Kuutazama Ulimwengu
Mbinu ya Mlango-kwa-Mlango
Kulingana na gazeti la Madrid El Pai̇́s, mapadri na maaskofu Wakatoliki wanapitia matatizo makubwa. Wakizidiwa na mvunjiko wa moyo, wengine wanaacha ukasisi au wanatafuta kujiuzulu mapema. Kati ya sababu zinazotolewa ni ule upweke wa useja wa kulazimishwa. Maaskofu pia wana wasiwasi juu ya ukuzi wa vikundi vingine vya kidini. El Pai̇́s ilisema kwamba kadinali mmoja alidokeza kwamba wanaseminari wafunzwe “mbinu ya mlango kwa mlango ili kwamba waende nyumba kwa nyumba kama wafanyavyo Mashahidi wa Yehova ili kusadikisha watu wakubali imani ya Kikatoliki.” Kulingana na gazeti hilo, kadinali huyo aliongezea kwamba Kristo na mtume Paulo walishiriki kazi ya kuhubiri nyumba kwa nyumba.
Tahadhari ya Jengo Lililo “Gonjwa”
Kwa kuwa sasa ishara za ugonjwa wa majengo unaosababishwa na uchafuzi wa hewa ndani ya majengo imedhihirishwa wazi, mtu anawezaje kugundua tatizo hilo kabla watu hawajakua wagonjwa? (Ona Amkeni!, 11/8/88, uku. 30 na 12/8/88, uku. 29 za Kiingereza) Kwa kutumia mimea, wasema maprofesa wawili katika Chuo Kikuu cha Dartmouth. Wanadai kwamba vichafuzi vinaweza kufanya mimea ionekane migonjwa kabla kemikali hizo hazijafanya watu wawe wagonjwa, hivyo ikitoa onyo la mapema. Idadi fulani ya mimea huonyesha majani yenye kujikunja na yenye kufa au huonyesha ukuzi usio wa kawaida inapowekwa wazi kwa kemekali ambazo hupatia watu maumivu ya kichwa, kizunguzungu, na itokeze ishara nyingine ya majengo “magonjwa.” Zaidi ya kuwa nyepesi kuathiriwa, wao waongezea kwamba mimea huwa na bei rahisi kuliko vyombo.
Kufua Miisho ya Bunduki Kuwa Vibao vya Kuchezea Mpira
Katika mwaka wa 1990 serikali ya Afrika Kusini ilitangaza mpunguzo mkubwa katika matumizi ya ulinzi, kulingana na Financial Mail. “Wenye kuchunguza mambo ya kijeshi wanatabiri kwamba angalau Rand bilioni 1 [elfu milioni (Dola 400,000,000, za U.S.)] zaidi zitaondolewa katika makadirio ya matumizi ya ulinzi ya mwaka ujao,” likasema jarida hili la Afrika Kusini. Ili kuiweza hali hiyo ya kupungua kwa uhitaji wa silaha, kiwanda cha silaha kimeingia katika ushirika na viwanda vidogo ambavyo hutokeza bidhaa za biashara. Kiwanda kimoja cha kutengezea silaha “kimebadili mashini zake zilizotumiwa kutengezea miisho ya bunduki za mbao ili kwamba vibao vya kuchezea mpira vilivyo bora sana viweze kutengenezwa,” laripoti gazeti la Johannesburg The Star. Vibao hivyo vya kuchezea mpira vinatumika katika mchezo wa kiangazi ujulikanao sana katika Afrika Kusini na vimejaribiwa na kupata kibali cha mchezaji maarufu wa mchezo huo.
Vipepeo Wenye Kupungua
Ulaya ina aina 380 ya vipepeo wanaojulikana, theluthi moja zikiwa zinapatikana kwenye bara hilo pekee. Ripoti moja katika gazeti The European laonyesha kwamba “karibu wote. . .wamepungua kwa kiwango kikubwa na baadhi yao wakabiliwa na hatari ya kumalizika.” Nchi zinazoathiriwa zatia ndani Uholanzi, Ujerumani, Uswisi, na Uingereza. Nini ndiyo kisababishi? Ongezeko katika mazao ya kilimo, likihimizwa hasa na ukuzi wa Shirika la Ulaya, limeongoza kwenye uharibifu wa makao ya wanyama. Kulimwa kwa nyika, kukaushwa kwa mabwawa, utumizi wa mweneo mkubwa wa dawa za mimea, uharibifu wa nyua za vichaka, na usimamizi mbaya wa mashamba ya majani umezidisha hali mbaya.
Wahalifu Wachanga
Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Haki ya Japani, “watoto [wanasimamia] asilimia 57.4 ya washukiwa wote waliohojiwa au kukamatwa,” laripoti The Daily Yomiuri. Wastani wa miaka ya wahalifu wachanga imeshuka kila mwaka kwa miaka zaidi ya kumi. Gazeti hilo laongezea kwamba “kulingana na uchunguzi huo, zaidi ya watoto asilimia 70 watukutu walifanya uhalifu wao wa kwanza kati ya miaka 13 na 15. Kati ya wale waliozuiliwa angalau mara mbili, wengi wao walifanya uhalifu wao wa kwanza kabla ya umri wa miaka 10.” Uchunguzi huo ulifunua kwamba wengi wa vijana watukutu katika Japani wana wazazi wasiotoa adhabu ya kutosha. Wanatoka kwenye familia “zisizo na uwezo wa kupashana habari katika njia ya maana.”
Biblia ya Kimongoli
Watu wenye kusema lugha ya Kimongoli katika ulimwengu sasa wanaweza kupata sehemu ya Biblia katika lugha yao wenyewe. Ilimchukua mwanachuo Mwingereza John Gibbens miaka 18 kumaliza tafsiri yake ya Maandiko ya Kigiriki. Kulingana na Bw. Gibbens, “lugha ya Kimongoli ndiyo lugha ya kitaifa ya mwisho kupata Agano Jipya katika ulimwengu,” laripoti Asia Magazine. Hata hivyo, gazeti hilo linaongeza kwamba idadi ya wale wanayoiamini Biblia “inakadiriwa kuwa si zaidi ya kumi na wawili kati ya watu milioni 2.2 wanaoishi katika Jamhuri ya Watu wa Mongolia.” Sosaiti moja ya Biblia katika Uingereza yaeleza kwamba kuna upendezi unaokua katika Biblia kama kitabu bora cha ulimwengu.
Kutopatana kwa Wakatoliki
Gazeti la Kifaransa Le Figaro laripoti kwamba kulingana na uchunguzi wa hivi majuzi nchini kote juu ya maoni ya Wakatoliki Wafaransa, wengi wa Wakatoliki Wafaransa (asilimia 57) hawakubaliani na mafunzo rasmi ya kanisa yanayohusu adili. Walipoulizwa juu ya uaminifu wa ndoa, kupanga uzazi, kutoa mimba, na uhamishaji mimba usio asili, asilimia 60 walisema kwamba kanisa halipaswi kuweka sheria katika mambo hayo. Uchunguzi huo ulifunua kwamba asilimia kamili 69 ya Wakatoliki Wafaransa wasema kwamba wanakubali, kwa kanuni, kuwa na uhusiano wa kingono kabla ya ndoa. Isitoshe, asilimia 49 walisema kwamba walikuwa wakipendelea kule kuondolewa kwa useja uliolazimishwa mapadri Wakatoliki, na asilimia 51 walifikiri kwamba wanawake wanapaswa kutiwa ndani ya ukasisi. Kwa kupendeza, ni asilimia 8 pekee waliofikiri kwamba Kanisa Katoliki bado ni jaminifu kwa mafundisho ya Yesu.
Ibada ya Kishetani
Ripoti juu ya ibada ya kishetani, ambayo ilikuwa imetupiliwa mbali zamani kuwa haiwezekani, zinatokea mara nyingi kwa wingi na mwendelezo wenye kufadhaisha,” laripoti The Globe and Mail la Kanada. Ripoti hizo zinatia ndani kuudhiwa kingono, ulaji wa nyama ya mwanadamu, na dhabihu za wanadamu. Wengine hudai kwamba wahanga wa dhabihu za kibinadamu wanatolewa kutoka kwenye watu zaidi ya 50,000 wenye kuzurura na wasio na makao ambao huripotiwa kila mwaka katika Amerika Kaskazini kuwa wametoweka. Pia kuna hoja zinazotolewa kwamba kuna watoto wanaozaliwa na kufichwa kwa kusudi la kuwatumia katika dhabihu za kibinadamu. The Globe and Mail linaongezea kwamba katika “Kanada, mkadirio wa watu 2,000 wamejitokeza wakidai kwamba wamedhulumiwa katika ibada za kishetani.” Ili kukabiliana na tatizo lenyewe, idara za polisi katika sehemu fulani fulani za Kanada zinatia ndani ibada ya kishetani katika mfululizo ya masomo yao. Maofisa wana wasiwasi kwa “uvutio wa kishetani juu ya vijana.”
Mafuta Yenye Afya
Uchunguzi wa hivi majuzi ulionyesha kwamba hesabu ya watu wanaopatwa na ugonjwa wa moyo wanoishi kando ya fuo za bahari za Japani ni ndogo kuliko wanaoishi katika bara. Sababu? Asiaweek laripoti kwamba utaratibu wa chakula ulio na wingi wa chakula cha baharini “umeunganishwa na kule kupungua kwa magonjwa yanayoathiri moyo.” Aina za samaki kama salmon na trout hasa wana kiasi kikubwa cha mafuta halisi yaitwayo omega-3. Imeaminiwa kwamba aina hii ya mafuta inaweza kupunguza kadiri ya triglycerides na ipunguze ‘ushikamano wa damu’— uelekevu wayo wa kugandamana na hivyo labda kuziba mishipa ya moyo,” lasema Asiaweek. Wengine hudokeza kwamba omega-3 huenda hata ikazuia magonjwa mengine, kama vile uyabisi, kansa ya matiti, ugonjwa wa figo, na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.
Mwuaji wa Miti Namba Moja
Kulingana na gazeti la Munich, Süddeutsche Zeitung, misitu ya Ujerumani imechukua mkondo kwa mabaya zaidi. Asilimia 56 ya misitu ya Ujerumani inasemekana kuwa imeharibiwa. Miti ya misunobari hasa imeathiriwa, kukiwa na matokeo mabaya kwa vilima, ambapo mizizi yenye vina virefu huwa na sehemu ya maana katika kuzuia maporomoko ya ardhi na mmomonyoko wa udongo. Süddeutsche Zeitung lataja kwamba kwa sababu ya kiasi kikubwa cha vitokezi vya magari katika Ujerumani, “wahifadhi wameomba tena serikali ifanye jambo kuhusu yule ‘mwuaji namba moja,’ gari.”
Kujifunza Nyumbani
Mamia ya maelfu ya wazazi katika United States wanawafunza watoto wao nyumbani badala ya kuwapeleka shuleni. The New York Times laripoti kwamba kulingana na makadirio fulani, kufikia watoto 500,000 wanafunzwa nyumbani. Uchaguzi huo unaenea kati ya wazazi wanaohangaishwa na “dawa za kulevya na uhalifu katika shule za umma na juu ya kushuka kwa ubora wa waalimu.” Kulingana na Times, waelemishaji wanasema kwamba watoto hawa “wanaachwa chini ya wazazi wenye kutaka mazuri lakini wasiohitimu.” Msemaji wa kike kwa ajili ya Shirika la Kitaifa la Masomo ya Nyumbani alikubali kwamba “masomo ya nyumbani si ya kila mtu.” Halafu akaongezea kwamba: “Lakini pia hata ya shule za umma.”
Tatizo la Kugharimia Makathedro
Ingawa Kanisa la Uingereza ndilo la pili kwa kuwa na umiliki wa mashamba katika Uingereza, inapata wakati mgumu katika kugharimia makathedro yake mengi. Kulingana na gazeti la Manchester Guardian Weekly, “kuna ishara kwamba watu wamechoka na miaka ya kutegemeza majengo hayo mazuri yanayoporomoka.” Maofisa kadhaa wa kanisa wanadokeza kufunguliwa kwa mikahawa kwenye wanja za kanisa au kupanua maduka ambayo tayari yapo hapo; katika York, maofisa wa kanisa waliongeza maradufu kodi za maduka ya huko. Juhudi za aina hiyo zililaumiwa kwa kadiri tofauti-tofauti kutoka kwa viongozi wa kanisa. Lakini Dkt. Robert Runcie, aliyekuwa Askofu mkuu wa Canterbury, hivi majuzi aliandikia serikali ya Uingereza barua akiomba msaada wa kifedha kwa ajili ya kanisa. Ile kathedro ya Ely ina suluhisho rahisi zaidi. Inatoza wageni pesa za kiingilio.