebisho wa Kiprotestanti, Kanisa Katoliki sana-sana linatumia neno uzushi badala ya mtengano.”—Theó—Nouvelle encyclopédie catholique.

1870 W.K. “Baraza la Kwanza la Vatikani, lililotetea ‘kutokukosa kamwe’ kwa papa, lilitokeza ule mtengano wa ‘Wakatoliki wa Zamani.’”—La Croix (gazeti la kila siku la Paris, Katoliki).

1988: Mtengano wa Askofu Mkuu Lefebvre, ambaye “alianzisha mtengano katika Kanisa Katoliki kwa kukaidi Papa na lengo la Baraza la Vatikani la pili . . . ambaye anawachukua Waprotestanti kuwa wazushi, ambaye anaona mwungamanisho wa dini zote pamoja kuwa kazi ya ibilisi, na aliye na nia ya kufa akiwa mwondoshwa ushirikani kuliko kupatanishwa na Kanisa ‘la umamboleo.’”—Catholic Herald.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki