Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 5/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MAZIWA BORA ZAIDI
  • “THAMANI BANDIA”
  • UKIMWI KATIKA CHINA
  • VIINI VYENYE KUUA
  • WAKATOLIKI NA BIBLIA
  • UZOEVU WA ALKOHOLI NA JENI
  • MAADILI YA MAKASISI
  • UNYONYESHAJI MATITI HULINDA
  • KUTEKA NYARA MAGARI
  • “HAKUNA SABABU YA KUADHIMISHA”
  • TAFSIRI MPYA ZA BIBLIA
  • BROSHUA YA BIBLIA KATIKA LUGHA 192
  • Kisasi cha Vijiumbe-Maradhi
    Amkeni!—1996
  • Kwa Nini Kanisa Linapoteza Uvutano?
    Amkeni!—1996
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1996
Amkeni!—1991
g91 5/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

MAZIWA BORA ZAIDI

Utafiti wa karibuni wa akina mama Waskochi na watoto wao waliotoka kuzaliwa waonyesha kwamba thamani ya vilishaji vya maziwa ya mama na ulinzi yanaotoa haviwezi kuigizwa na mifanyizo ya kibiashara. Uchunguzi huo uliochapishwa katika Le Figaro, gazeti moja la Ufaransa, waonyesha kwamba watoto wadogo walionyonyeshwa matiti kwa majuma 13 au zaidi kwa wazi walikuwa na maambukizo machache zaidi wakati wa mwaka wao wa kwanza wa maisha kuliko wale ambao waliacha kunyonyeshwa matiti kabisa kabla ya majuma 13 au waliopewa mifanyizo ya chupa tangu kuzaliwa. Maziwa ya mama hufaa ufanyizwaji wa aina fulani ya bakteria inayozuia ukuzi wa bakteria zenye kudhuru katika matumbo ya mtoto mdogo. Muundo wenye kutia vitu vingi wa maziwa ya mama pia hutofautiana siku kwa siku kwa kulingana na umri na mahitaji ya mtoto mchanga, hata yakiruhusu mtoto mchanga anayenyonya matiti abadilikane kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa. Le Figaro lasema: “Hayana kifani.”

“THAMANI BANDIA”

Akiwa na miaka 22, Boris Becker ni mmoja wa wachezaji tenisi wenye kuongoza ulimwengu; pia yeye ni mmoja wa walio matajiri zaidi—akiwa na mali inayokadiriwa $75 milioni (U.S.). Mali yake ilipatikana kwa kushinda mechi za tenisi. Hata hivyo, mwanariadha kijana huyo Mjerumani aamini kwamba yeye hulipwa kupita kiasi: “Ni mzaha unapofikiria hilo—kiwango ninachopata kwa ajili ya kupiga mpira wa tenisi upite juu ya wavu.” Kulingana na Parade Magazine, yeye alisema kwamba katika jumuiya ya leo “kuna fedha nyingi mno hivi kwamba hakuna mtu anayepaswa kuwa na njaa au kuwa bila makao. Watu huelekezea fikira nyingi mno thamani bandia.”

UKIMWI KATIKA CHINA

“Ni uhakika wenye kusikitisha kwamba vairasi ya UKIMWI imetokea China,” lilisema gazeti China Today. Ndiyo, bara hili kubwa limetiwa hivi karibuni kwenye orodha ndefu ya nchi zenye UKIMWI. Gazeti hilo laongeza kwamba “katika China, jitihada za kisayansi na kitiba za kuzuia UKIMWI zimeambatana na majaribio ya kukomesha lile tukio bovu la kijamii la hatua ya kwanza liwezalo kuongoza kwenye maradhi hayo—ponografia, umalaya, matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na kadhalika.” Baadhi ya waliopatwa wameambukiwa kupitia kudungwa vitu vilivyofanyizwa kwa damu. Kwa hiyo, katika jitihada ya kupunguza usambaaji wa UKIMWI, serikali ya China imekuwa ikiwekea vizuizi uingizaji nchini wa umaji-maji wa damu tangu 1984.

VIINI VYENYE KUUA

“Kinyume cha wazo lililoenea sana, numonia (kichomi) hakijapata kamwe kutoweka kisiwe kisababishi kikuu cha kifo baada ya kuanza kutumiwa kwa viua-viini. Ingali kisababishi cha kawaida cha kifo kinacholetwa na maambukizo na ni ya sita ya viuaji Waamerika vinavyoongoza,” laripoti The New York Times. Ingawa hatua kadhaa za kitiba za ki-siku-hizi, kama vile viua-viini na chanjo, zimepunguza sana visa vya maambukizo ya bakteria, hatua hizo “sikuzote haziwezi kutegemewa kuwa wokovu wa dakika ya mwisho, hasa ikiwa viini hivyo vimeimarika kwa kuenea katika mwili wote.” Times liliongeza kwamba “kati ya maradhi ya kuambukiza yanayokadiriwa kuwa 500, hakuna tiba yenye matokeo kamili kwa karibu 200.”

WAKATOLIKI NA BIBLIA

Kasisi mmoja wa parishi (tarafa) katika Sydney, Australia, amekubali waziwazi kwamba kwa kawaida Wakatoliki wana maarifa machache ya Biblia, kulingana na Daily Mirror la Sydney. Ili kusaidia kurekebisha ukosefu huo wa maarifa ya Biblia, Kanisa Katoliki limeamua kutoa mitaala juu ya Biblia katika vitovu kumi vya miji midogo katika jiji lote la Sydney. Mtaala huo uliopangwa utakuwa wa mihula minne ya majuma matano, na tumaini ni kwamba karibu 2,000 watajiandikisha. Daily Mirror lilieleza kwamba “kwa waabudu wengi hakuna kuambatana” kati ya Kanisa Katoliki na Biblia na kwa kufaa makala yalo ilikuwa na kichwa: “Kurudia Mambo ya Msingi kwa Waaminifu.”

UZOEVU WA ALKOHOLI NA JENI

Katika utafiti wa kisayansi wa hivi karibuni ulioripotiwa katika The Journal of the American Medical Association, wanasayansi wanadai wametambua jeni (chembe ya tabia) inayohatarisha watu wawe wazoevu wa alkoholi. Hata hivyo, wanasayansi watahadharisha kwamba hakuna jeni moja inayoongoza kwenye uzoevu wa alkoholi. Kiongozi wa kikundi hicho cha utafiti alisema: “Bwana aliye mwema hakufanya jeni ya kuzoea alkoholi, ila ile inayoelekea yahusika katika tabia za kutafuta anasa.” Badala yake, “watu fulani wenye jeni hiyo waliofanyiwa utafiti hawakuwa wazoevu wa alkoholi, hali wengine ambao hawakuwa na jeni hiyo walikuwa wazoevu wa alkoholi, [watafiti hao] wakasema. Hali za kijamii na kitamaduni zaweza kuanzisha shambulio kwa wazoevu alkoholi wengi ambao kwenye jeni hawaelekei kufanya [hivyo].”

MAADILI YA MAKASISI

Kulingana na The Toronto Star, dayosisi kuu ya Ottawa ya Kanisa Katoliki la Rumi katika Kanada iliagizwa hivi karibuni na mahakama ilipe $150,000 kwa kukosa kuchukua hatua juu ya lalamiko dhidi ya mmoja wa makasisi wayo. Kasisi huyo alishtakiwa kwa kushambulia kingono wavulana wachanga. Familia za hao walioshambuliwa “zilihisi zimelazimika kutafuta suluhisho la kiserikali kwa sababu, baada ya kwenda kwenye kanisa zisaidiwe baada ya mashambulizi hayo, zilifungiwa nje na maofisa, kutia ndani askofu mkuu,” akasema mwanasheria mmoja. Kulingana na Star, mwanasheria mwingine alitaarifu kwamba maofisa wa Kanisa Katoliki, wakiisha kugundua malalamiko ya watoto kutumiwa vibaya, kulingana na yaliyotangulia kutukia wameendelea kuacha makasisi katika uongozi wa kidini. Yeye alisema: “Badala ya kuwaripoti kwa polisi au kuwafukuza hapo kama shirika jinginelo lote, wao, kwa sababu ya uaminifu kwa wenzao, wamewahamishia kwingine kwa siri.”

UNYONYESHAJI MATITI HULINDA

Akina mama ambao hunyonyesha watoto wao wachanga matiti huwapa faida kubwa—mpunguo wa kuelekea kupata ambukizo—chakata kauli kikundi cha madaktari walioongozwa na Profesa Peter Howie wa Ninewells Hospital and Medical School, Dundee, Uskochi. Utafiti wa watoto wachanga wakati wa mwaka wao wa kwanza, uliotangazwa katika British Medical Journal, uliripoti kwamba watoto wachanga wanaonyonyeshwa matiti kwa majuma 13 ya kwanza ya maisha yao hupatwa na magonjwa ya matumbo yanayopungua theluthi moja ya yale yanayowapata wale wanaolishwa kwa chupa. Pia kunyonyesha matiti hutokeza mpunguo kama huo lakini ulio mdogo zaidi katika matatizo ya upumuaji. Madaktari hao walikata kauli kwamba ili watoto wapate faida hizo, akina mama “wapaswa kudumisha unyonyeshaji matiti kwa angalau miezi mitatu.”

KUTEKA NYARA MAGARI

Kwa kuwa motokaa nyingi zimewekwa mifumo ya kuzuia wizi, wezi sasa wanafuata mtindo mwingine. “Wakiwa hawawezi tena kuvunja kioo tu kabla ya kuwasha motokaa isiyo na mtu kwa kuunganisha waya na kuiendesha, wezi wengi wa magari sasa wanapendelea kuteka nyara wenye magari wasio na habari wanapokuwa safarini au wanapoketi katika motokaa zao,” laripoti Saturday Star la Johannesburg, Afrika Kusini. Wezi wamejifanya kuwa maofisa wa polisi wakiwa katika motokaa zenye taa za buluu zenye kuwaka-waka. Baada ya kumsimamisha watakayemwibia, wanaiba gari hilo kwa kutumia bunduki. Motokaa nyingine zimeibwa wakati madereva walipokuwa wamesimamishwa na taa za barabarani au walipokuwa wakifungua milango ya motokaa zao. Polisi wanaripoti kwamba motokaa za kibiashara zimetekwa nyara kwa kusudi la kuiba bidhaa zilizomo ndani na pia motokaa yenyewe. Wameonya wenye magari wafunge milango yao, wasiteremshe vioo chini sana, na wawe chonjo zaidi wanaposimama penye taa au penye ishara za kusimama.

“HAKUNA SABABU YA KUADHIMISHA”

“Stanley Matthews, bingwa wa mpira wa miguu wa Uingereza mwenye kuadhimishwa zaidi, na ambaye pekee ametunukwa kuwa Knight of the Kingdom, haoni sababu ya kuadhimisha,” lasema gazeti la Brazil O Estado de S.Paulo. “Yeye aona njia ya ki-siku-hizi ya kucheza kuwa yenye kushusha moyo kwa sababu furaha ya mchezo huo sasa haipo.” Matthews, ambaye aliacha kazi-maisha yake ya mpira wa miguu wa kulipwa katika 1965 akiwa na umri wa miaka 50, aona kwamba wachezaji wa ki-siku-hizi hawana adabu na sifa za kiadili na ni wenye jeuri na ukosefu wa uaminifu. “Wachezaji wa ki-siku-hizi hucheza isivyofaa zaidi kushinda ilivyokuwa wakati wangu, na sehemu kubwa ya burudani na furaha haipo tena,” asema Matthews. “Kila kitu kimebadilika sana. Kabla ya Vita ya Ulimwengu 2, kama ulichezea timu ya taifa na ufukuzwe, hungeitwa tena kamwe. Ungezomewa na mashabiki wako mwenyewe.”

TAFSIRI MPYA ZA BIBLIA

Biblia yote au sehemu zayo sasa yapatikana kwa asilimia 98 hivi ya idadi ya watu wa ulimwengu, ikiwa imetafsiriwa kwa sehemu au yote, katika lugha 1,928 tofauti-tofauti. Gazeti la Kifaransa La Croix laripoti kwamba tafsiri 21 mpya za Biblia zilitangazwa katika 1989. Zinazotiwa kati ya tafsiri hizo ni lugha kama vile Tok Pisin, namna fulani ya Kiingereza cha Pidgin kinachonenwa katika sehemu za Papua New Guinea; Kitruk, kinachonenwa kwenye kisiwa cha Truk na visiwa vingine vya Pasifiki ya Kusini; Lahu, lugha isiyo ya Kichina ya Sino-Tibetan ya Asia ya Kusini-mashariki; na Bawm, inayonenwa katika Bangladesh. Sasa kazi inaendelea ya tafsiri katika lugha ya Lap inayonenwa katika sehemu za Soviet Union na Scandinavia, na katika Romany, lugha ya Wagypsy.

BROSHUA YA BIBLIA KATIKA LUGHA 192

Guinness Book of World Records chini ya kichwa chacho “Uchapaji Mbalimbali wa Juu Zaidi” chatia ndani kitabu Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele, kilichotangazwa katika 1968 na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc. Kufikia Mei 1987 kitabu Kweli kilikuwa kimefikia jumla ya hesabu ya nakala 106,486,735 zilizochapwa katika lugha 116, kulingana na kitabu Guinness. Hata hivyo, hivi karibuni, Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakigawanya broshua Furahia Milele Maisha Duniani! Broshua hiyo, iliyotangazwa katika 1982 na sosaiti iyo hiyo, yapatikana sasa katika lugha 192, na nakala zaidi ya 60,000,000 zimechapwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki