Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 7/8 kur. 26-28
  • Nawezaje Kuwa Mtunza-Mtoto Mzuri?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nawezaje Kuwa Mtunza-Mtoto Mzuri?
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mwamrishaji au Mtoa Utunzi?
  • Njia za Ustadi za Kutunza Mtoto
  • Kutumia Kanuni ya Kidhahabu
  • Kulinda Watoto Kutoka Madhara
  • Kwa Nini Ni Lazima Niwe Mtunza-Mtoto?
    Amkeni!—1992
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Ubora wa Kutia Adabu katika Upendo
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Kulea Watoto tangu Uchanga
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 7/8 kur. 26-28

Vijana Wanauliza. . .

Nawezaje Kuwa Mtunza-Mtoto Mzuri?

‘TUNGEPENDA uwaangalie ndugu na dada yako wadogo.’

Kwamba unaiona kazi hiyo kuwa usumbufu wenye kuudhi au ushuhuda wa kutumainiwa, wazo la kubaki peke yako na wachanga wako laweza kukufanya uwe na wasiwasi. ‘Vipi wakikosa adabu?’ Unaweza kujiuliza. ‘Vipi ikiwa kuna mtu anayeingia bila kukaribishwa au moto? Na vipi ikiwa mmoja wao aumizwa au awa mgonjwa?’

Una sababu ya kuhangaika. Zaidi ya yote, watoto si vitu tu wala vyombo vya michezo lakini ni watu wenye mahitaji ya pekee. Wao ni wenye thamani kwa wazazi wao na Mungu. (Zaburi 127:3) Kwa hivyo uwe unaangalia wachanga au unatunza watoto kwa ajili ya kulipwa, kutunza watoto ni daraka na kazi yenye kudai. Hata hivyo, ukiwa na mwelekeo sahihi na mpango mzuri, unaweza kufanikiwa.

Mwamrishaji au Mtoa Utunzi?

Vijana wengine huonekana kuhisi kwamba kazi ya mtunza mtoto ni kuwa mwamrishaji. “Dada yangu hangeniacha nifanye hili, na hangeniacha nifanye lile!” akalalamika msichana mmoja. “Nilijaribu kumfanya aache kunisimamia, na akanipiga kofi!” Mvulana mmoja mchanga asema; “Nimekuwa na ndugu na dada yangu wakubwa wakinitunza, na inashangaza jinsi wanavyoshika uwezo huu akilini mwao kwa haraka!”

Kutoa amri kwa ukali kama sajini huenda kukaonekana kama mchezo. Lakini wazazi wako wakijua—yaelekea hivyo—“utawala” wako kwa ghafula waweza kuwa na mwisho wenye kuaibisha. Mithali 11:2 yaonya: “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu.”

“Bali hekima hukaa na wanyenyekevu [wenye kiasi, NW], yaendelea mithali hiyo. Kiasi hutia ndani kujua mipaka yako. Na ukweli ni kwamba wazazi—si watunza mtoto—ndio wana mamlaka ya kimungu ya kulea na kuwapa nidhamu watoto. (Waefeso 6:4) Sehemu yako ni ile ya ulinzi na utunzi.

Njia za Ustadi za Kutunza Mtoto

Hili si kumaanisha kwamba watoto wanaweza kuachwa huru ili ujifurahishe ukiangalia televisheni au kusoma. “Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye”—na taabu nyingi kwa mtunza mtoto! (Mithali 29:15) Kwa matokeo mabaya, matineja mara nyingi hawashughuliki kwa ustadi na watoto wasio na adabu.

Kikundi kimoja cha matineja wa U.S. kilijaribiwa katika upande huu na kuulizwa jinsi wangeshughulika na hali ambazo kwa kawaida hutokea wakati wa kutunza mtoto. Kulingana na jarida Adolescence, asilimia 8 tu ya vijana walionyesha kwamba wangeshughulika na jambo hilo katika njia ambayo ingelingana na hisi za mtoto. Baki la asilimia 92 lilionekana likitumia njia zisizo na matokeo, kama vile kutoa amri, makaripio, na vitisho. Watafiti walimalizia kwamba wabalehe huwa na mwelekeo wa kukosa hisia katika uhusiano wao pamoja na wachanga wao.”

Unawezaje kushughulika na watoto kwa matokeo mazuri na kwa ustadi? Wachungaji Wakikristo wasihiwa: “Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.” (Mithali 27:23) Sawa na hilo, ni lazima ujitahidi kuelewa mahitaji na hisia za watoto wadogo unaowatunza. Pata kuwajua mmoja mmoja. Upesi utajua kwamba watoto wadogo hawana kipimo cha uangalifu, subira, au nguvu ya watu wazima. Badala yake, “watoto ni dhaifu,” (Mwanzo 33:13) Wanasitawi juu ya upendo na uangalifu lakini huenda wakachoshwa haraka na kukosa utulivu.

Kutumia Kanuni ya Kidhahabu

Basi, wakati mwingine, watoto huchukuliwa katika michezo yao na huenda ukashikwa na hasira. Wanaweza kujihatarisha wenyewe na mwenendo mzembe. Au wanaweza kukujaribu ili waone jinsi wawezavyo kufanikiwa bila kupata adhabu. (“Wakati mwingine mimi huwafanyia hila watunzaji wangu,” akubali Douglas wa miaka saba.) Wakati hili latendeka usiwe mwepesi kupoteza furaha yako. Tumia kanuni ya kidhahabu: “Watendee watu siku zote kama vile wewe ungependa wao wakutendee wewe,” Mathayo 7:12, The New English Bible.

Kumbuka, “ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,” na si muda mrefu uliopita pia wewe ulijiendesha vivyo hivyo. (Mithali 22:15) Kazia kurekebisha tatizo (“acha tusafishe kilichomwagika”) badala ya kumlaumu mtoto. Epuka kujighafilisha na ‘kunena bila kufikiri kama mchomo wa upanga.’ (Mithali 12:18) Kumwita mtoto “mjinga” au “mpumbavu” ni kumtukana na kwaweza kumwumiza mtoto. Mithali 29:11 (Today’s English Version) hutukumbusha: “Watu wajinga huonyesha hasira yao wazi, bali watu wenye akili huwa na subira na kujizuia.” Msichana mmoja Mkristo asema: “Wakati ninapohisi kupiga dada yangu mwenye miaka minane, natoa sala, na hiyo yanisaidia nizuie hasira yangu.”

Shida zaweza kuzuiwa wakati mwingine ikiwa unakuwa na mfikio unaofaa. Mwenendo mzuri wenye kuthawabishwa huenda ukakufaa sana badala ya vitisho vya adhabu. Pia, watoto yaelekea hawachoshwi na kukosa utulivu ikiwa utapanga utendaji ufaao ambao ni wenye kufurahisha, kama vile michezo ya kutumia akili. (Linganisha Mathayo 11:16, 17.) Labda wakumbuka mingine uliyocheza ulipokuwa mtoto—au unaweza kubuni mingine mipya. Unaweza pia kujaribu kusomea mtoto sehemu anayopenda zaidi ya vichapo Kumsikiliza Mwalimu Mkuu au Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia.a

Wakati mwingine watoto wanahitaji nidhamu. Lakini ni vizuri kuzungumza na wazazi wako unaloweza kufanya kuhusiana na hilo. Hilo ni kweli hasa wakati unapotunza mtoto kwa kuajiriwa. Nyingi za shida zaweza kuachwa hadi wazazi warudi. Pia unajasiria kuumiza mtoto (acha kando hasira ya wazazi) ukijichukulia mwenyewe kutumia nguvu zako za kimwili. Yaonya Mithali 13:10: “Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanoshauriana.”

Kulinda Watoto Kutoka Madhara

Barbara Benton aonya katika kitabu chake The Babysitter’s Handbook: “Mchanganyiko wa kutokuwa imara kwake, udadisi wake, na kukosa kwake uamuzi kwamfanya mtoto aanzaye kutembea apatwe na mambo mabaya ambayo yaweza kuwapata watoto. Unahitaji kuwa mwangalifu siku zote—na mwepesi—kumfanya awe na usalama.” Tineja Stephanie alijifunza jinsi hili lilivyo kweli. “Nilikuwa nikichunga mpwa wangu,” akumbuka. “Kwa ghafula akaanza kukabwa koo na Popsicle! ilinilazimu niivute kutoka kinywa chake, na niliogopa kweli kweli!”

Nyingi za aksidenti mbaya zaweza kuzuiwa ikiwa utaweka jicho lako kwa watoto. Barbara Benton adokeza hatua nyingine tena: “Fanya ziara ya kukagua ili kutafuta na kuondoa kabisa hatari zozote zilizoko.” Unapaswa kujua mahali pa sanduku la fyuzi, chombo cha kuzimia moto, na vifaa vya huduma ya kwanza. Jifunze jinsi ya kutumia vyombo vya nyumbani vizuri na kwa usalama. Unaweza hata kufanya orodha ya mambo ya kuzuia hatari kama vile madirisha (yamefungwa?), ngazi (hazina vitu hatari?), matundu ya umeme (yamefunikwa vizuri?), sumu na dawa (zimehifadhiwa vizuri zisifikiwe na wachanga?), kamba za umeme (zimekunjwa na kuwekwa mbali?), funguo za nyumba (seti ya ziada ili usijifungie nje?).

Unaweza pia kujitayarisha vilivyo ili kushughulika na dharura. “Nilijifunza katika darasa la kutunza mtoto shuleni na nikajifunza huduma ya kwanza kwa watoto na wanaojifunza kutembea,” asema msichana mmoja tineja. Labda masomo kama hayo yanapatikana katika shule yenu. Weka karibu orodha ambayo ina nambari za simu za polisi, idara ya moto, daktari wa familia, hospitali, na kituo kinacoshughulikia sumu. Jua jinsi ya kuwasiliana na wazazi wako na labda majirani ambao wanaweza kusaidia wakati wa hatari.

Ikiwa aksidenti au hali ya dharura yatokea, USIWE NA WOGA MKUU! “Mwenye hekima huizuia na kuituliza [roho yake].” (Mithali 29:11) Kwa mfano, mtoto aweza kumeza sumu. Mara moja julisha hospitali au kituo kinachoshughulikia sumu. Ikiwa hilo haliwezekani, soma kwa uangalifu mashauri ya onyo la sumu hiyo. Kuamua hali kwa utulivu ni afadhali kuliko kufanya jambo kijinga (kama vile kushurutisha tapiko) ambako kwaweza kufanya hali iwe mbaya zaidi. Na hata iwe yenye kuudhisha au labda kuiaibisha namna gani, hakikisha kwamba umeripoti majeraha yoyote au misiba kwa wazazi wa mtoto. Wao wana haki ya kujua lililotokea, na wanaweza kuamua ikiwa hatua zaidi zaweza kuchukuliwa.

Kutunza mtoto kwaweza kuonekana kama daraka kubwa sana—na ndivyo ilivyo. Lakini ni kiolezo tu cha yale wazazi wako wamefanya kwa miaka wakikutunza wewe. Kwa hiyo chukua kazi yako kwa uzito. Kadiri uendeleapo kupata ujasiri na maarifa, inaweza kuwa yenye kuthawabisha na kufurahisha kwako.

[Maelezo ya Chini]

a Vilivyochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

[Sanduku katika ukurasa wa 28]

Miongozo ya Kutunza Mtoto

Uwe mwenye Ufundi. Hakikisha malipo yako yamekubaliwa.

Wasiliana. Hakikisha kwanza lile linalohusika katika kazi zako.

Uwe mwenye kuwahi na mwenye kutegemeka.

Pata kuwajua watoto kimbele.

Jua masharti ya nyumba.

[Picha katika ukurasa wa 27]

Watoto wanahitaji uangalifu daima ikiwa watalindwa kutokana na madhara

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki